Mke wangu amepanda cheo, ananidharau

Mke wangu amepanda cheo, ananidharau

Huu ushauri wa kijinga sana.
Wa kijinga kama mama yako et?
Tulia mama yako afukuzwe si analeta dharau kwa baba yako hadi mzee wa watu anaomba ushauri. Afukuzwe mamako nawe ufuate ***** wewe.
 
Hongera amepanda cheo, kamwe udikubali kudharaulika mnyooshe tu ila usioe mke Wa pili .

Don't make permanent decision for temporary emotions
 
Jiamini, acha hofu!
Mabadiliko ya tabia baada ya kupanda cheo ni jambo la kawaida!
mtu akiwa mkurugenzi, definitely atakuwa na muda mwingi kazini kuliko nyumbani!
huwezi kumlinganisha mke mwalimu na CEO!
Mwl hata akija na kazi ya kusahihisha nyumbani bado ana siku kadhaa za kuwa huru, CEO anafanya kazi 24/7 lkn pia kumaintain higher position kunahitaji dedication na commitment ya hali ya juu!
hata wewe ungepanda madaliko yangetokea na wala sio ya nia mbaya!
Mikopo bank, yes inapaswa akueleze, lakini kwa kujua tu kuwa amekopa nadhani amekwambia ila wewe ulitaka mpange akope kiasi gani, lini na kwa shughuli gani, which is good, lakini sio lazima!
ushari wangu kwako:
instead of kukaa chini na kumlalamikia mkeo, hebu msaidie afanye vema kazini kwake.
inferiority complex ya wanaume, imeua potential nyingi za wanawake wa kiTanzania na sababu kuu ni ujinga tu!
hofu ya mke kugongwa na wakubwa wenzake (hata wanawake wauza vitumbua uswahili kwetu wanagongwa na wengine sana kuliko hata CEOs), mikopo na upatu hawa wanawake wa uswahilini huku wanaingia na kujiunga vicoba/upate bila hata ya kutuambia waume zao yet hatulalamiki kwa kuwa tunajua ukuaji wao wa uchumi haututishi kwa kuwa bado watakuwa tegemezi kwetu!
  1. Tazama ni package gani unaweza ku-offer ktk ndoa yenu, mwanzo ulitegemea uchumi (mume kichwa kwa kuwa ndio provider) sasa mama amekuwa sawa na kichwa, then angalia angle nyingine ya uchangiaji itayokupa hamasa sawa na ile role uliyokuwa nayo mwanzo!
    • kuwa mzuri kitandani
    • kuwa mwenye busara na wa msaada kwake, mpitie kumchukua kazini na mpeleke kazini (kama una gari) ili kumuongezea muda wa kumalizia viporo vya kazi akiwa anaenda na kutoka job! elezea hiyo dhamira yako na siku Fulani usimpeleke home straight mpeleke kwa dinner hotelini kama sehemu ya kumuondolea stress za kazi, hutoibiwa!
    • chukua role ya kusimamia watoto, home work, kufuatilia ada, maendeleo shuleni-then utampunguia stress za umama na hivyo kuacha huru mikono na akili zake kwa ajili ya performance za kazini
  2. kuwa sehemu ya mafanikio yake, na chekelea kila ustawi wake. acha kujenga wivu kwa position yake ili isiwe sehemu ya mgogoro wenu! kwa wanawake/mtu yeyote anayejali carrier, ukiwa kikwazo hawezi kukusikiliza, anaweza kukudrop lakini sio kazi yake. usipigane vita ambayo huwezi kushinda, join her, kuliko kuwa na wivu wa kijinga, msaidie kufanikisha anayoyafanya, kumbuka kuna vijana/co-workers watakaojitia ukaribu au hata kutaka kumgonga mkeo sio kwa mapenzi bali kutaka favours. fight your battle alone na kimya kimya! ukiwa wa msaada atakurudia wewe Zaidi kuliko kuweka ukaribu na Mbweha wanaomvizia kwa favours.
  3. panga na mkeo, then she will trust you, wanawake ni tegemezi by nature, huwa wanatuamini kupita kiasi! cha msingi ni wewe kujionesha kuwa una-confidence! unajua hata mwanamke msomi anaweza kuolewa na std 7 na bado akaamini kuwa decisions kubwa baba anatakiwa kuonesha zifanyikaje! anaweza kukufuata kwa ushauri wa gari gani ya kununua hata kama akijua kuwa kwenu hata baiskeli hamna na yeye ameishi ktk nyumba yenye gari Zaidi ya 10! ukijipanga bado mke CEO utamuongoza!
    • ukibebwa na wivu na hofu, hata kama wewe ndiye ungekuwa na nafasi nzuri bado mke atatamani awe karibu na houseboy kwa ajili ya ushauri! na dnio anazidi kuwa na mazingira hatarishi ya kupenywa!
Shkamoo mkuu...ushauri bomba
 
Mke wangu amepanda cheo kazini. Tangu amepata cheo anaonyesha dharau; amebadilika tabia.

Zaidi amekopa benki bila kunitaarifu. Nifanyeje?
Ni kawaida yao mkuu! Pole,vumilia labda atabadilika.Ila akishaanza dharau ujue pia ameshaanza mahusiano nje.Mimi nilivumilia mwishowe ikabidi nibwage manyanga.Baadae alininitafuta nikawa nimeshaji commit mahali pengine nikamwambia it is too late.Anajuta sana.
 
Mwanaume aweza kuwa na elimu nzr kazi nzr muonekano wa maana ila akawa na mwanamke wa kawaida kabisa na mapenzi yakaenda ss geuza kinyume chake uone itakuwaje hv kwann mwanamke akikuzidi hata kakitu kadogo tu inakuwa tafran ndani ya nyumba? inaudhi sana wema mfanyiwe nyie tu vikiliwa vya somo na vya mwali viliwe!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom