Elections 2010 Mke wa Madaraka Nyerere Kugombea Ubunge CHADEMA - Jimbo la Kwimba

19144_100229920007453_100000613353513_3411_1109588_n.jpg


Mkwe wa Nyerere aiandama CCM

[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Na Maregesi Paul, Mbeya

LETICIA Nyerere ambaye alikuwa mke wa mtoto wa Hayati Mwalimu Nyerere, Madaraka Nyerere, ameanza rasmi kampeni za kukibomoa Chama cha Mapinduzi (CCM) huku akiwataka wananchi wajiunge na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Leticia alianza kampeni hizo jana kwa kuhutubia wananchi katika Jimbo la Mbeya Vijijini.

Alihutubia wananchi wa vijiji vya Idunda na Galijembe na kueleza ni kwa nini alijiunga na CHADEMA na kuachana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) alichokuwa akikiunga mkono kwa muda mrefu.

Akihutubia mikutano ya hadhara katika vijiji hivyo vilivyoko Wilaya ya Mbeya Vijijini kwa nyakati tofauti jana, Leticia alisema amejiunga Chadema kwa vile anaamini ndicho chama kinacholenga kuwakomboa Watanzania.

"Mimi CCM naifahamu sana huenda kuliko Watanzania wengi wanaoiunga mkono ingawa haiwasaidii kwa namna yoyote.

"CCM ilikuwa na sifa enzi za Mwalimu Nyerere, lakini baada ya mzee huyo kipenzi cha Watanzania kututoka duniani, chama hicho kimepoteza mwelekeo na matokeo yake ndiyo maisha magumu na vitendo vya ufisadi tunavyovishuhudia kila kona ya nchi," alisema Leticia.

Katika maelezo yake, Leticia alitumia muda mwingi kuwashawishi wanawake kujiunga na CHADEMA kwa vile kitendo cha kuendelea kuishabikia CCM kitawafanya waendelee kufariki kila wanapopata ujauzito na wakati wa kujifungua.

Leticia ambaye kwa sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani, alisema baada ya kujiunga na chama hicho cha upinzani hivi karibuni, amejiona huru zaidi kwa vile sasa ana uwezo wa kuikosoa CCM ikiwa ni pamoja na kuwashawishi Watanzania wengine waachane na chama hicho tawala. Leticia alijiunga na Chadema hivi karibuni mjini Ngundu wilayani Kwimba, Mkoa wa Mwanza, baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Kabwe Zitto kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji huo wakati alipokuwa katika ziara ya Operesheni Sangara kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mbali na Leticia, mwingine aliyejiunga CHADEMA hivi karibuni akitokea katika familia ya Mwalimu Nyerere ni Vicent Nyerere ambaye ni mtoto wa kaka yake Mwalimu Nyerere.
[/FONT]​

Gazeti la Mtanzania


Vicent Nyerere yeye anatarjia kugombea jimbo la Musoma Mjini...
 
Karibu sana Kwimba kwetu; nitakuunga Mkono mama madaraka; pigana hadi kieleweke; moto wako usiishie Ngudu tu nenda hadi sumve mwanza muigeuzie upinzani; nitakuunga mkono hutakosa watu walau 10 niliowashawishi; we need a change and a change is coming; keep it up
 
Karibu sana Kwimba kwetu; nitakuunga Mkono mama madaraka; pigana hadi kieleweke; moto wako usiishie Ngudu tu nenda hadi sumve mwanza muigeuzie upinzani; nitakuunga mkono hutakosa watu walau 10 niliowashawishi; we need a change and a change is coming; keep it up

Hongera sana and thank you for ur support to her na kwa chama pia.
 
Back
Top Bottom