Mke wa Mtikila ataka iundwe Tume kuchunguza kifo cha mumewe, Lowassa, Sumaye na Mnyarwanda watajwa

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
Mama-Mtikila.jpg


Hiki ndicho ameongea mbele za wanahabari:

Ndugu Wana-Habari,

Kabla sijawaeleza kilichonilazimisha kuwaomba kuongea nanyinyi, kwanza niwarudishe nyuma kama miaka saba iliyopita, ndipo maisha ya Baba, Mchungaji, Mwenyekiti na mume wangu, Mchungaji Christopher Reuben Mtikila yalipoanzwa kuwindwa:-

MAUWAJI YA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE

Mara tu baada ya kifo cha mbunge huyo, mchungaji Mtikila alitoa ripoti maalumu juu ya mauaji yake ambayo ilimjengea uadui kati ya baadhi ya vyama vya siasa pamoja na wafanyabiashara wakubwa ambao hadi leo ni wapinzani wa serikali hapa nchini.--Mchungaji Mtikila hadi anafikwa na mauti aliendelea kupata upinzani wa aina hiyo hiyo kwa sababu mchungaji Mtikila aliendelea kudai haki ya marehemu Chacha Zakayo Wangwe.

MAUAJI YA BULIGI

Hii ilimwongezea uadui baada ya kusema/kuandika ukweli juu ya watutsi wa nchi jirani kuvamia nchi yetu kwa mtindo wa kujifanya wafugaji wasio hama. L.I.F. ilibaini uharamia huo kuwa hawakuwa wafugaji bali walikuwa askari wa Jeshi la Rwanda waliokuwa na mpango wa kutumika na Chama kimoja cha siasa hapa nchini ili kuleta mapigano yatakayo zaa mapinduzi. Jambo hili lilisababisha Rais wa Rwanda, Paulo Kagame kutamka hadharani kuwa angemkamata Mwenyekiti wa chama chetu cha DP--kwa lengo la kumuua na Serikali yetu inajua hilo. Mara baada ya ripoti hiyo kutolewa na Mchungaji Mtikila "operation Kimbunga" ilizaliwa na kuponya nchi yetu; lakini chuki na uadui uliendelea dhidi ya Mchungaji Mtikila.

MCHAKATO WA URAIS NDANI YA CCM

Ikumbukwe kuwa mara baada ya mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM kuanza DP ilitoa ripoti iliyowahusu wagombea sita wa CCM waliotumia mapesa mengi na kuanza kampeni kabla ya muda na kusisitiza kuwa Lowasa ni mtu asiefaa kuwa Rais wa nchi yetu. Na baada ya kuhama CCM, Mwenyekiti wetu aliendelea kutoa tahadhari hadharani jinsi Lowasa asivyofaa kuwa Rais wa nchi yetu hivyo likaendeleza uadui wake na Chama.

VITISHO--KUANZA

Mchungaji Mtikila alipata nafasi ya kuongea katika kipindi kinachorushwa na STAR TV cha asubuhi "TUONGEE" ndipo alipoanza kupata vitisho toka kwa watu mbali mbali wengine kupitia kwenye simu wengine uso kwa uso. Kipindi cha kwanza kilirushwa tarehe 25/9/2015 na kufuatwa na cha tarehe 27/9/2015. Alipotoka studio hiyo asubuhi ya tarehe 27/9/2015 ndipo watu waliodai wametumwa na Mhe. Edward Ngoyai Lowasa na Mhe Frederick Sumaye walimuomba wampe nusu bilioni na apewe maovu ya mgombea urais wa CCM ili afunike-alivyowamaliza wao.

Mchungaji Mtikila aliwapuuzia mbali wale wajumbe waliyotumwa kwani aliawaambia kuwa yeye siyo malaya wa kuuza utu wake kwa tende na haluwa. Yakumbukwe kuwa mahojiano kwenye hivyo vipindi viwili kwenye STAR TV hayakuwa yanatetea mtu au chama yalikuwa yanatetea Taifa letu lipate Rais anayefaa.

