Mke wa mtu.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wa mtu....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, Jan 4, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Rafiki yangu ana ndoa ambayo sasa ina takriban miaka saba. Miezi miwili iliyopita alianiambia kuwa katika mizunguko yake alikutana na Dada ambae alitokea kuvutika nae ghafla..alifika ofisini kwake kwa madhumuni ya kutaka kufahamu iwapo anaweza kupata kazi. Rafikia yangu alimjibu tu kuwa hana hakika kwa sasa ila ampe namba yake ikitokea vipi atamtafuta. Hazikupita siku mbili rafiki yangu akasukumwa na sheetani la mahaba, akamtwangia yule dada, alipopokea akamweleza anamsalimu tu. Yule dada alionyesha uchangamfu na baada ya maongezi marefu katika simu rafiki yangu akaona kama anahitaji nguvu kidogo sana kumpata.


  Hazikupita siku mbili yule dada akampigia tena kuuliza kazi, rafiki yangu anamweleza labda amletee CV na ikiwezekana aweze kumtafutia sehemu nyingine zaidi..CV ikalewa. Rafiki yangu akaona atumie mwanya ule kumwaga itikadi zake, yule dada alionyesha kutomkatisha tamaa..akaimjibu, "sorry nitakuambia lakini sikutegemea" alipoondoka.

  Baada ya siku mbili, yule dada akampigia simu rafiki yangu, akiwa mchangamfu sana, alianaza na "Vipi dear najua upo job..eti ehee??" rafiki yangu akaona mambo shwari, nae akaitikia "job dear"..baada ya maongezi mafupi, yule dada akamweleza haya:

  :Hioney, nilikuwa naomba kama upo safi unisaidia kama ka milioni hivi, nashida, watoto wanadaiwa ada na sijui itakuwaje?" jamaa yangu aliposikia yale kengele ikagonga kichwani, hakutegemea:

  akatamka : "eh milioni, mbona, mbona, mbona hivyo.."

  Dada: "hivyo vipi..."

  Rafiki yangu: "duh, that's an up hill task kwangu kwa sasa, labda unipe kama ka mwezi hivi".

  Dada: "yaani huwezi??

  Rafiki yangu: "Naweza ila ..ila mambo si shwari kwa sasa na mimi watoto pale nyumbaniiiiiiiiii"

  Dada" yaani nakueleza watoto wanafukuzwa shule mpenzi hata kukopa sehemu huwezi.."
  Rafiki yangu: "Sawa, lakini sikutarajia hilo sasa, labada kama ..."

  Kabla hajamaliza yule dada akamfyatukia : " Wewe unashindwa ka milioni tu, je uliponitamani unajua mwanaume mwenzio anatoa ngapi kunitunza mimi na watoto, ?? Hivi kama mimi nitaachika kwa mume wangu kweli unaweza kunimudu kama ka ada tu ka watoto kanakushinda??"" Unadhani kila mwanamke unayemuona kima cha mkia wa mbuzi ehe, wengine ng'ombe babuuu!!., ukome kutongoza tongoza wake za watu"

  Akakata simu!!.

  Rafiki yangu anasema baada ya hapo alitafakari sana Moyoni kauli zile alizozisikia toka kwa yule mwanamke..na akajiona kumbe kachemka sana..na kujisemea "kumbe mke wa mtu ni ghali namana hii?"...
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Humu JF kuna pepo linalotuma wanaume kufuata wake za watu! Si bure
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tamaa zitawaua!!!
  Mwambie nae wakwake si ajabu wanalipiwa ada.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Ndio, ghali ni aghali.
   
 5. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hahaha alikomaje teh.
  anaona vyaelea anashoboka....... vimeundwa atiii.
   
 6. Bakulutu

  Bakulutu JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 1,919
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  na we kongosho paundi nagpi???
   
 7. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  eeh ndio mjue kuwa hizi k ni biashara...wee make money kula k na sepa ....lah sivyo itatukanwa na mwanamke ambaye sii lolote.
   
 8. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 852
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Duh! Ulivyoyanukuu hayo maongezi, kama ulikuwepooo! Au ni wewe Ngoshwe?? LOL!
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Ngabu's wife must be above suspicion.
   
 10. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Nahisi amesahau ule msemo usemao, "usione vyaelea vimeundwa"!!!!! :A S-coffee:
   
 11. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  dunia na vituko vyake!
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  And Ngabu must be by her side.
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Jan 4, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Most definitely, but her being above suspicion is a condition that must be met.

  I have uncompromising standards of morality. Therefore, she must be pure and honest in morals
   
 14. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hii story umeitoa wapi ??
   
 15. T

  Tall JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  kwani rafiki yake ngoshwe ni mwana jf??
   
 16. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,141
  Trophy Points: 280
  Mambo yale yale ya 'RAFIKI YANGU"
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  You shouldn't have to. Plus, a person that requires you to do so is simply not worth it.
   
 18. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Si ungemshauli akauze vitu ndani ampelee?uroho utamponza huyo.
   
 19. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Ni wanawake wachache sana Tanzania hii wenye msimamo kama huyu
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kutaka million ndio msimamo?
   
Loading...