Mke wangu askari Polisi bado anawasiliana na mzazi mwenzie ambae pia ni askari Polisi

Na wewe raia wasiliana na ex wako ambaye ni raia
Sio X tu mkuu ila ninamtoto kabisa ila nimeweka utaratibu kwenye Shule husika..
Nalipa ada mwaka mzima...
Bima ya mtoto ipo ..
nikitaka kumuona mtoto namfata Shuleni .
Sina mawasiliano na Mzazi mwenzangu kabisaa ...
Nimeamua kujenga mazingira magumu ili nisimkwaze mke wangu ..
Taarifa za mtoto wangu ni rahisi kuzopata kwa Mama angu mzazi kuliko kwa mzazi mwenzangu...
ila kwa mwenzangu naona anachukulia simple tu
 
Mkuu wangu asante kwa Ushauri ila bado siamini kuoa mwanamke mwenye mtoto kama ni dhambi...
Kwa sisi ambao tumepevuka kiakili sidhani kama naweza kusumbuana na vitoto vya kidacho cha 4 ...
Mimi niliangalia mwanamke ambae tutaelekezana tutakatazana na kuambiana ukweli...
Mwanamke ambae anajua Mume ni nini...
Maisha inatakiwaje...
Huyo ndio mwamamke niliekuwa namtafuta...
Wengi wenye watoto akili zinakuwa zimepevuka na kutambua majukumu yao ....

Kuoa single mother ni sawa na kuoa mwanamke aliyemaliza University College kielimu kwani ni mwelewa wa mambo mengi ikiwemo na jinsi ya kuchepuka salama bila kukuletea maumivu ndani ya nyumba kama hivi unavyoelezea lakini ukweli unabaki palepale yaani lazima wagegedane na ex wake wakati wowote pale wanaposikia mate yamejaa mdomoni...No way!
 
Ukweli ni kwamba mawasiliano mengi huwa kwa issue ya mtoto tu..
Kama kunamengine kiukweli sijawai kuyaona ..
Huwa nayafumania kwenye simu ya mke wangu maana tunatabia ya kushare simu..
Hapa ndipo unapokosea !!. Achana na simu ya mwanamke kabisa.
 
Mimi nikushauri kitu mkuu, kikawaida sisi wanaume tuna wivu hasa inapotokea unaona mawasiliano ya mke wako na mtu anaedaiwa kuwa alikuwa na mahusiano nae.
Mimi binafsi sipendi hii, kwa sababu zozote tu huwa hainifurahishi. Kwa mfano mimi nimetoka kazini,naketi kwenye chakula cha usiku mara simu inapigwa na ninasikia sauti ya mwanaume eti anaulizia habari za mtoto,kiukweli sio nzuri hata kama ipo wazi kuwa yule bwana ni baba wa mtoto.
Cha kufanya,mwambie mkeo kuwa unauwezo wa kumuhudumia huyo mtoto kwa mahitaji ya shule na pale panapo lazimika chochote utawajibika, hilo swala la simu kila mara halikupendezi, mwambie ukweli tu, yeye ni mke wa mtu na huyo mtoto ni mmoja wa familia hivyo atapata huduma zote kama watoto wengine.

Pawepo na heshima,sio kila saa mtu anapiga simu utazani anapiga kwa hawala yake eti kisingizio mtoto, au kama anaona mtoto atapata tabu namna ya kuishi pasipo mawasiliano,basi amchukue mtoto. Au amfungulie akaunti pesa iwe inaingizwa kwenye akaunti na itatumika kadri itakavyo kusudiwa ,ila hapo uwe makini kwani inaweza kupelekea kuzolota kwa mapenzi au mahusiano yako na mkeo,
 
Mwambie ampeleke mtoto kwa wazazi wake mwanaume na amtafutie shule ya boarding
 
Jibu swali langu kwanza
Unamiaka miwili sasa naye

Utampa mimba lini akuzalie

Mama mumewe hazai na yule mwingine akirudi kumpa mimba tena itakuwaje?

Au sasa hivi mkeo akipata mimba utahisi yako au siyo?

