Mke wa pili ...!A curse or blessing?

huo msemo sina uhakika nao,kwa mifano yangu mimi,wapo waliooa mke wa 2,maisha yakawaendea vyema kuliko mwanzo,na wapo waliooa mke wa 2,maisha yakawaendea vibaya.kwa hiyo ni mchanganyiko.na huku niliko,talaka kila kukicha na kama sio talaka basi watu wanaongeza wake wa 2,na wengi waliofanya hivyo,kimaisha sijawaona kutatareka,wengi ni hard work na maisha yao ni mazuri tu.ila kwa mfano wangu wa karibu,my father aliongeza mke na akatutelekeza kabisa,mama yetu alikuwa single mum kwa miaka yake karibu yote.kwa sasa baba yupoyupo tu,na huyo mke wake,yeye ana kipato kizuri kabisa,hataki kumuona baba tena.na kwa upande wa mama yetu,mambo yake sio mabaya.

Hapo tunakwenda sawa ni ukweli hata na mimi nakubaliana na hilo kumuacha mke wa kwanza huleta shida sana
 
huo msemo sina uhakika nao,kwa mifano yangu mimi,wapo waliooa mke wa 2,maisha yakawaendea vyema kuliko mwanzo,na wapo waliooa mke wa 2,maisha yakawaendea vibaya.kwa hiyo ni mchanganyiko.na huku niliko,talaka kila kukicha na kama sio talaka basi watu wanaongeza wake wa 2,na wengi waliofanya hivyo,kimaisha sijawaona kutatareka,wengi ni hard work na maisha yao ni mazuri tu.ila kwa mfano wangu wa karibu,my father aliongeza mke na akatutelekeza kabisa,mama yetu alikuwa single mum kwa miaka yake karibu yote.kwa sasa baba yupoyupo tu,na huyo mke wake,yeye ana kipato kizuri kabisa,hataki kumuona baba tena.na kwa upande wa mama yetu,mambo yake sio mabaya.

kwahiyo "Kuoa tena " ni balaa - right?
 
It all depends.

Kama ambavyo mwanaume ambae amejitahidi kujikomboa kimaisha anaweza akafanikiwa zaidi/baki palepale au akaanguka baada ya kuoa kwa mara ya kwanza ndivyo inavyoweza kua kwa ndoa ya pili au hata ya tatu.

Attitude na ability ya mwanamke kwenye kuongoza ndoa yake ni INDEPENDENT VARIABLE..inainfluence maendeleo ya mwanaume ambayo in this case ni DEPENDENT VARIABLE.Hii ipo kwenye ndoa zote...iwe ya kwanza au ya kumi.

Baadhi ya sababu zinazoweza kufanya mke yeyote (wa kwanza ama wa tano) asababishe maendeleo ya mume wake yapungue ni :
1. Matumizi mengi.
Ukioa mwanamke ambae anajua kwenda dukani na kununua tu vitu hovyo bila mpangilio na kuzingatia kipato chenu lazima maisha yataenda ndivyo sivyo.
2. Asiejua kujituma.
Kama mwenzako hachangii chochote wakati mwanzoni matumizi yalikua kwaajili yako tu alafu ukazidisha matumizi mara mbili na kipato ni kile kile kitakachobaki kwaajili ya maendeleo hakitakua kingi kama mwanzo hivyo kudhorotesha maendeleo kwa muda mpaka kipato kitakapoongezeka.
3. Mwanamke asie na akili ya maendeleo.
Ni muhimu kuwa na mtu anaeku-encourage kufanya mambo makubwa ambayo binafsi unaweza dhani huwezi. Sasa ukikutana na ambae hajali na hana muda wa kufikiria wala kujadiliana kuhusu maendeleo (na wewe ni mmoja wa wale watu wanaohitaji “a little push/encouragement “ now and then ) imekula kwako.
4.Kuongezewa majukumu zaidi ya ulivyopanga.
Kama mwenzako anategemea usomeshe na kulisha familia yake bila kujali maisha yenu binafsi na ukafanya hivyo wakati haikua kwenye mahesabu yenu...mahesabu yataenda vibaya.
5. .........

Sasa ukikutana na mwanamke wa aina hii iwe ni kabla au baada ya kuoa na kuachana na mwenzako lazima watu waseme mwanamke yule kamharaibia fulani maisha au kamloga.

