Sheria ya Mungu
Sheria za Mungu ni pamoja na amri kumi. Imeandikwa, Kutoka 20:1-17 "Mungu akanena maneno haya yote akisema.[1] Mimi ni Bwana Mungu wako niliye kutoa katika nchi ya misiri katika nyumba ya utumwa usiwe na miungu mingine ila mimi.[2] Usijifanyie sanamu ya kuchonga wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni wala kilicho chini duniani wala kilicho majini chini ya dunia usivisujudie wa kuvitumikia kwa kua mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu wenye wivu nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu.[3] Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, maana Bwana hatamuhesabia kuwa hana hataia mtu alitajaye jina lake bure. [4] Ukumbuke siku ya sabato uitakase siku sita fanya kazi utende mambo yako yote; lakini siku ya sabato ni ni ya Bwana, Mungu wako siku hiyo usifanye kazi yo yote wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. maana kwa siku sita Bwana Mungu alifanya mbingu na nchi na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibaria siku ya sabatu akaitakasa.[5] Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.[6] Usiue.[7] Usizini.[8] Usiibe.[9] Usimshuhudie jirani yako uongo.[10]Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wajirani yako, wala mtumwa wake, wala mjalkazi wake, wala ng'ombe wake wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako."