Nimemkimbia mke baada ya baba mkwe kutaka kuniadhibu bakora mbele ya mke na mama mkwe

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Aise, kwa hili hapana. Sikuwa tayari! Hata mzazi wangu asingeweza kunifanyia ukatili wa namna hii

Ni stori ya kitambo kidogo (2019), miezi sita baada ya kufunga ndoa, nilifuma sms za mapenzi kwenye simu ya mke. Kwa kuwa mimi si muongeaji ilinibidi nitunze jeraha moyoni

Kuna siku wafanyakazi wenzangu waliandaa party la pamoja, hivyo nikaalikwa kama mmoja wao. Sikuwa na mazoea ya kupiga maji zaidi ya chupa moja la Serengeti, lakini hiyo siku niligigida za kutosha kutokana na influence za marafiki zangu. Nakumbuka hiyo siku nilikanyaga za kutosha na za kila rangi

Niliposhtuka mida ya saa 11 alfajiri nilijikuta nimelala nje kolidoni. huku kifurushi cha nguo kikiteketea mbele yangu. Baada ya kuingia ndani nilikuta vitu viko vurugu vurugu, mke sikumkuta.

Ilivyofika saa nne asubuhi, jirani yangu mmoja alikuja na kuanza kunihoji hoji kuwa kwa nini jana nilikuwa kwenye hali ile? Baada ya kumuuliza vizuri kilichotokea, akasema usiku huo nilichachamaa sana huku nikizunguka zunguka na mkanda mkononi, nikipaza sauti kumlaumu mke kwamba ile namba inayoishia 88 ni ya nani? Baada ya hapo nikachukua nguo zake na kuzirarua kwa meno, nikaona haitoshi nikaziteketeza. Akaendelea kwa kusema kuwa mke akawa amekimbia

Siku ya tatu ya tukio nikawa nimeitwa nyumbani kwa binti. Huko nilikutana na baba mkwe akiwa amejawa na hasira kali hata salamu akashindwa kuitikia, hivyo nikawekwa mtu kati kutoa maelezo. Mwisho wa siku ilitolewa hukumu ya eti ili nirudiane na cheupe wangu itabidi nicharangwe viboko ishilini mbele ya mke na mama mkwe pamoja na wajomba. Wakadai kichwa nitatakiwa kukilaza juu ya gamba la kobe lililokuwa tayari uwanjani huku mkono wangu wa kushoto ukishikilia mkia wa ng'ombe ili mizimu ya ukoo itulize jazba. Yaani niache mpododo wangu juu mbele ya mama mkwe?!! Hapana kwa kweli

Nikaomba kwenda msalani kujiandaa kwa ajili ya viboko hivyo. Kilichofuata nikatokomea huko huko

Kilichonifanya kukumbuka, jana asubuhi nimekutana na cheupe wangu akiwa amempakata cheupe mdogo. Alivyoniona amecheka sana na kuniambia kwa sasa yeye ni mke wa mtu. Nimemuomba kupasha kiporo amenikubalia weekend hii

Tumshukuru mama
 
i ulikuwa upo sahihi na bado unaweza kuwafungulia kesi,mwanamke alitakiwa aende Kwa wazazi wako wewe na sio kwao,kwenda kwao tafsiri yake ni kuwa ametoroka,inategemea pia mliishi Kwa mkataba gani
 
Ni udhalilishaji sana, bora ulivyokimbia tu,

Hii story imewahi kumkuta mtu wangu wa karibu na mwanaume alimuacha mazima, na hii inafanyika kwa familia zinazojiona miungu watu
 
Aise, kwa hili hapana. Sikuwa tayari! Hata mzazi wangu asingeweza kunifanyia ukatili wa namna hii

Ni stori ya kitambo kidogo (2019), miezi sita baada ya kufunga ndoa, nilifuma sms za mapenzi kwenye simu ya mke. Kwa
Daaaah ndiyo maana kampeni ya kukataa ndoa imekuwa kubwa sahv hadi Mimi imenifikia..nipo tayari kuwa mweka hazina wa hiki Chama bila kulipwa mshahara Kwa muda wote wa utumishi wangu
 