Naelewa pale mwanaume aliyekua na bahati ya kukutana na mwanamke mzuri (mwendelezaji) na kumuoa alafu baadae akaja kupata ambae sio “mwendelezaji“ akiwa na mawazo uliyotoa. Ila tatizo ni kwamba kulaumu ndoa ya pili badala ya uliyeingia nae kwenye hiyo ndoa ya pili hakusaidii wala hakutoi mwangaza wa wapi lilipo tatizo ili uweze kulitatua. Hivyo utaishia kulaumu kitu ambacho sicho badala ya kutafuta kile ambacho ndicho na kukiELIMINATE.

Mpaka hapa binafsi siungi mkono hoja kwasababu wapo watu nnaowafahamu kuoa mara ya pili hakujaharibu chochote...wengine mambo yamekua mazuri zaidi na wengine ndo kama hivyo tena walishuka daraja kwenye kuchagua mke wa pili when it comes to maendeleo issues. Usitegemee miujiza sehemu ambayo haihitaji miujiza...jua ukiachana na mke ambae alikua anasaidia sana maendeleo yenu iwe ni kwa kipato chake au mawazo tu alafu ukajachukua ambae hajua kuchuma anajua kula tu lazima matunda yataisha ndani maana hayajileti yenyewe....

Kwahiyo ombeni tu mkifanya kosa ya kwanza msifanye kosa na mara ya pili au hata ya tatu...na kama ulibahatika mara ya kwanza omba ubahatike na mara zitakazofuata usije ukachanganyikiwa bure.
 
In most cases ndoa halali si vema kuivunja kwa sababu zozote zile mkingali hai, kweli ni kualika laana maishani mwenu, na laana hiyo haikawii,just a few years unaanza kujuta

Yah unachosema naweza kukubaliana na wewe bt kuna matatizo mengine hayavumiliki ndani. Mimi nina mfano hai kabisa, dadangu aliachana na mumewe kisheria kbsa (mahakamani) na dadangu huyu hakuchukua kitu chochote( kwenye mgawanyo wa mali) walichochuma na mumewe vyote alimuachia, its 4yrs tangu tukio hili limetokea, shemeji yetu akaoa mwanamke mwingine, hivi ninavyoandika hapa, mke 2 keshamuacha, mali zote hata moja hana, amebakiza kumbembeleza dada yetu warudiane na dada yetu huyo mambo yake sasa hivi ni supa.
 
wala sio kweli,mie baba na mama yangu waliachana na mama akamnyang'anya baba nyumba zote allikuwa hana mahali pa kuishi ila sasa ana nyumba nzuri tu kushinda hizi zetu,ana magari mawili na kamfungulia mkewe miradi ya bar na saloon nayo inafanya vizuri tu
 
Yah unachosema naweza kukubaliana na wewe bt kuna matatizo mengine hayavumiliki ndani. Mimi nina mfano hai kabisa, dadangu aliachana na mumewe kisheria kbsa (mahakamani) na dadangu huyu hakuchukua kitu chochote( kwenye mgawanyo wa mali) walichochuma na mumewe vyote alimuachia, its 4yrs tangu tukio hili limetokea, shemeji yetu akaoa mwanamke mwingine, hivi ninavyoandika hapa, mke 2 keshamuacha, mali zote hata moja hana, amebakiza kumbembeleza dada yetu warudiane na dada yetu huyo mambo yake sasa hivi ni supa.

Huo ndiyo uharibufu wa mke afuataye! So it is curse?
 
wala sio kweli,mie baba na mama yangu waliachana na mama akamnyang'anya baba nyumba zote allikuwa hana mahali pa kuishi ila sasa ana nyumba nzuri tu kushinda hizi zetu,ana magari mawili na kamfungulia mkewe miradi ya bar na saloon nayo inafanya vizuri tu

Kwa kifupi Mama yako "ameharibikiwa"? siyo?
 
Kweli kabisa, jinsi unavyozidi kuongeza mke ndivyo majukumu unayazidisha. Mimi napendelea kuwa na mke mmoja tu. Sema inabidi mtu uwe makini kumchagua maana one mistake, one goal.

Ni kweli kabisa kaka Apollo yaani kama kuna mahali pa kuomba sana ni kabla ya kufanya uchaguzi wa mke au mume maana one mistake one goal na itaathiri sana future yako kama utafanya mistake. Omba sana sana kwa kufunga Mungu akujalie
 
ee mwenyezi mungu nisaidie nisiolewe mke wa pili wala kuwa mama wa kambo nijalie nyumba yangu mwenyewe amina
 
Hapa naongelea wanaume wanaofanya maamuzi ya kuachana na wake zao na kuoa mke mwingine au wake wengine - kutokana na sababu wanazozijua wao. Kwa waliofiwa na wake zao - poleni sana - hii mada haiwahusu au kama itawagusa - samahani sana...