Nimeweka na sahihi kabisa
 
Pole sana, ila usijipe moyo kwakuwa leo mpo poa na mke wako na mnapendana sana , hapo ulipo ni sawa na kuwa kwenye ardhi yenye tabia yakupata mlipuko wa volcano , hivyo jiandae muda wowote kufumania au kupata habari kwa niia yoyote kwamba mke wako ana move na baba mtoto wake
 
"Wp rara hapo nikurenge aisee" Wp anachojoa kila kitu, kweli mapenzi upofu, yaani unaoa single mother halafu askari.
Pambana na maisha yako huenda ukainuliwa.
 
Nilichoshindwa ni kuanza mechi mpinzani akiwa anaongoza 1 bila, japo nna uhakika wa kusawazisha! Ila hofu ni kwamba mpizani atakuwa na faida ya goli LA ugenini so aggregate ikanisumbua kichwa km hivi!
 
Habari zenu wanajamvi wenzangu...
Nimeoa askari polisi miaka miwili iliyopita, japo nilimkuta mwenzangu akiwa na mtoto wa kiume..
Kutokana na maelezo yake Baba wa mtoto wake ni Police tena mwenye cheo kikubwa tu ..
Walishawai kuishi nae ila alimiacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine na kupelekea kuachana ..
Ila uko alipooa hakuwai kupata mtoto mwingine ..
Hivyo basi jamaa uyo amekuwa busy na kumfatilia mtoto kulipa ada na garama za mavazi ...
Sina wivu ila najaribu kutaka ushauri kwenu nyie wakubwa zangu mlionizidi kwa kila kitu kuhusu haya mahusiano ...
Vile vile sina tatizo na mke wangu..
Tunaheshimiana Tunapendana lakini mwisho wa siku nahitaji kupata ushauri wa tahadhari ili baadae yasinikute ...Naomba kuwasilisha ..
wapigie simu dada zako au shangazi zako wakutafutie binti mbichi ukaoe.kwa nini unaoa mwanamke ambaye ameshazalishwa?
 
Mkuu najarubu kutafakari ushauri wako ..
inamaana Mwanamke mwenye mtoto afai kuolewa tena...
Istoshe mke wangu huyu hajawai kuwa na ndoa na uyo Mzazi mwenza..
Swala la kuchunguza mpaka kufunga na ndoa halikuwa ni swala la siku moja ..
Vingi nilichunguza na nikajiridhisha ..
Wasiwasi wangu ni kwamba isifike mahali nikaanza kununua magunia ya mkaa ilhali sina jiko la mkaa ...!!
Uwo ndio wasi wasi wangu ..
Nikiamini kwamba kunawahenga wenzangu waliputia changamoto kama hizi na wakafanikiwa ...
Mwamba mbishi wewe, hivi unaposema ulichunguza hapo kabla ulibaini kuwa hawatawasiliana? Tatizo la watu kama ninyi ujana wenu umewapita bila ya kuwa na experience ya wanawake. Hakuna mtoto wa kiume aliyepitia ujana wake kwa kuwaelewa wanawake vizuri atathubutu kuoa single mother. Vinginevyo tuambie labda umefuata kitonga may be wewe ni mtu mission town ukaona afande ni up class kwako kumbe wenyewe wananuka njaa.

Nakuelewesha tu. Single mother huwa wanaolewa na over aged single men ambao utakuta naye anafurushi la watoto anatafuta tu mwanamke mlezi wa watoto wake.
 
Tatizo mkuu tumeshafunga ndoa na tayari tumejaliwa mtoto wa Kike ...
Hana shida tatizo ni hayo mawasiliano tu mkuu...
Naweza kumpiga marufu
Naweza peleka mtoto kwa Baba ake
Lakini naisi bado naitaji ushairi mzuri na wenye busara ili ndoa yetu isije kupata doa siku za mbeleni maana mimi na mke wangu hatujashindwana kwa chochote kile ..
Tunasikilizana fresh tu
WAZAZI HUWA HAWAACHANI MILELE. NA JAMAA AKITAKA HATA GEMU ATAPEWA. HIYO NDIYO GHARAMA YA KUOA SINGLE MOTHER. HUYO NI MZAZI MWENZAKE NA HUWEZI KUMKATAZA. KUNA JAMAA HUMU ALISEMA USIOE SINGLE MOTHER, JAMAA WAKAMPONDA SANA ILA NILIMUELEWA SANA. NDOA YA MASINGLE ZINAVYOKUWA HIVYO, KUWA MVUMILIVU TU
 
Back
Top Bottom