Mke wangu ananifanyia vituko ili tuachane

Huyo mke walikuolea nini? kama unaweza kutongoza tena acha kuumiza kchwa usimfatlie we fanya yako
 
Kwa hatua aliyokwisha fikia wakati mwingine kumbadili ni vigumu. Chukua uamuzi mgumu japokuwa utaandamana na maumivu makali lakini inaweza ikawa suluhisho la kudumu. Mimi wa kwangu alianza hivyo hivyo japo ni miaka mingi sasa imepita na nilijitahidi sana kutafuta suluhu lakini akashikilia msimamo wake. Na mwisho wa siku tukatalikiana , na baada ya kama muda alifunga ndoa na moja wapo kati ya jamaa zake aliyekuwa amefiwa na mkewe.
hazikupita siku nyingi, akagundua kuwa ni muathirika na baada ya hapo alitumia jitihada nyingi kunitafuta lakini ikawa haiwezekani tena
 
Pole sana...Ila kama.mn watoto kaaa kwa ajili ya wanao...!Hakikisha hukagui simu yake...wewe focus kuongeza kipato na kuwekeza kivyako....!
 
kwa ushauri Wangu kama unajiweza anza maisha mapya piga kazi vumilia ukifanikiwa mwachie nyumba na kila kitu hamia pengine. Hata siku yakimkuta hawezi kukufata Ila ukimwondoa kwenye nyumba ni rahisi kurudi
 
Leo hii ananitaka niondoke, nikaanze maisha kimpango wangu.

Kwanini wewe ndio akutake uondoke? si nyumba umesema mmejenga wote?!!!
 
Kwa bahati mbaya sana dini yangu hairuhusu mke zaidi ya mmoja...

Ukisikia pingu za maisha ndiyo hizo sasa, ulitamka mwenyewe ntakupenda kwa shida na raha, shida ndiyo hizo sasa unabidi ukabiliane nazo kiume.

Kukimbia tatizo siyo suluhisho, tafuta suluhisho la kupigania ndoa yako kwa gharama yoyote.

Inaonekana na wewe pia umechangia kumfikisha mkeo hapo alipofika.

Hebu kumbuka maneno matamu uliyokuwa unamuambia mkeo kipindi chote cha uchumba, umeacha kumwambia sasa amepata mwingine ambaye anajali kuliko unavyojali kwa sababu umemzoea naye ameshampa moyo wake.

Usikague simu ya mkeo, mpuuze fanya kama hamna tatizo lolote baina yenu. anza kumjali hata kama kinafiki tu itasaidia kukuweka tena moyoni mwake. kamwe usivunje ndoa yako hayo ni mapito tu yatapita baada ya kushinda kitakuja kipindi kitamu mno lakini msamaha wa kweli lazima uwe umepita kwanza.
 
yeye ndio anataka usepa na sio wewe....anata muachane....tuliza akili hapo.....pia asiejetaka mgawane mali maana hujamfukuza..ila sasa jiongeze usimlilie saaaana kama anakazana kugoma nakukufanyia maksudi
 
Tafuta michepuko na ikiwezekana mingine ingiza hadi chumbani kwenu mwenyewe atashika adabu.. Uache kuitaita wazee ni kuwasumbua
 
Kama umejitahidi kutaka kuinusuru ndoa yako na yeye bado hakutaki isiwe tabu mpaka akakutilia sumu,mwanamke akishafikia hapo ujue basi yuko anae mzuzua,afadhali ya nusu shari kuliko shari kamili,lakini kumbuka kua ukishasema basi ujue ndio basi sio basi halafu unachungulia DP mara sijui umekosea sms,jipange kiuwanaume na move on,sababu kutakua na vishindo vya hapa na pale mara kamuweka mwanao na Uncle sasa kuepuka yote usiwe unaangalia na kuhusu watoto
kama anataka kukanao sawa mpe kama niwadogo ukitaka kuwasiliana nao mpigie kachukue wanao cheza nao then warejeshe wajibika kwa watoto kama Baba mengine muachie Mwenyezi mungu atajuta kwanini alikua Rude kwako...
 
Mke mwenyewe ndiyo huyo kwenye avatar?
 
Usimuache Bali ishi Naye kama Dada yako,usiguse simu yakee ndio chanzo cha mitarafakano...!ongeza kipato chako..!akitaka kuondoka,muache aondoke zake.
 
Sioni haja ya kutomba kisa sms za honey sijui dear! Wala kuita ndugu, issue komaa mwenyewe ukizingatia ushamjua! Kaa kimya endelea Na maisha yako!
 
Samahani we mwanaume au mume?!
 
Anzisha miradi pembeni ya kukupatia kipato cha ziada ili ujipange zaidi yake. But, hawa viumbe huwa wanamihemko tu. Utashangaa ukifanya hivyo...anarudisha mazima honey kibao, darling, love zinakuwa zako zote.
kwani shida umejua ni kipato?
 
Mwanamke akishaanza kua na kiburi tayari jua kuna mwenzio na ni lazima tu kuna kitu kakuzidi

jaribu chunguza hao watoto wako kweli[emoji23] [emoji23]
 
Shida si kipato kwani maisha yanakwenda.
Tunacho kipata kinatutosheleza kabisa,ila nahisi kama anayahitaji maisha ya juu zaidi ya haya tulio nayo...
 
Mwanamke akishaanza kua na kiburi tayari jua kuna mwenzio na ni lazima tu kuna kitu kakuzidi

jaribu chunguza hao watoto wako kweli[emoji23] [emoji23]
Watoto ni wangu hilo sina tatizo nalo.Damu nzito kaka,ingekuwa si wangu,yangesha julikana kitambo sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…