Baada ya kufatilia kwa takribani miaka 40 - ndiyo arobaini na ushee - nimeonelea kuwa wanaume wengi ambao wameoa mara ya pili au zaidi wamekubwa na misukasuko mingi ya kimaisha kuliko wale ambao wamekuwa kwenye mahusiano ya ndoa na mke mmoja tu. Wanaume wengi ambao wameo mara ya pili au zaidi "wameharibikiwa" sana katika maisha katika njia nyingi mbalimbali....

Ninayo mifano zaidi ya 50 ya wanaume ambao "wameoa tena" na uzee wao umeishia pabaya sana ... Wengi wamegeuka kuwa ombaomba na masikini wa kutupwa pamoja na kwamba kabla ya "kuoa tena" walikuwa na maisha mazuri ya wastani au ya juu...

Ninapenda kuuliza, "kuoa tena" ni kujongezea mabalaa au ni changamoto za maisha...

Note: Wale ambao wanweza kuoa zaidi ya mwanamke mmoja kuishi nao hamuhusiki hapa...
Topic ni nyeti lakini ameileta kwa uchambuzi wa kitoto na wajuujuu, na haishawishi kuwa ameifanyia kazi, bali anapiga gumzo tu! lete data mzee na scope ya utafiti wako siyo ku-generalise issue kwani mtu mmoja akiumwa na nyoka wkt anapita njia fulani si lazima watakaopita baadaye huko ama kabla pia yaliwasibu vivyo hivyo!
 
Yah unachosema naweza kukubaliana na wewe bt kuna matatizo mengine hayavumiliki ndani. Mimi nina mfano hai kabisa, dadangu aliachana na mumewe kisheria kbsa (mahakamani) na dadangu huyu hakuchukua kitu chochote( kwenye mgawanyo wa mali) walichochuma na mumewe vyote alimuachia, its 4yrs tangu tukio hili limetokea, shemeji yetu akaoa mwanamke mwingine, hivi ninavyoandika hapa, mke 2 keshamuacha, mali zote hata moja hana, amebakiza kumbembeleza dada yetu warudiane na dada yetu huyo mambo yake sasa hivi ni supa.

Yaani kaka ram unayosema ya dada yako yamewafika wengi mmoja wapo ni mimi hapa ninayeandika hapa. Yaani kuachana na mume /mke wa kwanza mara nyingi ni laana maana Mungu mwenyewe alisema kwenye BIBILIA nachukiia kuachana kwenu. Mimi niliolewa kwa ndoa ya Kanisani tumekaa kwa amani miaka 3 ule wa nne maneno yalianza tokea kwa ndugu wa mwanaume "hazai , hazai" nasikia alikuwa malaya. Mimi nikasikitika sana kwamba maisha yangu nilitulia na kufundishwa na wazazi kwamba nikiguswa guswa na wanaume nitpata ujauzito. Kwahiyo nikasoma nikamaliza bila kuguswa mpaka nikaolewa. Laajabu miaka 4 imepita hakuna mtoto, na mwenzangu kwa vile makabila ni tofauti akaanza kuletewa maneno ya uongo akayasikiliza mpaka mwaka wa 5 tukatengana hakuna chakula hakuna matumizi ni mimi kila kitu mpaka nikaanza kupigwa bila sababu basdaye nikajiondoa baada ya kipigo kikubwa cha mwisho. Kwa ufupi mwenzangu alikuwa na msichana mkerewe walikuwa naye siku tele zilizopita. Basi wakakaa sana wanafanikiwa tu mimi maisha yangu yalikuwa kawaida tu. Mpaka siku moja nikaamua kufungua case mahakani baada ya kugundua kwamba waliisha funga ndoa Bomani. Case ikanguruma akaulizwa umefungaje ndoa na huku una ndoa nyingine?. Akafanya mipango case ikahamishiwa ADR Kisutu yaani mimi through wakili wangu alihongwa hela akasaini case iende kuvunjwa.....
Case ikavunjwa bila hata kusikilizwa neno lolote nikalia mahakamani wenzangu walikuja wamekamatana kama kumbi kumbi mahakamani wananicheka. Basi nikaambiwa halali yako mama ni laki 5, mwenzako atapata wapi hela za kukupa?. Nikasema mimi sichukuwi hizo hela nikatoka mahakamani nikaacha hata kufuatilia tena talaka na wakili wangu alisaini kila kitu kwa niaba yangu.
Baada ya miaka 3, aliyekuwa mume wangu na mkewe wote waliachishwa kazi wakahama hapa mjini wakenda nje ya Dar karibu ma Moro huko wanalima na kuleta mazao kwa biashara hapa mjini. Mnamo mwaka 2004, aliyekuwa mume wangu alituma rafikye akiniomba nimsamehe maana kila anachofanya hakifanikiwi.......
Ndoa ni moja ila kuna zingine unashidwa inabidi uvunje ila ukivunja ndoa hakikisha huna makosa la sivyo utakiona cha mtemakuni.....
 