Kwa hiyo basi wale waliochukizwa na mahojiano hayo ni wale amabo hawakubaliani na mawaidha ya Mchungaji Mikila aliyokuwa anawatahadharisha watanzania juu ya Mh. Lowasa kuwa hatari kwa usalama wa taifa letu kama atakuwa Rais wa nchi yetu. Hao watu ndiyo waliopanga mpango mzima wa mauaji ya Mh. Mtikila ambaye ni mume wangu.

Wakati yuko Bunda mjini watu wasiofahamika walimfuatafuata na tarehe 26/9/2015 gari lake lilifukuzwa na gari usiku wakati alipokuwa anatoka Bunda kwenda Mwanza kufanya mahojiano ya tarehe 27/9/2015 na Star Tv.

MPANGO WA MAUAJI HALISI

Mchungaji Mtikila alitafutiwa gari na Victor James Manyahi ambayo ilikuwa na madereva wawili. Mchungaji madereva hakuwajua. Hata mimi madereva hao sikuwajua wala sikuwaona. Walikodiwa kutoka wapi sijui, wala sijui wanafanana vipi. Na wala sijui Victor Manyahi alikodi gari hilo kwa nani na makubaliano yepi sijui.

Kwa hivyo basi, kwenye gari aliyosafiri nayo Mchungaji Mtikila kulikuwamo madereva wawili na Mgaya Patrick (tunayemfahamu). Wakati wanakwenda gari lilipata ajali Makambako. Wakati wanarudi wakapata "ajali" Msolwa Mchungaji akapatwa na mauti peke yake. Ajali ilikuwa mbaya sana-IKAUWA MTU MMOJA AMBAYE NI MCHUNGAJI MTIKILA NA HAKUKUWA MAJELUHI HATA MMOJA.-Cha ajabu kwangu ni kuwa mtu ambaye alikuwa ni mlinzi wa kujitolea (body guard) Mgaya Patrick sijawahi kumuona usoni mwangu kabla na hata baada ya mazishi kuja kuniambia kilichotokea eneo la ajali. Pamoja na juhudi zangu zote za kumpigia simu mara kadhaa aje anijuze Mgaya Patrick hajatokea hadi sasa ndugu zangu wanahabari ninapoongea nanyi. Lakini si kwamba huyu mtu hayupo, yupo lakini sijaonana naye, kwa nini sijui. Je ndugu zangu wanahabari nimuweke Mgaya Patrick kwenye fungu gani?

Ndugu Wana-Habari, baada ya kuwaelezea yote hapo juu nakuja kwenye suala nililowaomba nikutane nanyi ili niongee mbele yenu kuwa sikubaliani na uchunguzi kuwa Mchungaji Christopher Reuben Mtikila amekufa kwa ajali. Sikubaliani na kazi ya Polisi kuwa wamefunga file lao kutokana na Post-mortem report kuwa mauti yaliotokana na ajali. Nafuta kabisa taarifa--iliyotoka katika gazeti la Nipashe chini ya kichwa cha habari kuwa "FAMILIA YAFUNGUKA KIFO CHA MTIKILA"-ilitolewa mapema mno. Kila mwanafamilia alikuwa hajawa tayari kutoa kauli yoyote. Kwa niaba ya Chama na familia ya Mchungaji Christopher Reuben Mtikila naomba tusaidiwe yafuatayo kusudi haki ya mpendwa wetu-ionekane--inatendeka:-

Kwa sababu mtandao umeanza kuficha ukweli ili kulinda wauaji; tunaomba Mheshimiwa Rais aingilie utata wa kifo cha Mheshimiwa Mchungaji Christopher Reuben Mtikila kwa kuunda tume ya uchunguzi isiyohusisha polisi.

Tunaiomba mamlaka ya mawasiliano yaani Tanzania Communications Regulatory Authority, TCRA itusaidie yafuatayo:-

(a)----Mtu aliyeweka picha kwanza alfajiri kuonyesha mauti ya Mhe Mchungaji Mtikila alikuwa wapi? Kwenye tukio? Au ni hao wauaji walikuwa wanatoa taarifa kwa waajiri wao kuwa wamekamilisha kazi!

