Mke wa Tundu Lissu apewe tuzo

bmk

JF-Expert Member
Jan 27, 2015
571
857
Wajumbe?!

Nimeguswa kuandika hii thread, ukizingatia leo tunampokea Tundu lissu niliyempa jina la "Muujiza unaoishi".

Natambua sana kuwa wanawake ni wavumilivu sana sana hasa kwenye shida ngumu wanazopitia. Lakini leo nitambue uwepo wa Mke wa tundu Lisu kama mpambanaji aliyekuwa beneti na mumewe wakati wote wa shida zilizomkuta Lisu.

Tumeona karibu miaka yote hii akiwa na mumewe beneti mpaka sasa tunaona Lisu anatembea akiwa mzima. HUU NI USHUHUDA MKUBWA sana.

Ningependa Bavicha, waandae tuzo maalumu kwa ajili ya mke wa Lissu. Kwani ni mpambanaji anayestahili kupewa tuzo.

Ahsanteni.
 
wewe mke mwenza umepewa? au unapigia debe mke mkubwa tu
.
images-2.jpg
 
Huu ni moja wa mfano wa ile kauli ya "kwashida na Raha" sio wote wangeweza hili.
 
Lkn cha ajabu Tundu Lisu mwenyewe hamthamini Mke wake kabisa, kwani hajawahi kumtaja wala kumshukuru popote pale, Tundu Lisu ni Binadamu selfish sana siajabu akisoma huu uzi hata akanuna kwa wivu kwamba sasa Mke anasifiwa na sio yeye, huyu jamaa ni kama mtoto, ...
 
Ya kuwa mke?.. hii oyooooo
Naona leo mumepokea 💉💉💉mumeshushuka.. 😃😃😃
 
Hata mke wa Lowasa si hivyohivyo jamani. CCM wapo wote, ukawa wapo wote wanarudi ccm wapo wote, wanamdhamini Magu wakiwa jimboni kwao wapo wote, hivi mnatakaje tena?
 
Ni ukweli, ila halitakiwi kufanywa jambo la kichama. Ni la familia, libakie huko. Wakianza kuchanganya mambo ya familia na chama, itakuwa shida....mambo yanabadilika, changamoto za ndoa haziishi, leo wanapendana, kesho wameachana, ....ups and downs! Ni mke mwema sana na jasiri sana, lakini hilo halina uhusiano na chama/siasa. Ni maoni yangu tu.
 
Lkn cha ajabu Tundu Lisu mwenyewe hamthamini Mke wake kabisa, kwani hajawahi kumtaja wala kumshukuru popote pale, Tundu Lisu ni Binadamu selfish sana siajabu akisoma huu uzi hata akanuna kwa wivu kwamba sasa Mke anasifiwa na sio yeye, huyu jamaa ni kama mtoto, ...
Bila Shaka inakuuma lissu kurudi bongo

Kanye boga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom