Mimi nafikili jamaa ndio mwenye matatizo si mkewe, hapa hatuelezi kila kitu - na wala sioni kama huyo mwanamke ana nia thabiti ya kuua, anatishia tu baada ya kuchoshwa na nyenedo za jamaa.
Mkuu kumbuka wanawake wana inbuilt instinct za ajabu sana, sio za maternal peke yake wanaweza vile vile kuhisi by 99.5% kama mwanamume ana mahusiano nje ya ndoa - Sasa ku-act/react kunategemea hulka ya mwanamke zilivyo, kuna wanao weza kuhisi wakakaa kimya au kupeleleza pole pole wakisha pata uhakika na wao wanalipiza kisasi kwa kuanzisha mahusiano nje ya ndoa bila ya kujali wajihi/sura/class na anaye tembea naye - yeye anachotafuta ni kulipiza kisasi basi!!! Sasa wengine kama huyu dada hawafanyi hivyo, wanastick kwenye ndoa zao bila ya kuteteleka, lakini wakihisi wanasalitiwa na waume zao wana-react kwa hisia kali sana, oh yes wakati mwingine wanaweza kuua bila ya kukusudia.