Ndoa ni taasis ya kwanza iliyoanzishwa na Mungu mwenyewe,kulingana nahii mada hapa tunaongelea wale ambao tunaamini ndoa moja mpaka kifo..
Ndoa ni code # ya mafanikio
Adam na Eva ndio mifano ya ndoa ya kwanza,Eva alimdanganya Adam wakala tunda (hilo ni kosa ambalo Eva alilitenda)lakini Adamu hakumuacha mkewe na hakuomba apewe mke mwingine pamoja na kuwa Mungu aliona mapungufu kwa huyu Eva ila maisha yaliendelea mpaka walipomaliza muda wao.Na sijawahi ona mahali waliposema Eva/Adam walipata wenzi wengine
Kiukweli mume aliyefunga ndoa kanisani haijalishi mke ana maarifa au hana mume hana kibali cha kuoa mwanamke mwingine kwa kisingizio chochote ,hii inatokana na kiapo kile mlichoapa madhabahuni pamoja mpaka kifo.(inatupasa kusimama sawasawa hapa)
Ila inashangaza sana kuona wakristo wa leo wanafunga ndoa (baadhi) baada ya mwaka unakuta eti wameachana na mtu ana mke /mume mwingine na eti wamefunga ndoa ya serikali hii inasikitisha sana,huwa najiuliza kitu gani kinakuwa kimekosewa ?ni malezi ? au hamna mafundisho ya kutosha kuhusu ndoa ?au ni nini hasa
Sisemi mke/mume awe tayari kunyanyasika lahasha –ila nyumba yoyote ile isipojengwa kwa maarifa huangamia!lazima tufike mahali hasa wamama tutambue nafasi na majukumu yetu katika kuokoa ndoa zetu hata za wapendwa wetu.Dunia ina watu wawli she/he na tabia zao almost ni zilezile ni heri kubaki na # 1 na sio #2.
Naunga mkono hoja

:drum:
 
@KAPONGO:

- Watoto hawaruhusiwi KUOA wala KUOLEWA!
- Unataka data gani? Au na wewe bado unatafiti?
- Hili ni swala linalogusa jamii mmoja kwa mmoja - Huitaji ku-defend Thesis hapa! Mimi nimetafiti familia moja baada ya nyingine kwa miaka 40!
- Hapa nilikuwa nataka kujua jamii nyingine zina uzoefu gani na "kufukuza mke na kuoa mke mwingine"?
 
Nakuongezea kwenye hiyo sample baba yangu. Toka ameachana na mama mambo yake valu valu wakati alimuacha akiwa young millionaire.

Unajua nini aliyekuwa nawe wakati unatafuta pesa atajua kuzitumia kuliko aliyezikuta kwani in most cases hao wake wapya wanakuja wakijua hapa ni kisima ela zachotwa tu. Mnaingia kwenye anasa badala ya kuishi maisha yale yaliyokufanya ukawa nazo. Na wanaume wengi wakioa dogo dogo wanabadili mfumo wa maisha na kujifanya wao ni kina Biligate

@Ashadii: Kuoa mke wa pili mambo yakanyooka siyo sustainable - onaweza ikawa miaka mitano lakini haitazidi kumi - unakuta mwanaume amerudi mpaka kuwa mdoeaji wa Bia. Ukifuatilia sana unaambiwa huyu aliachana na mke akaoa mke wa pili akajenga maghorofa, akanunua magari, lakini baada ya muda mambo yakaanza kuharibika...

Mke wa pili anaweza akakunyanyua lakini utabakia hapo lazima utarudi chini kwa kasi ya ajabu... Kaa chini piga hesabu ya "matajiri" unaowafahamu ambao wanaweza kuwa kwenye miaka ya sitini au zaidi kidogo - waliosimama mpaka sasa ukifuatilia sana lazima utakuta ni wale wenye ndoa ambazo "hawakuoa tena"!
 
Back
Top Bottom