Wadau Ilikuwa ni hatari kusikia Mwanamke anatukana Matusi kama MHSENGE na Nyoko" wakati mama mzazi wa mumewe anasikiliza na hatimaye akaamua kuaga hiyo familia na kuondoka arudishwe kijijini.
Mumeo akiwa amelala sms ikaingia kwenye simu aliyoiweka mezani sebuleni. Mke akaisoma na Kuingia Chumbani kutoa kichapo cha maana na kumung'ata Meno.
Kisa cha hayo yote ni sms aliyo ikuta kwenye simu ya Mumewe iliandika [" Uko wapi?, Nimekumiss sana, Usiku mwema]
Je, Mshahara wa hiyo sms ni kung'atwa memo na matusi?:angry:
Kwa mtazamo wangu,uhusiano kati ya mtu na mtu inategemea pia lugha mnayotumia,
mfano wanywaji wa pombe wana lugha yao,ma infid... Wana lugha yao, walokole sijui wacha Mungu wana lugha yao nk nk,
Sasa inaonekana hawa ndugu mazingira yao yana lugha ya matuc, mke kumtukana mume,mume kumtukana mke ni kawaida, wakati mtu akifurahi kinywa kinatoa tusi,akichukia tusi.
Ndo maana hakuwa na brake ya kutoa hilo tusi mbele ya mm mkwe, ndicho kilichoujaza moyo wake, ikisukumwa tena na hasira inakuwa hasara kabisa.
Kuhusu msg si bure lazima kutakua na kitu nyuma ya hio msg, manake ka ni hivo watu tusiwamic hata kaka zetu kwa sababu wameoa? Tusiwatakie usiku mwema?
Lazima atakuwa anajua imetoka wapi na nini maana yke, ikafufua hasira iliokuwepo moyoni mwake. Lakini kaka UPENDO HUSITIRI WINGI WA MAKOSA, kama wampenda msamehe.