Mke wa Madaraka Nyerere Kugombea Ubunge CHADEMA - Jimbo la Kwimba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke wa Madaraka Nyerere Kugombea Ubunge CHADEMA - Jimbo la Kwimba

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Regia Mtema, Jun 18, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Jun 18, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu habari!

  CHADEMA imeendelea kujiongezea hazina ya wanawake wazuri wanaowania majimbo kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge mwezi Oktoba mwaka huu.

  Kati ya wanawake hao mmoja wao ni Leticia Nyerere mke wa Madaraka Nyerere mtoto wa hayati Mwl Nyerere.

  Mama huyu Leticia Nyerere anatarajia kuondoa hodhi ya Chama Cha Mapinduzi ambacho kwa kipindi cha miaka yote ya mfumo wa vyama vingi imekuwa ikitawala katika Jimbo hilo la Kwimba mkoani Mwanza bila mabadiliko yoyote ya kiuchumi na kijamii na maendeleo kwa ujumla.
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Inapendeza wanawake wanaanza kujitokeza zaidi, na cha kufurahisha hawasubiri viti vya 'upendeleo'.

  Ataweza kupambana na Bujiku Sakila? Naelewa kuwa naye ana upinzani ndani ya CCM kutoka kwa mtanzania mwenye asili ya kihindi Shanif Hirani (ambaye inaelekea ni tishio kwake)
   
 3. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kwakweli nawasifu kinamama wanajitahidi sana kisiasa hapo Tanzania. Chadema wanatakiwa wajipange vizuri sana hasa kwenye majimbo ambayo wagombea wao ni akina mama. Kinachonitia mashaka sana na bila kuwepo hisia yoyote ya kibaguzi ni hawa jamaa zetu wenye asili ya kiasia wanavyo pamba moto kuingia kwenye siasa wakati matukio mengi yanaonyesha kuwa wakishafika juu wanakua viungo hatari sana katika ufisadi. Hili ni jambo la kuangalia na kuwa makimi sana.
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  Jun 18, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Sakila hagombei tena amejikatia tamaa!

  Leo nilikuwa nazumgumza na Mama Leticia akaniambia kuwa yeye anatamani sana huyo mhindi apite ndio atakuwa mwepesi zaidi kwake, anadai kama angeweza kufanya kampeni ili apitishwe ndani ya chama chao angefanya hivyo.. Inasemekana huyo mhindi anamougopa Leticia..Lets wait and see!

  By the way mmeniudhi kuniletea sredi yangu huku ingawa ni ndio mahali pake. Watu hawaji huku hivyo ujumbe haufiki kwa wengi..Watu bado hatujalizoea jukwaa hili labda kwa kuwa wakati wake rasmi bado!
   
 5. b

  buckreef JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  GS,

  Mwambie huyo mama asijiamini sana, hao Wahindi wana njia nyingi sana za kuwarubuni wananchi. Unajua wananchi wamekata tamaa, hivyo yeyote anayeweza kuwajaza mifuko yao wanampa kura.
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  Jun 18, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kujiamini ni muhimu ila ni kweli kwamba isipite kiasi kwani kila jambo too much is harmfull.Mwaka huu hakuna rushwa sheria mpya ya gharama za uchaguzi,mya be itasaidia..lakini pia uwepesi wake hautokani na uhindi wake,ni sababu nyingine kabisa ambazo siwezi kuzisema in public.
   
 7. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  all along i was made to understand kwamba Leticia alimkimbia madaraka,reading all this i now assume this was not the case
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,184
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ndiyo kusema huyo Leticia anapenda miteremko siyo? Ataweza kazi kwa style hii ya kupenda vyepesi vyepesi? Hajiamini nini?
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Jun 19, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha,umenichekesha sana Kiranga.Kugombea sio mchezo,hata Pinda mwenyewe hawezi kukubali apelekewe mtu ambaye angempeleka puta katika kushinda kwake,kifupi ni kwamba kwenye ushindani wa siasa tunapenda wale wepesi wepesi,ofcoz kwenye politik huwezi kujiamini asilimia zote..Spika Sitta mwenyewe kajasho kanamtoka.hali ndio iko hivyo Mkuu.
   
 10. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Go Leticia go!
   
 11. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Huyu Mama anajiamini sana na si wa kukurupuka, kwa hivyo alivyosema ni just a portion ya kile kilichonyuma ambacho wakati wa kampeni CCM hawatamsahau. Makamba aka Baba ule mwezi wa kwanza, anatamani huyu mama agombee kupitia chama kilichoasisiwa na baba mkwe wake.

  Bravo Leticia!!
   
 12. Makalangilo

  Makalangilo Senior Member

  #12
  Jun 19, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Leticia Musobi Mageni go go go...mabukwimba!Mhindi kishashindwa,Chadema oyeeee!
   
 13. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kila la heri mama. Lakini nafikiri 50/50 ni kwa sisiem tu, kama nawao wataiweza!
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,184
  Trophy Points: 280
  Sasa kama anajiamini mbona anakuwa anasema anataka sana fulani apite kuwa mpinzani wake? Hii si alama ya mtu anayejiamini, hii ni alama ya mtu mwenye mashaka na uwezo wake na anayetaka mpinzani wake awe kibonde fulani.

  Mtu anayejiamini na anayefikiri ana uwezo atakwambia "mleteni yeyote mimi niko tayari".Nikisoma hii thread naona huyu mama ana favorites na wala hajiamini hivyo.

  By the way huyu mama akiweza kuchukua ubunge CHADEMA hii familia itakuwa imeweka rekodi CCM, Babu Nyerere ndiyo hivyo tena kutoa TANU mpaka CCM, Babu Mwingine Mageni (Upande wa Leticia) alikuwa Mwenyekiti wa CUF, Makongoro Charles alikuwa mbunge wa NCCR Arusha Mjini, Rosemary alikuwa (bado ni?) mbunge wa CCM, Na sasa Leticia anataka kugombea CHADEMA.

  Wametapakaa vyama vikubwa vyote kama sisimizi.
   
 15. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 16. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #16
  Jun 19, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Bado hujanipata tu?
   
 17. n

  nndondo JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Leticia go my sister this is your time , son of alaska acha cheap characterization of people, as we focus on bringing about positive change in our country we do not have time for cheap staff, let us look at leticia and support her on the basis of her strenghts we should thrive for positive vibes na kwa hili humu ndani patakua hapatoshi kama watu watadekeza mambo ya 'udaku' hayana nafasi hapa. Tumpe leticia hekima kama walizoanza kutoa wengine humu what should she be working on to rip success kwa sababu unlike mr alasta, yeye ameweka anachosema kwenye action
   
 18. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #18
  Jun 19, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Naona hujamuelewa son of Alaska.Tafadhali soma tena...
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,184
  Trophy Points: 280
  Labda ukijibu swali tunaweza kupatana.
   
 20. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #20
  Jun 20, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Haya bana umeshinda wewe ila huyu mama anajiamni kuliko unavyodhani..
   
Loading...