Mke wa mfanyabiashara maarufu Dar kortini deni la Mil. 20

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Dina Mgala, mke wa mfanyabiashara maarufu wa maduka ya kufua nguo kwa machine jijini Dar, Khalid Laundry amefikishwa katika kizimba cha Mahakama ya Mwanzo, Ilala Mtaa wa Pangani akidaiwa kuingia mitini na Shilingi Milioni 22 za mjasiriamali anayejulikana kwa jina la Zenna Kengera au maarufu Anti Zena.

Kwa mujibu wa chanzo, mwaka 2020 Dina alijipatia kiasi hicho cha pesa baada ya kumlaghai mlalamikaji huyo kwamba angemrejeshea baada ya miezi sita ahadi ambayo hakuitekeleza.

Kwa mujibu wa chanzo, awali mwaka huo wa 2020, mlalamikiwa huyo alikwenda nyumbani kwa mlalamikaji na kukopa kiasi cha shilingi milioni 36 kwa mjasiriamali huyo na alipokuwa akipiga chenga kulipa, mwanasheria wa mkopeshaji alimwandikia barua ya kumkumbusha deni hilo na kulipa kiasi kidogo cha pesa kwa awamu, kinyume na makubaliano.

Iliendelea kudaiwa kuwa, baada ya kutoa ahadi nyingi bila utekelezaji, baadaye, mlalamikiwa akawa hapokei simu na mwishowe aliamua kuizua (block) namba ya mlalamikaji asimfikie kwa njia yoyote ile.

Hata hivyo, mlalamikiwa hakuwepo mahakamani siku ya tarehe 13, 2023 ambapo kesi yake ingetajwa kwa mara ya kwanza baada ya kutoa udhuru kwamba anaumwa.

Hakimu aliisogeza kesi hiyo hadi Oktoba 19, 2023 ambapo mlalamikiwa alitakiwa kufika bila kukosa ujumbe uliyotumwa kwake kupitia kwa mwakilishi wake?
 
Habari yako ina maswali mengi sana..
Mbaya zaidi na wewe ukamaliza kwa kutuuliza Swali sisi wasomaji.
 
Bora hiyo kesi ingekuwa ni ya wizi wa kuaminiwa, linapokuja suala la kukopeshana hapo danadana za mahakamani zitakuwa nyingi maana mkopeshaji sio taasisi iliyosajiliwa means inalipa kodi etc na dhamana ilikuwa ipi etc..Hizi kesi lazima ucheze nazo vizuri otherwise utapoteza zaidi na sheria mpya ya kukopeshana inaweza ikakugeuka..

Mambo ya kukopeshana kwa KUAMINIANA YAMEPITWA NA WAKATI, we kopesha lakini jua possibility ya kupoteza ni kubwa..ndio maana nchi jirani hapa mtu akikukopesha na asilipe huwezi mpeleka kwenye vyombo vya sheria maana utapata kesi kwanza wewe ndio maana inaishia watu kumaliziana mtaani au kufanyiana ukatili..
 
Back
Top Bottom