Mke wangu anaomba nimpe ruhusa akacheze harusini(ukumbini)

Mke wangu anaomba nimpe ruhusa akacheze harusini(ukumbini)

Mkuu sio kwamba namchunga, hiyo harusi yenyewe mimi pia nimepewa kadi na nitahudhuria ila hofu yangu naona mke wangu kunengua hadhari itanipa tabu

[emoji23][emoji23][emoji23] safi sana mkuu inaelekea heshima kwako unaipa kipaumbele ila suala la kucheza sio baya ila asipitilize sasa
 
Hakuna tatizo ..muache akacheze kwani...kwenye harusi hua wanacheza vibaya. Si step tu za hapa na pale...Sasa wivu hapo wa Nini?
 
Hebu ngoja nipiyie nyuzi au comments zako za zamani kabla ya kuweka chochote hapa...
 
Kuna wimbo fulani wa Marquis wanaimba

"Na mume wangu yuko hapahapa, ameniruhusu kucheza muziki wa kwetu..."
 
Image ya mke wangu pamoja na mimi nahisi itaporomoka mkuu
Mke anachezaje harusini, napata tabu kidogo
USIMRUHUSU KUCHEZA A.K.A KUKATA VIUNO MBELE ZA WANAUME WENZIO. HUYO NI MKE WA MTU LAZIMA AJIHESHIMU. NDIO MWANZO WA KUVUNJIWA HESHIMA NA WEZI WA WAKE ZA WATU... UTASIKIA SHEMEJI UMEPENDEZA...MARA SHEMU UNAJUA KUCHEZA..HAPO UTAAMBULIA MANYOYA.

HALAFU HUYO MKEO NA YEYE INAONEKANA ALIRUKA STAGE NDIO MAANA ANAKUSUMBUA KUTAKA KWENDA KUNENGUA HARUSINI WAKATI NI MKE WA MTU..ATAKUSUMBUA SANA..
 
Usimruhusu mkuu mimi ndio mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya hiyo harusi mkeo kapanga amwage radhi kabisa ukumbini
 
Hivi majuzi mke wangu aliniletea ombi akihitaji nimpe kibali cha kwenda kucheza katika harusi ya kaka wa rafiki yake inayokwenda kufanyika mwanzoni mwa mwezi November

Wakuu hivi ni sawa mke wa mwanaume kwenda kucheza kwaito na mastep mengine mbele za watu?

1. Mke kucheza mziki mbele za watu sio tatizo kubwa. Ila kumbuka harusini ni sokoni, kucheza kutamfanya aonekane na hivyo kuwa bidhaa.yenye kugombewa na wateja. Ni kweli kuwa kila eneo sokoni ila kucheza harusini ni Soko Kuu la.Kariakoo

2. Kwanini ang'ang'anie kucheza ktk harusi ya KAKA WA RAFIKI YAKE? Kuna lipi kubwa? Walikuwa wapenzi hao hivyo anakwenda kushangilia x mpenzi kuoa. Pia kumnanga mke kuwa ajiandae tu kushirikiana naye kufaidi dhakari.

Amua kwa busara ukijua kwanini acheze, faida na hasara zake. Ukiona unaweza beba changamoto na /au matatizo yatayojiri baada, mruhusu tu. Kumbuka ni kucheza tu

Bazazi!
 
Inategemea na wanacheza nini.

Mimi niwekwe kwenye kamati nitachanga hela wanayotaka ila sio kuwa kiburudisho cha wageni[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Mruhusu mke wako maana hadi amekuomba ni kwamba amejiona anaweza kwenda kuburudisha na kusheheresha sherehe.
Kumbe hupendi niiangalie chura yako ikinesanesa?
 
Haya mambo nahisi kwa mke wangu naelekea kutomruhusu kwa nionavyo but thanks kwa ushauri wako
Inategemea kwenye jamii wewe, ni nani, bado siko kwenye ndoa ila napata picha kama ningekuwa nimeolewa, siwezi Fanya Hiki kitu

Hili swala Mkeo ilibidi ajitathimini kabla hajakwambia, ajuwe status yako bwana. Ila kama mkeo ni wale wa Dada wa mwananyamala,ndivyo walivyo, mwache aende.

Ahaaa kama nakuona Mr cha wivu,
 
Habari wakuu
Nimepata changamoto ya kimaamuzi hapa katika familia yangu hii ambayo nimedumu tangu nioe ni yapata mwaka mmoja sasa

Hivi majuzi mke wangu aliniletea ombi akihitaji nimpe kibali cha kwenda kucheza katika harusi ya kaka wa rafiki yake inayokwenda kufanyika mwanzoni mwa mwezi November
Jibu nililompa ni kwamba asubiri nitampa majibu lakini imekua kero muda wote anakumbushia nimpe ruhusa kwani muda huu wameanza kushiriki mazoezi ya steps na nyimbo mbalimbali

Wakuu hivi ni sawa mke wa mwanaume kwenda kucheza kwaito na mastep mengine mbele za watu?

Naombeni majibu ili Leo apewe majibu maana muda huu ndio narudi nyumbani
Usisikilize ushauri usio na msingi mkuu, wengine wanadai mke usipomchunga ndio huchapiwi. Ukweli ni kuwa kama humpendi ndio utamwacha ajichanganye hovyo, hata wakimlala huko huyojua kwa sababu uliingia kwenye ndoa kama fashion tu. Ni ushauri wa ajabu mno.

Mke ameolewa akatengwa na dunia kwa ajili ya mume. Kwa hiyo imempasa kukusikiliza wewe asilimia mia moja na si ushauri wa vibaka wa nje. Mpe jibu moja tu, awaambie mume wangu hataki nicheze hata makwaito. Wewe ndio mwenye mke, usiishi kwa kufuata jamii iliyoharibika akili. Wako mabinti wengi tu wanawza kuziba pengo hilo, unless labda kama mkeo ni bingwawa hiyo kwaito, jambo ambalo si jema.
 
Asante sana mkuu kwa ushauri murua
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom