Mke wangu ananiumiza kichwa



Rafiki yangu aliolewa na wakina ngosha, alisomeshwa mpaka masters, walivyoachana ngosha alilia 'ee nimewasomeshea'.
 

Bora umefungua umejua kuliko ungejitia kuendelea kumwamini. Heri Ukweli Mchungu kuliko Uongo unaovutia. Hapa hata ukiamua kuendelea nae hata aje kufanya nini haitakuumiza mana ushajua ni mtu wa aina gani.
 
Hizo ndio zao mkuu,wengi wameshatendwa nao,sio mtu wa kwanza wewe kuweka thread ya aina hii hapa JF,kama ni msomaji mzuri wa post zinazohusiana na mahusiano.
 
Ndugu jaribu kutumia tafsida basi maana kuzungumza matusi waziwazi tunakuwa hatuna tofauti na wahuni wa vijiweni...inawezekana au isiwezekane kwamba katembea nao kwani sijaona message hata moja ambayo kijana anaongea kufurahi kukutana faragha na kuinjoi...zaidi ni message za kipuuzi za udhalilishaji kwa Mke wa mtu. Like nipo kitandani, nakula hiki, napika, nimetoka kuoga ndio navaa, ninekumisi sana, nataka kusikia sauti yako, una ratiba gani leo, unafanya nini Sasa hivi, nataka nikuone, mume wangu amerudi tutachat kesho, nipo kitandani baridi, natamani ningekuwa karibu yako nikupe joto n.k
Sijaona message ya direct inayoonesha wamefanya ngono na hao vijana but bado suala linabaki palepale kwa Mke wa mtu kuna aina ya message hutakiwi kuchat kabisa....ningeiona message ya moja kwa moja ningeenda kumpumzisha kwao ila sijaiona hivyo sina ushahidi direct kama amefanya au ni chatting tu za kipuuzi


Tena huyo mpuuzi mmoja ambae ni underground artist anamshawishi Mke wangu aende Mwanza kwenye show yake halafu bila aibu anasema mi sijui kuimba wala kucheza, jamaa anamwambia upo na mie nitakufundisga kuimba na kucheza kwani hakuna aliyezaliwa anajua kusoma. Akasema mume wangu hawezi niruhusu ndio chalii anamwambia muage unaenda kusalimia ndugu zako kisha unakuja kwangu...upuuzi upuuzi wa kipumbavu huku Mimi navuja jasho analagaiwa na vivulana visivyokuwa na mbele wala nyuma.
 
Hata mimi kuna nyau mmoja alifanya hivo hivo
Kila siku anagawa namba yule kenge
 
kama hii story ni ya kweli pole sana ila nimesoma btn lines kuna sehemu umedanganya umesema ulimkuta darasa la saba ukamuoa na akasoma QT na diploma na kupata mtoto katika kipindi cha miaka minne. Ukiangalia vizuri muda unakinzana na alivyovipata content ya story sina tatizo nayo. Ushauri piga vibao mtimue harudi kwao ili aone ukubwa wa kosa na pia wazazi wake wajue nini binti yao anakosea ili wamfunze. Akiomba radhi msamehe ila atajua wewe huna mzaha. Mambo ya kukaa nae hotelini na kuongea nae kistaarabu achana nayo utaonekana boya na utaendelea kuchapiwa. Onyesha hasira zako na action pia
 
Pole ya kawaida hayo, ongea nae delete hiyo account Facebook, jipe muda maumivu yapungue msamehe maisha yaendelee.....
Kirahisi hivyo! He! Kwetu wana methali inasema "Akushabilila katafile tomanya nka akelekela" literal translation: Mtu anayetembea na mke/mme wako kama bado yuko hai huwezi jiaminisha ameacha! Msamehe, ameacha au jifanye hakuna jambo kama hilo? Anyway ni vizuri kuvumilia lakini inahitaji moyo! Ushauri wako ni mzuri anyway
 
Unaweza kuta hajawahi toka nje ya ndoa ila ni tabia tu za wengi pindi anapoingia kwenye mitandao na kuanza kuchat na kila mtu ilimradi anapoteza mda tu.

Wengi wa binadamu sasa unaweza mkuta anachat na mphilipino huko Manila na hata ndege hajawahi panda lakini kakazana tu.

Sio wote wanafanya kweli ila huenda amekuwa bored inabidi uwe unamtoa out (kama hamtoki) ili ajisikie.

Utakuta hata wewe unachat na marafiki hewa 1000 lakini in reality hujatembea nao hata wawili katika hao.

Take it easy
 
Very well said mkuu funzadume
 
Story nyingi za humu huwa ni fictions!
 
Mkuu pole sana kwa mkasa huo, ila tambua hakuna Jipya chini ya Jua yote Marudio ila Kabla halijakupata utaliona Jipya, mwenye maamuzi ni wewe uendelee kuwa nae au umuache. Jipe mda wa kutafakari na kuchunguza kwa undani juu ya kile ulichokiona je kina uhalisia ktk Matendo.

Naamini kama umemkuta sio bikira jua wapo watu waliokuwahi kabla na hivyo kwa vyovyote vile ukiona anasaliti ndoa jua sio kitu cha kushangaa na kustaajabisha.
 
Hata ukisema unaendelea kukaza ni kujiumiza tu moyo na kujipa stress kama kafanya kafanya tu haibadiliki
Unabaki na option mbili tu
1:huwezi kumsamehe, vunja ndoa
2:jipe muda maumivu yapungue, msamehe maisha yaendelee
Baaas
 
2009-2011 akafanya mtihani wa form four, 2012 February inshallah akapata matokeo sio mazuri sana wala sio mabaya akaingia certificate ila 28 July akadaka ujauzito, 21 November 2012 ndoa..15/4/2013 akajifungua mtoto wa kike. 2013-2015 Diploma kamaliza Mwaka Jana akapumzika Mwaka huu anaapply degree, mtoto wetu ana miaka mitatu now...nikutaarifu tu huyu binti alijaa vyema nilianza kumsomesha QT January kabla sijapata jibu kuwa ni demu wangu kisha April 2009 ndio akakubali kuwa kwenye uhusiano akiwa anasoma.
 
Hata ukisema unaendelea kukaza ni kujiumiza tu moyo na kujipa stress kama kafanya kafanya tu haibadiliki
Unabaki na option mbili tu
1:huwezi kumsamehe, vunja ndoa
2:jipe muda maumivu yapungue, msamehe maisha yaendelee
Baaas
Option ya kwanza to me is preferred! Evelyn are you married? Can you take the second option. Anyway, kwa wanawake mnakutana nayo sana mume kuwa na hawala nje wachache wanaondokaga na kuvunja ndoa! Kwa mwanamume Mh!!!!!!!!!
 
Jipu hilo, tumbua. Ndoa ya miaka 4 hutajuta ukim-dump, fungua ukurasa mpya kwa sababu hii haitakutoka moyoni maishani and you will never trust her.
Chukulia ulilamba garasha, okota tena karata nyingine lakini usifanye maamuzi ya haraka, mjue kwanza at least a courtship period of 15 months will give you an insight.
Vinginevyo pole, najua ni kiasi gani inauma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…