Mdau anaomba ushauri: "Nimetembea na Mfanyakazi wangu ana sifa zote za kuwa mke ila ameshazalishwa, nifanyeje"

Aug 31, 2022
54
99
Huu ni ujumbe wa Mdau kutoka Instagram huko.

"Nina miaka 25 nataman sana kuoa lakin naumiza kichwa sana kuangalia mwanamke wakunifaa kulingana na wanawake wa siku hizi.

Sasa kuna Dada nafanya nae kazi mimi ni kama boss wake nimemuajiri ananiuzia Mitumba, yeye anamiaka 26 ana mtoto mmoja, nishalalaga nae sasa ni ananipenda kupita kiasi sjui kama anaigiza lakini ananipenda sana na anatama nimtamkie kumuoa.

Mimi sihitaji kumuoa maana tayari kashazalishwa lakin kiukweli anafaa sana kuwa mke wa MTU na anatamani apate mwanaume alie serious amuoe, sometime roho inanisukuma kumuoa lakin daaah nahisi kuna kitu tu kinanizuia lakin yeye ni mwaminifu sana hacheat, hadangi, hajui kuomba omba hela na kiufupi tu namdrive navotaka.

sasa nifanyeje na ukingatia kashazalishwa na mimi napenda ambae ni hajazaa tuanze nae upya, hata Nyumban nikiwambia mke wangu anamtoto wa pemben hawawez kufurahi
 
Kama Kuna kusita kumuoa ndani yako basi tii kile unachosikia ndani yako na sio kile macho yanachoona.

Mfanye kuwa rafiki wa kawaida tu.

Kwanini uanze kufikiria kuoa?!

Sio kila urafiki lazima muoane au kuzaa hayo Ndiyo makosa wengi hufanya na kisha kujutia.

Kwani amekwambia anataka umuoe?

Tena afadhali hiyo muwazi wengine angekudanganya hajazaa kisha uingie mkenge kirahisi.

Hata hivyo wapi walozaa ambao wanafaa kuwa wake wazuri na wapo wengi hawajazaa lakini hawafai kuoa.
 
Kwisha Habari Yako!!
Ndugu Zangu Oeni Elimu Ni Bure Mpaka Kidato Cha Sita
Oa Haraka Huyo Huyo Unayempenda Vinginevyo Unapoteza Bahati Na Uelekeo
Mambo Ni Mengi Sana Kumbuka 2024 Uchaguzi Local Government
2025 Uchaguzi Mkuu
Hutapata Nafasi Tena Tena
 
Hisia zinaweZa kufanya usifikiri vizuri kabla hujafanya maamuzi.. hata hivyo mara nyingi wanawake waliokwisha zalishwa hutamani sana kuolewa,atafanya chochote ili uone anafaa kuwa mke umuoe. Inawezekana kweli akawa na tabia nzuri lakini sifa ya single mother inaleta ukakasi! Ukiachana na mambo ya kuchapiwa na mme wake wa zamani, kuna timbwili la ubaguzi huko mbele kwenye malezi ya watoto

Alafu kingine "umri"! sio kila mwanamke mwenye sifa (wife material) lazima awe mkeo/umuoe mzee wapo wanaoendana nae sio wewe! Mzidi angalau basi miaka miwili/mitatu, ukiendekeza kale ka msemo ati "umri ni namba" shauri yako.

Kukupenda isiwe sababu ya wewe kuhama njia (usilewe upendo). Kila atakaekupenda utamuoa?
 
Back
Top Bottom