Mke wa Kelvin.........

Mke wa Kelvin.........

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
23,265
Reaction score
17,135
Mke wa Kelvin anajivunia mume mtulivu, hashindi baa na hatongozi
videmu. Akitoka kazini huenda kucheza basketball na hurudi nyakati za
dinner. Siku moja mkewe akamhurumia. Anachoka na kazi. Mtu gani
asiyependa starehe japo kidogo? Mke akamlazimisha outing, Kelvin
akabisha lakini taxi ikafika. Gonga Club & Lodge.

Walipofika mlangoni tu, mlinzi akaita, Mambo Kelvin! Poa
Nilidhani huwa huji club, inakuwaje mlinzi anakufahamu? mke akauliza
Yule mgambo, mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time
hapa akajibu Kelvin.

Wakachagua meza. Kukaa tu tayari mhudumu ameshaleta castle lager.
Akamuuliza mama anakunywa nini. Mhudumu alipoondoka mama akauliza,
amejuaje unakunywa castle kama hakufahamu?

Wakati Kelvin anajikanyaga aanze vipi kujitetea, mhudumu wa vyumba
akawa amefika na kuuliza.
Mkuu kama kawaida nimekuandalia namba tano, nendeni tu vinywaji
nitawaletea huko huko

Kufikia hapo mama akawa hana simile tena, akanyanyuka akitukana kama
chizi. Akatoka nje mbio na kuingia katika taxi iliyokuwepo pale.
Wakati anapatana bei na dereva, Kelvin naye akaingia. Mama
yakamporomoka matusi kibao na kilio juu. Alipovuta kamasi na kupiga
kwikwi akamsikia dereve anasema.

Duh, eee bwana Kelvin huyu malaya uliyeokota leo balaaaaaaaaaaaaaaa!

Mamaa akazimiaaaazzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
 
Duh mkuu ume-edit jina la msela nini ,hii kitu iliwekwa tayari,ikarudiwa mara ya pili kwa jina la frank ,weye umekuja na lako eti kelvin,lol its copy and paste ,anyways ngoja nicheke teh teh teh teh teh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom