Mke wangu amepanda cheo, ananidharau

Mke wangu amepanda cheo, ananidharau

Kwanza jiulize hiko cheo kapandaje! Ukishajua jinsi alivyokipata inaweza ikakupa mwanga.
 
Kwanza mimi naona huu uzi ni wa kipuuzi tu. Sasa kama mke wako amepanda cheo anaanza kukudharau maanake nini? Sisi tunajua mnavyoishi huko kwenu hadi utuombe ushauri. Pili unawajua watu unaowaomba ushauri hasa kwa issue nyeti kama hiyo? Mi nadhani tunapotezeana muda tu humu jf kwa thread za ajabu ajabu kama hii. Wachawi wa ndoa yenu ni nyie wenyewe msitegemee wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wawaletee amani na upendo katika ndoa yenu kama ninyi wawili hamtaweza kutambua makosa yenu na kujisahihisha!
Safi saaanaa
 
Ndiyo tabia za wanawake walio wengi, akipata cheo kikubwa kuliko wewe ni shida, akisoma zaidi yako nalo tatizo mbaya zaidi mkeo unamuanzishia mradi Na kumpa madaraka yote ya mradi sasa akizoea kuishika hiyo hela dharau haichelewi. Nakushauri uishi nae kwa akili maana hata vitabu vitakatifu vimetuasa hivyo.
 
mkuu inategemea na wewe ulivyo kama kweli amepanda cheo na amekuzidi mshahara kiasi cha juu, lazima akudharau anakuona dume suruali tuu huna lolote

√√lakini kama kweli amepanda cheo na hajakuzidi chochote katika pesa, kazi,vitega uchumi na anakudharau my friend tafuta haraka chanzo cha kupanda cheoo, ukitaka kujua kasikilize ile nyimbo ya "Mkasa wa bosi"
 
Mke wangu amepanda cheo kazini. Tangu amepata cheo anaonyesha dharau; amebadilika tabia.

Zaidi amekopa benki bila kunitaarifu. Nifanyeje?
Temana nae
Usiendekeze ujinga kama hajielewi.

Ishi kwa makini sana na hawa watu.
Mwanamke hupewa kiburi na Mwanaume tu
Tafakari chukua HATUA
 
Vitu vingi vinapimwa kwa ratio ni kama wanavyosema ratio kwa kila Watanganyika 4 mmoja ni kichaa je waliwapima watanganyika wote ndo wakagundua hvyo? siku zote wanasema (winner- takes - all )
Hiyo ratio yako wewe uliipimia wapi kama siyo hisia zako tu? Acha uvivu wa kufikiria mambo. Usijastify udhaifu wako kwa assumptions!
 
Mke wangu amepanda cheo kazini. Tangu amepata cheo anaonyesha dharau; amebadilika tabia.

Zaidi amekopa benki bila kunitaarifu. Nifanyeje?
Jiamini, acha hofu!
Mabadiliko ya tabia baada ya kupanda cheo ni jambo la kawaida!
mtu akiwa mkurugenzi, definitely atakuwa na muda mwingi kazini kuliko nyumbani!
huwezi kumlinganisha mke mwalimu na CEO!
Mwl hata akija na kazi ya kusahihisha nyumbani bado ana siku kadhaa za kuwa huru, CEO anafanya kazi 24/7 lkn pia kumaintain higher position kunahitaji dedication na commitment ya hali ya juu!
hata wewe ungepanda madaliko yangetokea na wala sio ya nia mbaya!
Mikopo bank, yes inapaswa akueleze, lakini kwa kujua tu kuwa amekopa nadhani amekwambia ila wewe ulitaka mpange akope kiasi gani, lini na kwa shughuli gani, which is good, lakini sio lazima!
ushari wangu kwako:
instead of kukaa chini na kumlalamikia mkeo, hebu msaidie afanye vema kazini kwake.
inferiority complex ya wanaume, imeua potential nyingi za wanawake wa kiTanzania na sababu kuu ni ujinga tu!
hofu ya mke kugongwa na wakubwa wenzake (hata wanawake wauza vitumbua uswahili kwetu wanagongwa na wengine sana kuliko hata CEOs), mikopo na upatu hawa wanawake wa uswahilini huku wanaingia na kujiunga vicoba/upate bila hata ya kutuambia waume zao yet hatulalamiki kwa kuwa tunajua ukuaji wao wa uchumi haututishi kwa kuwa bado watakuwa tegemezi kwetu!
  1. Tazama ni package gani unaweza ku-offer ktk ndoa yenu, mwanzo ulitegemea uchumi (mume kichwa kwa kuwa ndio provider) sasa mama amekuwa sawa na kichwa, then angalia angle nyingine ya uchangiaji itayokupa hamasa sawa na ile role uliyokuwa nayo mwanzo!
    • kuwa mzuri kitandani
    • kuwa mwenye busara na wa msaada kwake, mpitie kumchukua kazini na mpeleke kazini (kama una gari) ili kumuongezea muda wa kumalizia viporo vya kazi akiwa anaenda na kutoka job! elezea hiyo dhamira yako na siku Fulani usimpeleke home straight mpeleke kwa dinner hotelini kama sehemu ya kumuondolea stress za kazi, hutoibiwa!
    • chukua role ya kusimamia watoto, home work, kufuatilia ada, maendeleo shuleni-then utampunguia stress za umama na hivyo kuacha huru mikono na akili zake kwa ajili ya performance za kazini
  2. kuwa sehemu ya mafanikio yake, na chekelea kila ustawi wake. acha kujenga wivu kwa position yake ili isiwe sehemu ya mgogoro wenu! kwa wanawake/mtu yeyote anayejali carrier, ukiwa kikwazo hawezi kukusikiliza, anaweza kukudrop lakini sio kazi yake. usipigane vita ambayo huwezi kushinda, join her, kuliko kuwa na wivu wa kijinga, msaidie kufanikisha anayoyafanya, kumbuka kuna vijana/co-workers watakaojitia ukaribu au hata kutaka kumgonga mkeo sio kwa mapenzi bali kutaka favours. fight your battle alone na kimya kimya! ukiwa wa msaada atakurudia wewe Zaidi kuliko kuweka ukaribu na Mbweha wanaomvizia kwa favours.
  3. panga na mkeo, then she will trust you, wanawake ni tegemezi by nature, huwa wanatuamini kupita kiasi! cha msingi ni wewe kujionesha kuwa una-confidence! unajua hata mwanamke msomi anaweza kuolewa na std 7 na bado akaamini kuwa decisions kubwa baba anatakiwa kuonesha zifanyikaje! anaweza kukufuata kwa ushauri wa gari gani ya kununua hata kama akijua kuwa kwenu hata baiskeli hamna na yeye ameishi ktk nyumba yenye gari Zaidi ya 10! ukijipanga bado mke CEO utamuongoza!
    • ukibebwa na wivu na hofu, hata kama wewe ndiye ungekuwa na nafasi nzuri bado mke atatamani awe karibu na houseboy kwa ajili ya ushauri! na dnio anazidi kuwa na mazingira hatarishi ya kupenywa!
 
ukiona hvyo kuna kitu anakifanya ndo kilimpandisha cheo
 
pole mkuu,ungejua jitihada alizotumia kupata hicho cheo usingeumiza kichwa! manyoya hayo,watu washakula....
 
Nawe muombe Bosi wako akupandishe cheo zaid yake, mlilie shida kuwa mkeo anakunyanyssa, mwambie akupandishe hata cheo jina tu sio lazima mshara kupanda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom