Mke wa Mugabe aamrishwa kurudisha nyumba tatu

Mke wa Mugabe aamrishwa kurudisha nyumba tatu

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Jaji mmoja nchini Zimbawe amemwaagiza mke wa rais Robert Mugabe, Grace Mugabe, kurudisha nyumba tatu alizompokonya mfanyabiashara nmoja raia wa Lebanon, kufuatia zabuni ya pete ya almasi ya gharama ya dola milioni 1.35.

Kulingana na kesi iliyowasilishwa na mfanyabiashara huyo, Bi Mugabe alitaka kurudishiwa pesa baada ya pete hiyo ya almasi iliyonunuliwa mjini Dubai. ilipowasilishwa kwake baada ya kutengenezwa na mtu tofauti.
Grace Mugabe katika mzozo wa pete ghali ya almasi.

Mugabe: ''Nilikufa kisha nikafufuka''
Wakati Jamal Ahmed alishindwa kulipa pesa hizo kwa akaunti mjini Dubai, na licha ya yeye kusema kuwa pesa hizo zilitumwa kupitia kwa benki moja ya Zimbabwe, Bi Mugabe alichukua kwa nguvu nyumba zake tatu mwezi Oktoba.

Jaji Clement Phiri alisema kuwa Bi Mugabe pia ni lazima ahakikishe kuwa wafanyakazi wote waliokuwa wakihudumu kwenye nyumba hizo wamerudishwa kazini.

Pete hiyo ilikuwa ni kama zawadi kwa mke wa rais Mugabe, Bi Grace, kuadhimisha miaka 20 ya ndoa.
 
Hawa ndiyo Viongozi wa Afrika.Nchi zao ni masikini wa kutupwa Mfalme aka Rais anathubutu kutengeneza Pete ya $ 1.36 milioni na makabwela wanapiga makofi.Hakika aliyeturoga kafa
 
Back
Top Bottom