Mke wangu anaenda Ughaibuni for good

Mke wangu anaenda Ughaibuni for good

Maisha ni kutafuta popote pale muache aende ila usisahau kumpa nasaha naamini atakuelewa tu ila pia kitu kimoja ukizingatie mkeo akiondoka usiingize mwanamke mwingine ndani ya nyumba yenu hata kama kwa siri akija kujua amekuacha mazima.
 
Mkuu kwa maisha ya sasa, watu wanaangalia maslahi, wapi kuliko na malisho ya kijani kibichi kingi..!

Kujivunia kazi kulikuwa enzi za socialism wakati nchi ilipokuwa haijaingia katika mfumo wa kibepari..

Wapo watu wengi tu wanaojivunia kuzifanya hizo kazi.
 
Mkuu kwa maisha ya sasa, watu wanaangalia maslahi, wapi kuliko na malisho ya kijani kibichi kingi..!

Kujivunia kazi kulikuwa enzi za socialism wakati nchi ilipokuwa haijaingia katika mfumo wa kibepari..

Kwani nimebiiishaaa? Hata mi nshapiga sana tu box, isipokuwa mtu asije akadanganyika kuwa akienda abroad basi kila kitu ni kubonyeza, inauma kuziita shame jobs but ndio ivyo

Sent from nokia Jeneza
 
Anaenda kutembea au kutafuta maisha??si mbaya kama mpo ktk upendo. Mengi uwa yanatokea ktk situation hiyo nawajua watu waliosalitiwa na wanawake zao ktk hali hiyo yule dada alienda US kwa dada yake 2005 mpaka leo hakuna ata simu tu kujua anaendeleaje na hakuna anayejua kama ni mzima au vipi!!!watu wanabadirika sana.
Wanawake/wanaume wengine wana bahati sana wanakwenda nje na maisha yananyooka na wanaleta na familia zao.Tatizo baada ya kutawaliwa na wazungu mda mrefu waafrika wengi bado wanadhani ukifika nje lazima ufanye kazi za CHINI hapana hayo yalikuwa zamani.Binafsi kitengo nilichopo kuna wajerumani sita ambao wanaripoti kwangu,mambo ya Shame jobs kama walivyokwambia hapo juu yapo lakini si kwa wote inategemea na bahati ya mtu.
 
Hebu fafanua, huyo ni mkeo au mzazi mwenzio? Maelezo yako yanaonyesha unampenda mzazi mwenzio, lakini yeye yuko tu. Ndio maana mwaliko wa 'supposedly' mlezi wake umekuwa wa muhimu kuliko wewe. Afu una hakika ni mlezi wake tu? Hakuwa anajilipa kweli huyo mlezi? ANyway, nsikujaze taka kichwani.
(yaani mie mtu saa hivi aniite ulaya, kama zombie haendi, hiyo safari haipo, uwiii mapenzi niue mahaba nizike, kama ulaya nitafika hata kwa ndotoni)

Kama na yeye anakupenda, fanyeni maamuzi ya kufungandoa fasta ili akifika ughaibuni, kama mna nia ya kuishi pamoja iwe rahisi wewe kwenda kupitia mgongo wake.

Naona dalili za manyoa manyoa
 
Uko right kabisa, big up kwa kuona hili mkuu Kiwa

mkuu watu especially vijana wanakosea sana maana ya neno MKE. MKE au MUME ina maana kubwa sana. ukiona kwamba mkeo anaweza kufanya hivyo basi ujue huyo ni mkeo kidini, kimila au kisheria but HUNA mamlaka ya MUME kwake kwa kusimama kama MUME.
 
Umeshasema maisha sio mazuri, muache aende bwana we akasake hela.

Acha kulia lia. If she is meant to still be yours then nothing will come between you.
 
Dah aisee kama anakupenda vzr kbs usijali, ila si salama sana unless atakua anafanya kazi (not shame jobs). Ila kama ni kutafuta senti fanya fasta umfate, kuna mijama ya west Afrika inapenda sana dada zetu yaani na huu upweke na life style la majuu bila company ngumu sana.

