ataenda kuchukua tena mkopo ili tufanye renovationaiss na apartment zikiungua moto?!
Majukumu gani hayo umeoa???
kwa bahati mbaya umeshazeeka bila kuwahi kukutana na mwanaume ambaye umempenda sana na ndiomaana unaona kama haiwezekani. Umri wako ushapita, waachie vijana.kwanza umeandika kishari shari, kiugomvi ugomvi, dizaini kama unamkoa hivi.... hizi ndoa jamani, ehhh mungu zisimamie. kama mimi ndio mkeo, huo utumbo siwezi kuukubali hata iweje, akikubali mkeo, atakua kiazi kama wewe.... akope pesa, yeye, mlipaji yeye, ili wewe ufaidike maana unataka kumzidi kipato kwa mgongo wa huyo huyo mkeo... kweli stupid...


Nimeishia kutabasamu kwa namna unavyopiga mahesabu ya kumpiga bao mkeo.Wadau,
Mke wangu amenizidi mshahara, kwa mfano: kama mimi napokea mshahara sh laki moja basi yeye anapokea laki mbili-ukijumlisha na house allowance, transport na pesa nyingine zisizo na kichwa wala miguu.
Hii kiukweli siipendi kabisa toka muda mrefu kama mwanaume, sasa nimekuja na mkakati ufuatao wa kumzidi kipato mke wangu nitahitaji mawazo yenu.
Nataka nimshauri mke wangu aende akachukue mkopo bank (mkubwa tu kwa mshahara wake) na baada ya kumchukua mkopo ukichanganya na akiba tuliyonayo nataka tufungue kampuni( tayari nimeshaanza michakato michakato)
Ambayo mimi nitakuwa msimamizi mkuu wa uendeshaji wa kampuni. Mapato yote yatakayokuwa yakiingia mimi ndio nitakuwa controller kwakuwa yeye kazi yake inambana sana na hawezi kupata nafasi ya kufatilia kwa undani sana biashara inavyoenda.
Kwa mkakati huo hapo juu basi mke wangu atakuwa anakatwa pesa bank kutoka kwenye mshahara wake (kwa miaka mitano mfululizo) huku mimi mshahara wangu ukiwa vile vile-hapo nitakuwa nimeshampiga pigo la kwanza
Kwa kipindi hicho chote mi ndio nitakuwa controller wa ofisi na mpaka inaisha hiyo miaka mitano ya kukatwa pesa ya mkopo na bank basi kampuni yetu itakuwa imekwisha simama na ina generate faida nzuri hivyo hata akishamaliza mkopo na kuanza kulipwa mshahara wake mi nitakuwa naingiza pesa nyingi kwenye kampuni-Pigo la pili
Kampuni isipofanikiwa nitafanya nini?
Nitanunua kiwanja, baada ya hapo nitamwambia akachukue mkopo tena bank mkubwa mara dufu ya ule ambao atalipa hata kwa miaka 10, kisha tunajenga apartments za kupangisha mi ndio nitakuwa mpokeaji wa kodi.
Mwanamume ni mwanaume tu wadau na usikubali mwanaume tu.Wadau usikubali mkeo aukuzidi pesa atakuwa na kiburi
Karibuni