Mke wangu ana VVU

Mke wangu ana VVU

nengunia

Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
12
Reaction score
12
Nimeoa januari 2013 ndoa ya kanisani na tulipima ila nadhani mke wangu alifahamiana na madokta,mwezi uliopita nimegundua anatumia ARV toka april 2013.

Nimepima mara nyingi sina virusi hata leo nimepima. Yeye ananipenda ila nimeingia hofu naogopa mno hata kumgusa.

Nifanyeje wakuu?
 
Kwaiyo kuanzia mwaka 2013 nyie mnatumia protection tuu?
Kama ni hivyo ata mtoto mmoja hamjapata.sio?
 
Pole ndugu usiwe na wasi wapo wanandoa wengi wanaishi na kuzaa watoto na huku mme au mke ana vvu.Kama hajakuamvukiza muda wote huo basi ujue si rahisi kukuambukiza tena usihofu
 
Pole sana kaka. Ila jaribu kupata ushauri kwenye vituo vya afya. Nadhani kama kweli unampenda unaweza kuendelea kuwa naye kwa kufuata taratibu fulani ili usiweze kupata na akaweza hata kupata na mtoto asiye na VVU.
 
'parapanda italia parapanda...parapanda italia parapanda...hiyo parapanda.....'
Ndugu angalia usije imbiwa huo wimbo aisee! Huyo hakupendi kama angekupenda angekulinda. Angekwambia ukweli kabla hamjaoana.

Ila Mungu ni mwema...amekulinda kwa muda wote huo. Sasa vile umejua basi huenda ulinzi wa Mungu kwako ukakoma maana sasa Mungu atakuacha uamue mwenyewe...kujiponya au kufa!

Unaweza kujilala kitandani ukazinduka kumbe umemlalia nyoka. Ni Mungu amekuponya! Sasa ukiamua kuendelea kulala na nyoka wakati tayari umemuona eti Mungu ataendelea kukulinda...pole,...utakuwa unamjaribu Mungu!
 
Pole sana Ndugu,nakumbuka story ya mtu mmoja ivo ivo Njia panda Clous radio Ilikuwa january siku ya j2..sikimbuki tarehe2015..kuna mtu alishudia kuwa mke wake aligundulika kuwa na VVU na mume hana.

Lakini mke wake alijua sana ni +ve akijua ili hali hakumjulisha mumewe..na siku ya kupima alijua kabisa majibu yake yatakuwaje bt hakuwa amemuambia mumewe akihofia mumewe angemuacha... ilikuwa story ndefu sana ya kusisimua.

Nakumbuka watu wengi pia walituma sms kushuhudia ndugu zao na rafik zao wa karibu ambao wana hali kama uliosema...Hizo ni hali za na zipo na siyo wa kwanza wewe...Cha msingi hapo ni imani ya kimungu zaid inatakiwa na siyo za kibinadamu...mungu akufanyie wepesi kwa kweli...!
 
Una bahati sana kaka, miaka yote hii hujaukwaa? Kama member mmoja kauliza hapo juu, hamjazaa? Je kama mmezaa mtoto mzima?
 
mimi napenda sana kuangalia taarifa ya habari usiku sasa muda huo huutumia kwenda kumeza dawa toka 2013..na kanipa maelezo ya kutosheleza bila kudanganya kuwa toka namuoa ana vvu na madokta aliwapanga waseme hana

Kwahyo umeamuaje?

Kwa ushauri wangu binafsi mrudishe kwao kwasababu amekudanganya ambalo ni kosa la kukugharimu maisha.
 
Back
Top Bottom