Life is soo stressful bila kuwa na company ndio mana mambo ya bf n gf wamewaacha watoto wanaendelea tu as long as wako above 16

upo sawa mkuu, hawa ndugu wa west wanapenda sana dada zetu...
 
mmh mahusiano mengi hata ya ndoa huyumba sababu ya hizo safari za nje, tena hiyo ambayo hata haijulikani malengo, kama umeshamruhusa acha tu aende ila muwekeni Mungu mbele sana
 
Hi wadau,
Mi ni mgeni Hapa JF ila napenda kushare Jambo linaloninyima usingizi.Mke wangu anataraji kusafiri kwenda ughaibuni ifikapo mwezi wa nane,nimezaa nae mtoto mmoja na naishi nae katika mji mkoa mmoja Hapa Tz.Safari yake hii imegubikwa na utata kutokana na kwamba mlezi wake amemwita na hajui atachukua mda gani huko ughaibuni,Maisha yetu Hapa bongo si mazuri sana,na yeye anashawishika kumwacha mtoto kwa mzazi wake na kwenda ughaibuni.Sasa inaniwia ugumu kumuachia aende. Hebu put yourself in my shoes ingekuwa wewe ungelifanya nini,ukizingatia invitation imeshafika na process za visa na tiketi zinaendelea, naomba ushauri on a serious note kwa wadau

Depressed hubby

Sent from my iPhone using JamiiForums
Du hatari sana ndugu yangu,ila sijakuelewa vizuri.Ameitwa na mlezi wake ambae ni baba yake ama ameitwa na mlezi aliemlea tu? By the way dhumuni na lengo la safari hiyo ni nini hasa?Kama huelewi kinachoendelea mwambie na wewe unataka kwenda nae maana alichokiunganisha Mungu mwanadamu tena mlezi asikitenganishe,ala nani hapendi upepo wa ulaya
 
Umenipa faraja mkuu ni baba yake alimtelekeza awali sasa ameibuka anadai anataka kumsaidia mwanae aliyemwacha miaka 15 iliyopita

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
mmh mahusiano mengi hata ya ndoa huyumba sababu ya hizo safari za nje, tena hiyo ambayo hata haijulikani malengo, kama umeshamruhusa acha tu aende ila muwekeni Mungu mbele sana

Bado tunashauriana nimeweka Hapa kupata mawazo zaidi

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Umeshasema maisha sio mazuri, muache aende bwana we akasake hela.

Acha kulia lia. If she is meant to still be yours then nothing will come between you.

Every cloud has a silver lining,hii ni alert kwangu na nsipoangalia naweza kuwa nimeolea wamarekani weusi

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Every cloud has a silver lining,hii ni alert kwangu na nsipoangalia naweza kuwa nimeolea wamarekani weusi

Sent from my iPhone using JamiiForums

You worry too much! Give some room for benefit of doubt bwana weeee.
 
Mkuu kwa maisha ya sasa, watu wanaangalia maslahi, wapi kuliko na malisho ya kijani kibichi kingi..!

Kujivunia kazi kulikuwa enzi za socialism wakati nchi ilipokuwa haijaingia katika mfumo wa kibepari..

Welp, kila siku mimi nakutana na watu wanaojivunia kazi zao.
 
Umenipa faraja mkuu ni baba yake alimtelekeza awali sasa ameibuka anadai anataka kumsaidia mwanae aliyemwacha miaka 15 iliyopita

Sent from my iPhone using JamiiForums

Kaka pole sana lakini kama kweli baba yake anataka ustawi wa ndoa yenu shurti angetaka na wewe uambatane nae lakini yeye kwa kutaka mwanae ndiye aende nina walakini ila ni ngumu sana.Vipi wakati anaandaliwa safari hiyo baba mkwe alikushirikisha ama aliwasiliana na mtoto wake tu basi
 
Hakunishirikisha he simply told my wife akae na kujadiliana na Mimi kuhusu safari ila hajanipigia personally.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unaogopa kumegewaa na wadhungu hahahhhahhhahha
#nyani ngabu yupo tayari kumpokea mbeba box mpya!!!
 
Amua.,..wew ni mume kama hukubaliani nalo ongea naye atakuelewa tu.
 
Shame jobs kivipi? Kama mtu shughuli zako zinakuingizia rizq halali na unajitegemea na hicho chochote ukipatacho (hata kiwe kidogo namna gani) na huombi mboga wala chumvi kwa mtu, shame itoke wapi?

Kwa argument hii hata wale dada zetu wanaosimama mabarabarani usiku pia wanajiingizia kipato halali so si shame job
?
 
Back
Top Bottom