(b)----Mtu aliyeweka picha ya Dr. Jean-Bosco Ngendahimana kwenye mtandao kuwa ndiye anahusika na mauti ya Mhe. Mch. Mtikila na kumusingizia kuwa amekamatwa na polisi akiwa anajiandaa kukimbia;

(c)-----Wote wanaoendelea kumhusisha Dr. Jean-Bosco Ngendahimana na mauaji ya Mhe. Mchungaji Mtikila, tuwafahamu ili watueleze vizuri.

Ukweli na haki ni vya Mungu hakuna anayeweza kuviua au kuvizuia. Tunategemea Mungu atawatumia watendaji wa Serikali/nchi yetu wenye nia njema, na makusudi yaliyonyooka kwa ajili ya nchi yetu ili Mhe. Mchungaji Mtikila apewe haki dhidi ya wauaji wake.

Asanteni,

Georgia C . Mtikila,

-KM DP/Msemaji-Familia
 
Gari akodi yeye mwenyewe kwa hela zake mwenyewe kutoka kwa mtu aliyemfahamu mwenyewe akiendeshwa na dereva aliyemchagua mwenyewe akaambatana na wachungaji wake mwenyewe kwa ujinga na ubishi wa kijinga akaamua kutofunga mkanda yeye mwenyewe dereva akajiendeshea kwa jinsi alivyotaka mwenyewe gari ikaacha njia na akajifia mwenyewe halafu leo mnaleta stori za kijinga!
 
Kwanza pole kwa msiba uliowapata, lakini sitaicha mada hii ipite bila kuichangia, kwenye mada yako kuna kipengele umekitoa kwamba marehemu alianza KUWINDWA.....na vitisho vilianza baada ya kumzungumzia Mh. Lowassa, mimi nafikiri nikujibu hivi... mtu kufikia mpaka kuwindwa lazima awe tishio kwa wapinzani wake,ambapo marehemu hakuwa na sifa hiyo....hakuwa tishio kwa chama chochote kikubwa au kidogo.... hakuwa na wafuasi wa maana ndomana hata mikutano yake alitumia TAX.... marehemu kazi yake ilikuwa ni kuchafua siasa badala ya kuijenga siasa alikuwa MWANA MAPINDUZI MPINGA MAPIDUZI....kila siku yeye na mahakama alikuwa anamshitaki kila mtu, kwa kweli kila anaye mjua kisiasa, alimchoka... watu wakimsikia wanataka kutapika...mahakamani jumatatu hadi ijumaa yeye ana kesi, angalia sasa kipindi kilichorushwa na Star TV..alitumia muda mwingi sana kumchafua Lowassa na kumdhalilisha badala ya kujenga hoja za kisiasa....!! ni kweli Lowassa mgonja lakini nauliza mbona bado yuko hai?? tumuachie Mungu..niwa ngapi hawakufikiriwa wagonjwa leo wamemtangulia mgonjwa wetu Lowassa?... nafikiri familia ya marehemu mumuombe mungu awaongezee BUSARA.
 
Mke wa marehemu Mch. Mtikila aibuka na kumuomba Rais Kikwete aunde tume ya kuchunguza kifo cha mme wake


Katibu Mkuu wa chama cha Democratic Party (DP) na Msemaji wa familia ambaye ni Mke wa marehemu Mchungaji Christopher Mtikila (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari mepema muda katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo suala la kutoridhishwa na ripoti ya jeshi la Polisi ambapo amemuomba Rais Dk. Jakaya Kikwete aunde tume huru ya kuchunguza kifo hicho. (Picha na Andrew Chale, Modewjiblog).​


Hatimaye Mke wa marehemu Mch. Christopher Mtikila, Bi. Georgia Mtikila mapema leo ameibuka mbele za waandishi wa habari na kumtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete anaunda tume huru haraka iwezekanavyo ilikupata ukweli wa kifo cha mmewe kwa kile alichokieleza kuwa ni cha mashaka huku uchunguzi huo wa jeshi la Polisi ukiwa hauna ukweli na wala haukutenda haki kwa familia hiyo.


