Mke wangu atasababisha nife kwa kweli...

Mke wangu atasababisha nife kwa kweli...

Hata Mzee Yusuphu kabla hajastaabu taarabu hakuwa bwege hivi
 
Hayo ndo matokeo ya kumpenda sana KE,kuliko yeye anavyokupenda.Eb jarb kuficha hisia zako kumpima kama anakupenda au la!.
 
🙁😡 Nimeumizwa na kuudhika sana na maneno ya mijanadume mingine humu ndani. inaonekana wengi hawajui mapenzi wanaendekeza mfumo dume tu na ubabe. mapenzi ni kuaminiana. namwamini na nampenda sana mke wangu. maisha ya sasa ni kusaiiana na kupeana mapenzi shatashata. sijaona ubwege wangu ni nini hapo.kumpenda?kumsaidia kazi?au kumwamini? acheni hizo msipende tu kuvamia ndoa za watu na kuwaona mabwege.

yeye ni malkia wangu, kwa nini nimtese?sipendi kumuudhi abadani. nlitegemea wanaume wenzangu pia mjifunze kuwapenda wake wenu.naona wengine mmenishukia.nimesikitia mpaka machozi yamenitoka...watu kumbe kweli wana wivu na hata yeye huwa ananambia wengi hawapendi maisha tunayoishi. wanataka kutugombanisha tuachane watucheke. bwege mwenyewe mi siyo bwege na wala sijalimbwatishwa kitu. mtu akisema amechoka hatak ufanya tendo la ndoa week mbili au 3 unamlazimisha? si ndo kubaka huko?

nimeumia sana kwa baadhi ya maneno ya watu. machozi yananitoka tu.
Na Bado utakunywa diesel badala ya mafuta ya taa,,, yaani wewe ni mbwete kabisa
 
Umemaliza kuandika skript au tusubir sehemu ya pili?
 
Toka nimemuoa huu ni mwaka wa 2 nampenda sana kiasi hata yeye anajua kuwa kwake sipumui, sihemi yaani nakuwa kama fala tu. Kiukweli nilihangaika sana kumpata nimemfukuzia kama miaka 2 hivi siku moja kama ndoto akakubali basi tukaanza uhusiano ila aliniambia nisifikirie kabisa habari za kukamuana mpaka ndoa basi nikawa mimi nauza naye sura tu. Ananipigia simu nimpeleke au nikamchukue sehem fulani siku nyingine akiwa ana kunywa na rafikize wa kike na kiume then ananiambia nikamchukue naenda bila hiyana nampeleka kwake.

Kipindi chote hicho alikuwa akinitambulisha kwa rafikize kuwa mi ni rafikiye nilimuuliza why akanambia hatujawa wachumba so hawezi niita mpenzi wakati bado, ila nilikuwa naenjoy sana kuuza naye sura maana ameumbika sana huyu dada alikuwa anaweza nipigia simu hata saa nane usiku nikamchukue klabu naenda namrudisha kwao alikuwa anapenda sana kwenda klabu na rafiki yake anaitwa Benny. Huyu jamaa alikuwa rafiki yake sana na alinambia hamna wa kuwatenganisha urafiki wao mpaka leo huwa ananiaga anaenda kumsalimia Benny.

Sasa nimemuoa yaani napata unyumba wakati mwingine kwa week mara moja tu nami sipendi kumsumbua sana maana sipendi niichoshe sehemu yake ya siri tena nikipiga moja tu anasema basi anataka kulala mi mashine inakuwa bado inataka tena but siwezi mlazimisha, hivyo nakunywa mafuta ya taa hamu inaisha nalala siku nyingine anarudi amechoka sana ananambia nimletee chakula room ale akila anajitupa kitandani basi natoa vyombo na kusafisha meza tunalala hapo hataki hata nimkumbatie na kiukweli kukumbatiana nako kuna joto sana basi namwacha mke wangu mpenzi alale.

Mimi ntakufa tu kwa mapenzi maana nampenda huyu mwanamke acha kabisa salary yangu yeye ndo huenda kutoa nlimpa kadi ya bank na password alibadilisha akaweka anayoijua yeye tu ili nisiwe natoa hela halafu naonga michepuko so huwa anatoa kkisha ananipa kiasi ya nauli kwa mwezi. ananonekana ananipenda ana wivu sana. akirudu toka kwenye mizunguko yake huwa anaoga tu na kuangalia tv mimi inabid ndo nimwandalie kila kitu kwa jinsi tunavyopendana.

kuna siku alirudi amelewa tukalala naye akawa maskini anaota anamtaja benny nikamwonea huruma jinsi ambavyo analalamika kuwa benny anamuumiza afanye polepole ikabidi nimuamshe ili asiumie zaidi nikamwambia ndo akasema huyo benny alikuwa anamkuna mgongoni hivyo alikuwa anamwambia amkune polepole. basi ndo hivyo mapenzi yangu jaman na huyu mwanamke yamfika mlima kilimanjaro...yaani tunapendana kufa.
Hongera mkuu...wasiliana na Shigongo...
 
Sasa nimemuoa yaani napata unyumba wakati mwingine kwa week mara moja tu nami sipendi kumsumbua sana maana sipendi niichoshe sehemu yake ya siri tena nikipiga moja tu anasema basi anataka kulala mi mashine inakuwa bado inataka tena but siwezi mlazimisha, hivyo nakunywa mafuta ya taa hamu inaisha nalala siku nyingine anarudi amechoka sana ananambia nimletee chakula room ale akila anajitupa kitandani basi natoa vyombo na kusafisha meza tunalala hapo hataki hata nimkumbatie na kiukweli kukumbatiana nako kuna joto sana basi namwacha mke wangu mpenzi alale.
Pole sana ndugu
 
Mkuu usikasirike kubali tu heshima ya ubwege na kwanza umeshapitiliza toka kwenye ubwege. Hakunaga kama kama wewe kwa VIP treatment unayomfanyia mkeo. Mbona unakubali Benny ammege mkeo? nawe unasema unamwamini mkeo arudi usiku wa manane kachoka hataki kukupa tunda? Kama unakataa kuitwa bwege mbona unakiri kuwa mkeo siku moja atasababisha madhara kwako? funguka mkuu!
 
Brother samahani kwa hili " Lakini kama kweli basi una akili NUSU " zinazotosha kuvaa tu na kumpikia mkeo . By the way Pole ndo kupenda kwenyewe Japo wenzio hatufanyi unayoyafanya wewe😀😀😀😀😀🙂🙂😵
 
Hhahahaha TEA WITHOUT SUGAR PLEASE hii movie unatarajia kuizindua lin?
 
Back
Top Bottom