Mke wangu anajamba sana usiku, nifanyeje?

Status
Not open for further replies.

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,407
1,110
Jamani mnisaidie.

Siku za karibuni mke wangu anajamba sana nyakati za usiku, tena kwa sauti kubwa.

Kujamba kwake kunanishtua sana usingizini, na nashindwa kuendelea kulala.

Jambo hili linanitesa sana maana hata nikiwa kazini ninachoka sana maaana silali masaa ya kutosha.

Nimemuuliza ni nini, ila hata yeye hajui chanzo. Siwezi kumkimbia.

Je, hili ni jambo la kawaida? Hivi kuna dawa ya kuzuia hilo?

Nisaidieni mwenzenu!

=====
SIMILAR CASES:
Ndugu wana MMU,

Nimeishi na mke wangu kwa muda wa miaka 2 na tuna mtoto mmoja. Kwa ufupi tunaelewana sana, tatizo kubwa ni tabia yake ya kujiachia(ushuzi) mbele yangu.

Nimejaribu kumweleza kama sifurahishwi na anavyofanya aingie chooni lakini yeye anacheka na kunieleza anapumua.

Sasa nimeongea mpaka nimechoka, nimeamua kuacha tu.

Naomba ushauri wenu, je kujamba mbele ya mpenzi/mume/mke ni kupumua tu?

Na je akijamba mgeni akiingia ndani(imewahi tokea) na kukutana na harufu atatuanaje?

Please help

Mwingine:
Mimi na mke wangu tunapenda sana utani. Lakini huu utani wa kufikia mahala haoni aibu mpaka anakua ananijambia tukiwa kitandani..mi sipendi kweli. Mpaka nasafoketi.

Afu anajamba mpaka pua inachachuka kabisa. Nikimwambia anaona kama utani...

Nipeni ushauri wadau.... Nampenda sana mke wangu.
 
Ni kweli au unatania jamvini. I am trying to imagine mtu kujamba ukasituka usingizini.

Mbona watu wanajamba sana wakiwa faragha? Huna haja ya kubana hewa chafu isitoke. Sasa wewe ya kuamka usingizini kali.

Mpeleke kwa daktari. Au anashiba sana usiku.
 
Nachelea kuamini kama hapa kiukweli unamzungumzia mkeo wa ndoa, ubavu wako, sehemu ya mwili wako, mama wa watoto wako na sabuni yako ya roho.

Kama kweli unamzungumzia mkeo then naamini kweli kuna laana nyingine ni za kujitafutia.
 
Nachelea kuamini kama hapa kiukweli unamzungumzia mkeo wa ndoa, ubavu wako, sehemu ya mwili wako, mama wa watoto wako na sabuni yako ya roho.

Kama kweli unamzungumzia mkeo then naamini kweli kuna laana nyingine ni za kujitafutia.
kwani kuna shida gani jamani.? mshauri bwana
 
kwa nn hujambi sana?
sili sana especialy usiku mi jioni huwa nakunywa juice,maziwa na matunda matunda
pia napiga pushap tano kitandani mwili unakuwa relaxed !
sasa kama huyo mama usiku anakula ugali maharage na samaki mzima sato jumlisha mchicha na maparachichi matatu kwa nini asifanye milipuko ya mabomu ndani?
 
Cheki na jamaa wa barrick au airport wanavile vifaa kama headphones za kuzuia sauti itakusaidia sana mkuu.
 
sili sana especialy usiku mi jioni huwa nakunywa juice,maziwa na matunda matunda
pia napiga pushap tano kitandani mwili unakuwa relaxed !
sasa kama huyo mama usiku anakula ugali maharage na samaki mzima sato jumlisha mchicha na maparachichi matatu kwa nini asifanye milipuko ya mabomu ndani?

mbona maziwa yanajambisha sana au wewe uko lactose tolerant?
 
Jamani mnisaidie,siku za karibuni mke wangu anajamba sana nyakati za usiku,tena kwa sauti kubwa,kujamba kwake kunanishtua sana usingizini,na nashindwa kuendelea kulala,jambo hili linanitesa sana maana hata nikiwa kazini ninachoka sana maaana silali masaa ya kutoshanimemuuliza ni nini ila hata yeye hajui chanzo,siwezi kumkimbia,je hili ni jambo la kawaida?....hivi kuna dawa ya kuzuia hilo?....nisaidieni mwenzenuu

Kwani wewe hujui kwamba kujamba ni afya???? anyway mwambie asile chakula kinachomletea gas/acid nyingi tumboni....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom