Mke wangu amenizidi mshahara

Mke wangu amenizidi mshahara

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Wadau,

Mke wangu amenizidi mshahara, kwa mfano: kama mimi napokea mshahara sh laki moja basi yeye anapokea laki mbili-ukijumlisha na house allowance, transport na pesa nyingine zisizo na kichwa wala miguu.

Hii kiukweli siipendi kabisa toka muda mrefu kama mwanaume, sasa nimekuja na mkakati ufuatao wa kumzidi kipato mke wangu nitahitaji mawazo yenu.

Nataka nimshauri mke wangu aende akachukue mkopo bank (mkubwa tu kwa mshahara wake) na baada ya kumchukua mkopo ukichanganya na akiba tuliyonayo nataka tufungue kampuni( tayari nimeshaanza michakato michakato)

Ambayo mimi nitakuwa msimamizi mkuu wa uendeshaji wa kampuni. Mapato yote yatakayokuwa yakiingia mimi ndio nitakuwa controller kwakuwa yeye kazi yake inambana sana na hawezi kupata nafasi ya kufatilia kwa undani sana biashara inavyoenda.

Kwa mkakati huo hapo juu basi mke wangu atakuwa anakatwa pesa bank kutoka kwenye mshahara wake (kwa miaka mitano mfululizo) huku mimi mshahara wangu ukiwa vile vile-hapo nitakuwa nimeshampiga pigo la kwanza

Kwa kipindi hicho chote mi ndio nitakuwa controller wa ofisi na mpaka inaisha hiyo miaka mitano ya kukatwa pesa ya mkopo na bank basi kampuni yetu itakuwa imekwisha simama na ina generate faida nzuri hivyo hata akishamaliza mkopo na kuanza kulipwa mshahara wake mi nitakuwa naingiza pesa nyingi kwenye kampuni-Pigo la pili

Kampuni isipofanikiwa nitafanya nini?
Nitanunua kiwanja, baada ya hapo nitamwambia akachukue mkopo tena bank mkubwa mara dufu ya ule ambao atalipa hata kwa miaka 10, kisha tunajenga apartments za kupangisha mi ndio nitakuwa mpokeaji wa kodi.

Mwanamume ni mwanaume tu wadau na usikubali mwanaume tu.Wadau usikubali mkeo aukuzidi pesa atakuwa na kiburi

Karibuni
 
Tatizo mfume dume umekutawala ,maendeleo yanakuwa ni shida kidogo
 
Bangi ni mbaya sana.
 

Attachments

  • 1427308377270.jpg
    1427308377270.jpg
    47.4 KB · Views: 563
Back
Top Bottom