Mke wa Lukuvi kung'oka sababu ni nini?

Mke wa Lukuvi kung'oka sababu ni nini?

Kuna style fulani ya kukomoana!Huyu Rais wetu lazima ajaribu ku analize mambo kabla ya kuzunguma mbele ya kadamnasi...
Ova
Yeye mwenyewe alipokukuwa waziri mkewe alikuwa anafundisha oystrerbay basi nae angekuwa mwalimu wa vijijini huko ndio tungeelewa. Haiingii akilini kwamba ilikuwa coincidence yeye kuwa waziri na mkewe kufundisha mjini tena oystrerbay karibu kabisa na nyumbani kwake! Tuache unafiki wa kushabikia mambo bila kuangalia uhalisia
 
1. mama Mahiga
2. mama Lukuvi
3. next....
 
ATCL haiwezi kukosa kashfa ya matumizi mabaya ya pesa.
KUNA WATU WASHAKUWEPO HAPO ATCL MPAKA WAKAWA MAMEYA WA JIJI....WALITUMBUAA SANA HELA ZA ATC..
KITAMBO KILE

OVA
 
Itakuwa amehusika kupiga deal, na kwa sbb n mke wa waziri wakashindwa kumchukulia hatua, ss muheshimiwa naye kashindwa kumuondoa kwa sbb hana ushahidi wakutosha au deal lilifanyika kitambo, so katumia vyombo vya habari ili ajiondoe mwenyewe ATCL mpya ianze kazi bila zengwe
 
Mbona hiyo standard haisemwi kwenye vyama vya siasa? Sasa hivi hata Ma - house girl na waganga wa kienyeji wa familia za vigogo wamejaa kwenye vyama vya siasa. Unakuta baba, mama, mwana, mkwe, shemeji, n.k wote wako kwenye chama. Sioni shida sana ila kama mke wa waziri imekuwa nongwa kuwa mhasibu wa ATCL basi hata huko kwenye vyama tuangaliane.
 
ngoja niwaze kwa sauti...

1, mke wa waziri kila siku asubuhi anaenda kazini huku ofisi haina kazi...
mke wa waziri haende kazini na hakuna wa kumuuliza na mshahara anakuala kama kawa..
mke wa waziri labda kahusika kufilisi shirika hasa ukiangalia muda alio kaaa..
mke wa waziri labda anakaribia kustaafu kaona mmmh naweza asivumiliwe kufika huo muda bora ajiweke pembeni..
mengine kapuni.. nawaza kimya kimya
 
Mbona hiyo standard haisemwi kwenye vyama vya siasa? Sasa hivi hata Ma - house girl na waganga wa kienyeji wa familia za vigogo wamejaa kwenye vyama vya siasa. Unakuta baba, mama, mwana, mkwe, shemeji, n.k wote wako kwenye chama. Sioni shida sana ila kama mke wa waziri imekuwa nongwa kuwa mhasibu wa ATCL basi hata huko kwenye vyama tuangaliane.
nikiangalia nafasi yake ya uhasibu nadhani ameogopa kugusa hapo ingeharibu upande wa pili nahisi imetengenezwa hiii..
 
Kumekuwa Na mjadala Juu ya Mke wa Waziri wa Ardhi Mh.Lukuvu mtumishi wa ATCL.Mjadala huu unahusu huyu mama Kung"oka Utumishi.Je amefanya nini mpaka kuwe Na mjadala? Je hakutakiwa kung"oka au kalazimishwa? Kwa wanaujua watujuze.Kidumu chama cha Mapinduzi.
Huo mjadala uko wapi?
 
Acha ajiuzulu ili mkuu ajue si yeye pekee asie jaribiwa hata wake wa mawaziri wake hawajaribiwi, nafasi iko wazi ampe ambae anaona anastahili kuwepo hapo.
 
Ni Mkewe lukuvi au mkwe? Yaani mke wa Lukuvi kufanya kazi zaidi ya Miaka 25 ATCL ina maana mkewe lukuvi ana miaka zaidi ya 50?
 
Kuna shida! Raisi wa Nchi mbele ya Kadamnasi anatamka kuwa Mkwe wa Waziri! Labda kama ndani ya ATCL kuwa wake zaidi ya wawili wa Mawaziri katika mazingira hayo unaweza kubaki kuona hali ya hewa ikoje. Lakini kama mkwe wa Waziri ni huyo mmoja kwa kweli huko nikudhalilishana na kama ni kwa wenzetu kauli ya Raisi siyo ya kiustaarabu na wala heshima. Ukizingatia mwenye mke ni sehemu ya Baraza la Mawaziri.
Raisi anaweza kuwe na sababu au taarifa ya ubovu wa kiutendaji wa mhusika lakini mahala pakusemea issue kama hizi siyo kwenye majukwaa maana kuja kuproof issue za uwajibikaji ni ngumu sana ,labda ya uwizi.
Tena kwa mshangao aliouonyesha mkulu ni ishara tosha kua hukupendezwa na huyo mama kuwepo pale, hivyo kwa muungwana hutumia medulla oblongata na kupata jawabu nini afanye
 
Nasema awamu hii 5 tuna shida sana, hekima, busara hazina nafasi ni kuropoka mwanzo mwisho
 
Ni Mkewe lukuvi au mkwe? Yaani mke wa Lukuvi kufanya kazi zaidi ya Miaka 25 ATCL ina maana mkewe lukuvi ana miaka zaidi ya 50?
Kwani Lukuvi ni mtoto yule? Kwa kumuangalia tu yuko 60's
 
Back
Top Bottom