Katika Mkutano huo, Bi Georgia alieambatana na viongozi wawili wa chama hicho akiwemo Kaimu Mwenezi wa chama hicho cha DP, Feruz Msambachako, ambapo ameeleza kuwa majibu ya ripoti ya Polisi wanamashaka nayo kama familia na hivyo wanataka tume huru iundwe kuchunguza hilo.


Mbali na kumuomba Rais aunde tume hiyo na kuja na majibu, Bi. Georgia ameomba mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, kuchunguza mtu aliyesambaza picha za awali kabisa zilizokuwa zinaonyesha mwili wa Mch. Mtikila huku akihoji kuwa mtu huyo ni nani na alikuwa wapi wakati wa tukio hilo muda huo ambapo amebainisha mtu huyo aliyesambaza kifo ashikiliwe ilikutoa ushirikiano.


Hata hivyo katika mkutano, Bi. Georgia alienda mbali na kuwataja baadhi ya viongozi kadhaa wakiwemo waliowahi kuwa Mawaziri wakuu wa Tanzania kuwa waliwahi kumtishia maisha mmewe kupitia watu waliotumwa kwa minajiri ya kumnyamazisha baada ya kutoa taarifa kupitia moja ya kituo cha habari nchini.


" Mchungaji Mtikila alipata nafasi ya kuongea katika kipindi kinachorushwa na …..(anakitaja kipindi hicho) cha asubuhi ‘Tuongee asubuhi' ndipo alipopata vitisho toka kwa watu mbalimbali wengine kupitia kwenye simu na wengine uso kwa uso.


Alipotoka studio hiyo asubuhi ya tarehe 25/9/2015 na kufuatwa na tarehe 27/9/2015, ndipo watu wawili waliodai wametumwa na …(Akiwataja hao Mawaziri Wakuu wa zamani wa Serikali ya Tanzania) walimuomba wampe nusu bilioni na apewe maovu ya mmoja wa wagombea kutoka chama cha siasa hapa nchini ilikufunika alivyowamaliza wao" alieleza Bi. Georgia na kueleza mengi zaidi ambayo pia alisambaza rundo la nakara za maelezo yake hayo iliyokuwa na karatasi tatu.


….endelea kufuatilia kwa taarifa zaidi juu ya habari hii
 
Gari akodi yeye mwenyewe kwa hela zake mwenyewe kutoka kwa mtu aliyemfahamu mwenyewe akiendeshwa na dereva aliyemchagua mwenyewe akaambatana na wachungaji wake mwenyewe kwa ujinga na ubishi wa kijinga akaamua kutofunga mkanda yeye mwenyewe dereva akajiendeshea kwa jinsi alivyotaka mwenyewe gari ikaacha njia na akajifia mwenyewe halafu leo mnaleta stori za kijinga!
Huyu ugumba ndio unamsababishia kupungukiwa hekima na busara.
 
Jk kuunda Tume sio tatizo kwake ,tatizo ni kusimamia mapendekezo ya Tume ..wewe mama umekosea timing kabisa Jk mwenyewe anahangaika Ccm ibaki madarakani hiyo Tume ataunda saa ngapi
 
si mmemtaja lowassa na sumaye sasa anaomba tume ya nini yeye apeleke ushahidi mahakamani lowasa na sumaye wakajibu mbona simple tu
kuna uzi wa evashari wa raia mwema ulipita humu ulisema kosa la polis tz kuwahisha kumiza hili

go go go gergia damu ya mmeo lazima uipiganiea mjane wewe na wenawake wote wakuunge mkono ktk hili
 
Acha kujitoa ufahamu,waambie waliokutuma wamfufue,jukwaa hili haliwezi kuwa ukumbi wa propaganda za mawakala wa magamba.

Msaada pekee ninaoweza kukupa kama mjane,ukimaliza arobaini ya mumeo naomba uni PM.Nimejitolea kukuoa ili nikupe matunzo uepukane na weweseko la kupoteza mwenza wako,ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom