Kaka yetu anasaidia ndugu wa mke wake, sisi hatusaidii

mpwayungu village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
9,866
16,341
Katika maisha kosea vyote ila sio kuoa. Huyu kaka etu ana roho ya uchuro yani sisi wadogo zake tumbo moja tukiwa na shida ya kifedha jibu lake atasema Sina pesa ukibahatika sana basi utapewa nusu tu au unapewa kwa masimango lakini ndugu zake mke wake anawajali anacheka nao kila shida anawasaidia.

Mama mkubwa ametuambia karogwa na mke wake sisi kama ndugu tutafute mganga tumnasue maana huenda kapewa rimbwata. Huwezi sahau nyumbani kwenu ukawa unatunza watu ambao sio nduguzo, kwanini Hao watoto wasipewe hela na ndugu zao huko halafu waje kwa kaka etu kuwa ombaomba, kila nikienda kumsalimia broo nawakuta wapo, kila rikizo za shule na vyuo wakifunga wanaenda kwa broo.

Halafu utasikia shemeji shemeji, shemeji ya minyoko. Kuna siku miaka mitatu nyuma nilikwazika kweli, niliomba pesa ya ada akasema hawezi nipa mkononi akaenda benki akalipia, ila ndugu wa mke wake akitaka pesa ya Ada anampa cash in hand ila mimi haniamini. Binafsi nimeacha hata kwenda kumsalimia ila ipo siku atanikumbuka tu
 
TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
4,215
12,171
Katika maisha kosea vyote ila sio kuoa. Huyu kaka etu ana roho ya uchuro yani sisi wadogo zake tumbo moja tukiwa na shida ya kifedha jibu lake atasema Sina pesa ukibahatika sana basi utapewa nusu tu au unapewa kwa masimango lakini ndugu zake mke wake anawajali anacheka nao kila shida anawasaidia.
Umesahau kutuambia kwamba wewe ni kijana mdogo wa miaka 37.
 
Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
72,279
145,611
Katika maisha kosea vyote ila sio kuoa. Huyu kaka etu ana roho ya uchuro yani sisi wadogo zake tumbo moja tukiwa na shida ya kifedha jibu lake atasema Sina pesa ukibahatika sana basi utapewa nusu tu au unapewa kwa masimango lakini ndugu zake mke wake anawajali anacheka nao kila shida anawasaidia.

Mama mkubwa ametuambia karogwa na mke wake sisi kama ndugu tutafute mganga tumnasue maana huenda kapewa rimbwata. Huwezi sahau nyumbani kwenu ukawa unatunza watu ambao sio nduguzo, kwanini Hao watoto wasipewe hela na ndugu zao huko halafu waje kwa kaka etu kuwa ombaomba, kila nikienda kumsalimia broo nawakuta wapo, kila rikizo za shule na vyuo wakifunga wanaenda kwa broo.

Halafu utasikia shemeji shemeji, shemeji ya minyoko. Kuna siku miaka mitatu nyuma nilikwazika kweli, niliomba pesa ya ada akasema hawezi nipa mkononi akaenda benki akalipia, ila ndugu wa mke wake akitaka pesa ya Ada anampa cash in hand ila mimi haniamini. Binafsi nimeacha hata kwenda kumsalimia ila ipo siku atanikumbuka tu
Limbwata zinatufelisha sana aisee
 
Kaka pembe

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
2,355
3,675
Tafuta pesa zako uzipangie matumizi.

Ndugu mna laana sana kulilia pesa za kaka/dada zenu.

Huko ndiko anakothaminiwa na kuheshimiwa ninyi inaonesha hamnaga msaada zaidi ya kulakamika.

Ukiona vipi aachane na mkewe wewe uchukue nafasi ya mke na mpe kila apewacho na mke🤣🤣🤣🤣
Akioa atajua. Jibu Safi na alifanyie kazi. Yawezekana alikua anasubiria mchongo wa sensa halafu walimu wakapindua meza so imebidi lawama ziende kwa kaka.
 
jokotinda_Jr

JF-Expert Member
Apr 9, 2022
669
1,040
Mimi binafsi maisha ya kuomba pesa kwa ndugu kwa namna yeyote nilisha jipiga marufuku .... tafta pesa zako kwa jasho lako

1: Kwanza utaheshimika nyumbani
2:Utakuwa na uhuru nazo
3: Utaepuka dharau zisizo na msingi

Nakusisitiza wewe na nduguzako wengine tafteni pesa zenu kwa jasho lenu omba omba huleta unyonge hasa kwa watoto wakiume ..... umenielewa meku???
 
14 Reactions
Reply
Top Bottom