Mke wa Lukuvi kung'oka sababu ni nini?

Mke wa Lukuvi kung'oka sababu ni nini?

Kuna shida! Raisi wa Nchi mbele ya Kadamnasi anatamka kuwa Mkwe wa Waziri! Labda kama ndani ya ATCL kuwa wake zaidi ya wawili wa Mawaziri katika mazingira hayo unaweza kubaki kuona hali ya hewa ikoje. Lakini kama mkwe wa Waziri ni huyo mmoja kwa kweli huko nikudhalilishana na kama ni kwa wenzetu kauli ya Raisi siyo ya kiustaarabu na wala heshima. Ukizingatia mwenye mke ni sehemu ya Baraza la Mawaziri.
Raisi anaweza kuwe na sababu au taarifa ya ubovu wa kiutendaji wa mhusika lakini mahala pakusemea issue kama hizi siyo kwenye majukwaa maana kuja kuproof issue za uwajibikaji ni ngumu sana ,labda ya uwizi.
mke wa Lukuvi yupo pale kabla ya mKULu kuwa mbunge.. ni mdomo mchafu na kujifanya mjuzi wa kila kitu ndio kunaponza kichwa.. tunakoelekea sio kuzuri kabisa
 
Tuliuliza watoto wa viongozi kujazana ndani ya vyama na serikali mkasema hakuna kosa.
Sasa leo mke wa waziri au kiongozi mwingine yeyote kufanya kazi ktk mashirika au taasisi za serikali kuna kosa lipi?
Mama huyo kaonewa kuachwa jobless sababu tu mmewe ni waziri leo. Hivi asipokuea waziri kesho si maafa nyumbani?
Mungu anawaona.
 
Picha yake tafadhali, nataka nimfamahu tu, mama waziri aliyekuwa anakula mshahara wa bure
 
Kama ana sifa zinazohitajika kwa kazi anayofanya/aliyoajiriwa mi naona hakuna shida, maana ana haki ya kufanya kazi sehemu yoyote bila kujali ni mke wa Waziri au sio mke wa Waziri.
Ni kweli akiwa sifa zinazi stahili ni haki yake kufanya kazi lakini ubaya uliofanyika ni hilo shirika kulipa mishahara ya wafanya kazi 300 huku likiwa halifanyi kazi na pia yeye akiwa ndio bosi wa hilo kusababisha hasara kubwa kama ulimsikiliza mh raisi akitaja zile ujanja wote zote walizokua wakitumia hao wafanya kazi.
Kwahiyo yeye ilitakiwa ajiuzulu mapema wakati wengine wakitumbuliwa tena hadharani. Na nahisi mh raisi alikua analikua analijua hili tatizo lakini alukua anammezea na kumuangalia tu sasa ikafika mahali ikabidi amtumbue tu na yeye.
 
Kwani mke wa waziri ni kosa kisheria kuajiliwa?.

Mimi sioni kosa huyo mke wa waziri kuajiliwa ATCL kama ana sifa kwa nini asiajiliwe na nihaki yake kuajiliwa kama raia wa Tanzania.

Pia sio vizuri viongozi wa kubwa serkalini kusimangana kwenye majukwa.

huyu mama kaonewa sana sioni kosa lake.

Pole mama Mungu akupe nguvu kipindi Hiki kigumu,usijali cha muhimu uzima haya mengine yote ni ya kupita tu
 
Anaweza kupokea salary kubwa kuliko hata wateuliwa wa raisi ndio maana she must go!
 
KUNA WATU WASHAKUWEPO HAPO ATCL MPAKA WAKAWA MAMEYA WA JIJI....WALITUMBUAA SANA HELA ZA ATC..
KITAMBO KILE

OVA
kufa kwa atcl ni matumizi mabaya ya rasilimali, kikubwa ni mzunguko wa fedha ndani ya shirika na baina ya wadau wa shirika; hapo kitengo cha fedha hakiruki.

kwa utumishi wa miaka 20+, hata kama aliingia na cheti muda huu ni senior kwenye kitengo hivyo kwa namna moja au nyingine anaufahamu au umepita mikononi mwake uozo wa atcl.

kwa namna hii mkuu kamtumbua mtu kwa busara zaidi, angalau!
 
Back
Top Bottom