Aise, kwa hili hapana. Sikuwa tayari! Hata mzazi wangu asingeweza kunifanyia ukatili wa namna hii

Ni stori ya kitambo kidogo (2019), miezi sita baada ya kufunga ndoa, nilifuma sms za mapenzi kwenye simu ya mke. Kwa kuwa mimi si muongeaji ilinibidi nitunze jeraha moyoni

Kuna siku wafanyakazi wenzangu waliandaa party la pamoja, hivyo nikaalikwa kama mmoja wao. Sikuwa na mazoea ya kupiga maji zaidi ya chupa moja la Serengeti, lakini hiyo siku niligigida za kutosha kutokana na influence za marafiki zangu. Nakumbuka hiyo siku nilikanyaga za kutosha na za kila rangi

Niliposhtuka mida ya saa 11 alfajiri nilijikuta nimelala nje kolidoni. huku kifurushi cha nguo kikiteketea mbele yangu. Baada ya kuingia ndani nilikuta vitu viko vurugu vurugu, mke sikumkuta.

Ilivyofika saa nne asubuhi, jirani yangu mmoja alikuja na kuanza kunihoji hoji kuwa kwa nini jana nilikuwa kwenye hali ile? Baada ya kumuuliza vizuri kilichotokea, akasema usiku huo nilichachamaa sana huku nikizunguka zunguka na mkanda mkononi, nikipaza sauti kumlaumu mke kwamba ile namba inayoishia 88 ni ya nani? Baada ya hapo nikachukua nguo zake na kuzirarua kwa meno, nikaona haitoshi nikaziteketeza. Akaendelea kwa kusema kuwa mke akawa amekimbia

Siku ya tatu ya tukio nikawa nimeitwa nyumbani kwa binti. Huko nilikutana na baba mkwe akiwa amejawa na hasira kali hata salamu akashindwa kuitikia, hivyo nikawekwa mtu kati kutoa maelezo. Mwisho wa siku ilitolewa hukumu ya eti ili nirudiane na cheupe wangu itabidi nicharangwe viboko ishilini mbele ya mke na mama mkwe pamoja na wajomba. Wakadai kichwa nitatakiwa kukilaza juu ya gamba la kobe lililokuwa tayari uwanjani huku mkono wangu wa kushoto ukishikilia mkia wa ng'ombe ili mizimu ya ukoo itulize jazba. Yaani niache mpododo wangu juu mbele ya mama mkwe?!! Hapana kwa kweli

Nikaomba kwenda msalani kujiandaa kwa ajili ya viboko hivyo. Kilichofuata nikatokomea huko huko

Kilichonifanya kukumbuka, jana asubuhi nimekutana na cheupe wangu akiwa amempakata cheupe mdogo. Alivyoniona amecheka sana na kuniambia kwa sasa yeye ni mke wa mtu. Nimemuomba kupasha kiporo amenikubalia weekend hii

Tumshukuru mama
Utoto Kama utoto
 
Alikuja kuolewa na yule yule Jamaa ambaye namba yake inaishia na 88?
 
Sidhani mkuu, according to their chats, ilionesha wazi kuwa yule 88 ni mume wa mtu. Huyo mwamba aliyemuoa inasemekana hakuwa na mke hapo awali (maelezo ya binti tulipokutana tena)
 
Ni udhalilishaji sana, bora ulivyokimbia tu,

Hii story imewahi kumkuta mtu wangu wa karibu na mwanaume alimuacha mazima, na hii inafanyika kwa familia zinazojiona miungu watu
Na kweli mkuu, familia za kitamaduni na mizimu. Zile za ili ndoa ifungwe ni lazima ukamwagilie mbege kwenye makaburi ya wazee kisha kuyasujudia

Bado tuko nyuma sana waafrika
 
Back
Top Bottom