Mke wangu ananichanganya

Mke wangu ananichanganya

Nasubiri walau thread moja kutoka kwa mwanandoa akieleza sifa nzuri kutoka kwa mwenzie.Hii itafanya mambo kuwa balanced.
 
Pole sana...maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua...hebu kaa chini na mkeo mpange mipango endelevu na katika kupanga hiyo mipango muache mkeo ndo awe msemaji mkuu ili uone anapanga nini then wewe ushauri kutokana na alichopanga yeye, ninyi wanaume huwa mnakosea sana mnapojidai kwmba ndo kichwa cha familia halafu yakiwashinda mnageuka na luona hamsaidiwi....hebu mshirikishe mkeo kama nae ni kichwa cha familia uone itakavyokuwa....
 
Mimi ninafanya kazi na mume wangu kwa kweli ndo mlezi wa hii familia kwa sababu tuna kipato tofauti....lakini hajawahi kunidharau eti kwa sababu nina kipato kidogo kuliko yeye...huwa ananishukuru na kuonyesha furaha pale ninapotumia pesa yangu kununua kitu...sasa na wewe hakikisha unamuonyesha mkeo kwamba hata shilingi 100 itokayo kwake mkeo kwako wewe ni kubwa na inathamani .....jamani MAISHA YA NDOA NI GWARIDE HIVYO JITAHIDI USIPOTEZE STEP MAANA UKIANGUKA WENZIO WANAKANYAGA WANAPITA HAKUNA WA KUKUOKOTA.
 
Hapo ndo huwa nachoka na hawa viumbe.Halafu utakuta wanalalamika mfumo dume.Mchape mimba akae kwanza nyumbani iwe ndiyo mwisho wa kazi na heshima itarudi.Samahani kama nitakuwa nimekukwaza, ngoja nilale asubuhi tutaendelea

sasa akimchapa mimba si ndio majukumu yanaongezeka?
 
Tuna miaka tisa sasa yenye maisha ya kawaida yenye furaha, mimi nikiwa nafanya kazi katika kampuni moja hapa tabora yeye akiwa mama wa nyumbani.
Miezi nane iliyopita alipata kazi, wana jamii naomba msaada toka apate kazi amekuwa na kiburi, anataka hela yangu ndo itumike tu yakwake wala hataki isaidie.nimemuelimisha kuhusu ugumu wa maisha lakini wapi, tatizo lolote likitokea ni mm ndo wa kusolve.. P/se help

Wewe ndio utakuwa na matatizo, muda wote alipokuwa hana kazi mbona haukichanganyikiwa, kaanza kufanya kazi ndio unatolea mshiko wake macho? acha kukwepa majukumu yako.
 
Afadhali ijulikane moja kama tangia mwanzo.Huyo mke wake ameburuzwa na wanawake wenzake wasiopenda maendeleo ya wengine na yeye bila kufikiri ameingia kichwakichwa.

Mh!ngumu kumeza na hiyo mimba c mpaka mwanamke akubali kuibeba?hapo akae na mke wake wawekane sawa tu!
 
mpe nafasi aizoee hela. Live as if she doesnt exist, haitakuwazisha. Hawa ndio viumbe tuliopewa na Mungu. Usipokua mvumilivu, ujue Presha na Kisukari viko karibu.

You are right mdoe
 
Last edited by a moderator:
tupe feedback mkuu,mkeo kashashusha ghorofa kwao?lol:smiling::A S 100:
 
Back
Top Bottom