Kuna kitu kikubwa cha kujifunza kupitia hii

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,988
Mke wa Petro anajivunia mume wake ni mtulivu sana hashindi baa na hatongozi videmu. Akitoka kazini tuu ndani. Siku moja mkewe akamhurumia. Anachoka na kazi. Mtu gani asiyependa starehe japo kidogo? Mke akamlazimisha outing, Petro akabisha lakini taxi ikafika wakaenda Club

Walipofika mlangoni tu, mlinzi akaita, “Mambo" Petro, “Poa”

“Nilidhani huwa huji club, inakuwaje mlinzi anakufahamu?” mke akauliza

“Yule mgambo, mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time hapa” akajibu Petro

Wakachagua meza. Kukaa tu tayari mhudumu ameshaleta castle lager. Akamuuliza mama anakunywa nini. Mhudumu alipoondoka mama akauliza, “amejuaje unakunywa castle kama hakufahamu?”

Wakati Petro anajikanyaga aanze vipi kujitetea, mhudumu wa vyumba akawa amefika na kuuliza.

“Mkuu kama kawaida nimekuandalia namba tano, nendeni tu vinywaji nitawaletea huko huko”

Kufikia hapo mama akawa hana simile tena, akanyanyuka akitukana kama chizi. Akatoka nje mbio na kuingia katika taxi iliyokuwepo pale. Wakati anapatana bei na dereva, Petro naye akaingia. Mama yakamporomoka matusi kibao na kilio juu. Alipovuta kamasi na kupiga kwikwi akamsikia dereve anasema.

“Duh,huyu malaya uliyeokota leo ni zaidi ya balaaaaa wote unaowachukuaga!”

Mama akazimia

Hivi kama we ndio huyu Petro utafanya nini?
Na kama we ni ndio huyu mama utafanya nini?
 
Nimeandika nikafuta nikaandika tena nikafuta
 
Ningekuwa mi ndo Petro si ningekana mara tatu kesi kwisha.. uliza jengine mkuu...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sawa bwana KENZY jeuri kwenye maandishi.........

vipi ile manzi bado unaionea aibu mkuu?
 
🙄🙄 Mkuu manzi gani Tena..??
 
Mke wa Petro anajivunia mume wake ni mtulivu sana hashindi baa na hatongozi videmu. Akitoka kazini tuu ndani. Siku moja mkewe akamhurumia. Anachoka na kazi. Mtu gani asiyependa starehe japo kidogo? Mke akamlazimisha outing, Petro akabisha lakini taxi ikafika wakaenda Club

Walipofika mlangoni tu, mlinzi akaita, “Mambo" Petro, “Poa”

“Nilidhani huwa huji club, inakuwaje mlinzi anakufahamu?” mke akauliza

“Yule mgambo, mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time hapa” akajibu Petro

Wakachagua meza. Kukaa tu tayari mhudumu ameshaleta castle lager. Akamuuliza mama anakunywa nini. Mhudumu alipoondoka mama akauliza, “amejuaje unakunywa castle kama hakufahamu?”

Wakati Petro anajikanyaga aanze vipi kujitetea, mhudumu wa vyumba akawa amefika na kuuliza.

“Mkuu kama kawaida nimekuandalia namba tano, nendeni tu vinywaji nitawaletea huko huko”

Kufikia hapo mama akawa hana simile tena, akanyanyuka akitukana kama chizi. Akatoka nje mbio na kuingia katika taxi iliyokuwepo pale. Wakati anapatana bei na dereva, Petro naye akaingia. Mama yakamporomoka matusi kibao na kilio juu. Alipovuta kamasi na kupiga kwikwi akamsikia dereve anasema.

“Duh,huyu malaya uliyeokota leo ni zaidi ya balaaaaa wote unaowachukuaga!”

Mama akazimia

Hivi kama we ndio huyu Petro utafanya nini?
Na kama we ni ndio huyu mama utafanya nini?
Petro kawa petrol
 
Back
Top Bottom