Mke wa Gwajima aibua hofu afya ya mumewe

Mke wa Gwajima aibua hofu afya ya mumewe

Jibu ni rahisi mimi sio askofu mkuu kama Gwajima na situkani Pengo sababu namjua si wa kutukana yule ni kisiki cha mpingo.Shukuru tu leo nimeamka vizuri nigekporomoshea matusi ya nguoni hadi nipigwe ban.

Labda kama wewe ni mzee tena kikongwe au computer system umetegeshwa uvulege mijadara ya wenzio hapo sawa,ila kama ni kijana tena bado unandoto za kuwa kama walee walio ktangulia nakuhakikishia kwa majisifu hayo hautopgwa bana na jf-pekee ban litaktafna kila utakapo na kila uingiapo.
 

​
Gwajima-30march2015.jpg

​

Familia ya Kiongozi wa Kanisa la Ufunuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, imeeleza hofu yake kwamba imeshangwazwa na hali ya afya ya kiongozi huyo kubadilika ghafla akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi akihojiwa.Akizungumza na waandishi wa habari jana, katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam, mke wa Askofu Gwajima, Grace Gwajima, alisema familia bado haielewi ni kwa namna gani Askofu huyo alizimia ghafla wakati aliondoka nyumbani akiwa mzima wa afya.

Alisema kama familia kuna vitu vinavyowachanganya na hawapati majibu haraka ikiwamo la Askofu Gwajima kuondoka nyumbani akiwa mzima wa afya huku akitembea, lakini muda mfupi baadaye anapelekwa hospitali akiwa amezimia akihojiwa na polisi.

“Tunahisi kuna kitu amefanyiwa, kwa maana haiwezekani mtu aondoke nyumbani akiwa wa afya, lakini baadaye kidogo tunapewa taarifa amezimia yupo TMJ, hapa kutakuwa na kitu,” alisema Grace akiwa na mmoja walinzi wa Askofu Gwajima.

HALI YA ASKOFU GWAJIMA
Akizungumzia hali ya Askofu Gwajima, aliyelazwa hospitalini hapo kwa siku tatu, Grace alisema mumewe anaendelea vizuri na madaktari walikuwa wanajiandaa kumtoa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) jana na kumpeleka wodi ya wagonjwa wa kawaida.

Alisema kwa sasa Askofu Gwajima anaweza kuongea, kula chakula na hata kuzungumza na watu mbalimbali wanaofika kumjulia hali. “Kuna improvement zimeaza kujitokeza, ki ukweli kuna hali ya uzima na anaendelea vizuri,” alisema Grace.

Hata hivyo, waandishi wa habari walizuiwa na uongozi wa Hospitali ya TMJ kwenda kumwona Askofu Gwajima na badala yake walimwita Grace azungumze na waandishi.

KUKAMATWA KWA WACHUNGAJI
Mke wa Askofu Gwajima (Grace), alidai kuwa juzi usiku Polisi walifika hospitalini hapo na kuwakamata wachungaji 30 waliofika kumjulia hali Askofu Gwajima.

Alidai kuwa Polisi waliwakamata wachungaji hao pamoja na magari yao na kuwapeleka kusikojulikana.

“Jana usiku kulizuka tafrani hapa hospitalini, Polisi walifika na kuwakamata wachungaji wapatao 30 wa Kanisa la Ufufuo na Uzima na kuondoka nao,” alidai Grace.

Hata hivyo, NIPASHE lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuthibitisha taarifa hizo, lakini alisema angetuma taarifa hiyo kwa vyombo vya habari. Hata hivyo, hadi tunakwenda mitamboni Kova hakutuma taarifa hiyo.

ULINZI WAIMARISHWA HOSPITALINI
Hali ya ulinzi katika Hospitali ya TMJ iliimarishwa ndani na nje ya eneo hilo, kwa kuwapo kwa askari waliovalia nguo za kiraia.

Askari hao walionekana wakiimarisha doria nje ya wodi aliyolazwa Askofu huyo na kuzuia watu kusogelea wodi hiyo.

Nje ya hospitali hiyo kulikuwapo na gari la Polisi lililokuwa limeegeshwa likiwa na askari waliovalia nguo za kiraia, huku wengine wakiingia ndani na kutoka kila mara.

Mbali na askari hao, pia walinzi wa Askofu Gwajima nao walionekana wakiwa karibu na wodi hiyo.

Ijumaa iliyopita, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilimhoji Askofu Gwajima kwa tuhuma za kumkashifu na kumtukana hadharani Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Policarp Kardinali Pengo.

Muda mfupi wakati wa mahojiano hayo yakiendelea, Askofu Gwajima alizimia ghafla akiwa kwenye chumba cha mahojiano katika Kituo cha Polisi Kati.

Kufuatia hali hiyo, Askofu huyo alipelekwa katika hospitali tofauti ikiwamo ikiwamo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na mwishowe kupelekwa TMJ.

CHANZO: Nipashe

​
Pole mama! Jitie nguvu mungu bado ni mwema!
 
mbona mmewe analivyofumwa na frola mke wa mtu hakusema chochote??
 
Huyo mke wa Gwajima anatia huruma.Hata ukimwona kwa kweli kajikatia tamaa.Jitu likiwa zima kazi kutukana watu kwenye majukwaa kanisani na kutembea na viruka njia akina Flora Mbasha.Likiumwa mke ndie anatupiwa zigo la kuliuguza na kulitolea maelezo linaendeleaje.
Pole mke wa Gwajima.Pokea pole toka moyoni mwangu kabisa.

Una laana wewe siyo bure
 
Uliona Gwajima alivyokuwa akishangiliwa na waumini wake wakati akiporomosha matusi akimporomoshea Pengo? Kama hujaona basi si tatizo nenda mkutano wowote wa CHADEMA uone matusi kwa serikali yanavyoporomoshwa na wanywa viroba wafuasi wa CHADEMA wanavyoshangilia.


Nilijua tu kwa mavi haya utakuwa Ni ccm
 
Huyu Baba mtu mzima lakini sijui kwa nini hajiheshimu,nimesikia yale mazungumzo anayo mchamba Pengo,utadhani mtunzi wa Taarab na anaongea bila aibu wala wasiwasi na anasahau kua yeye ni binadamu kama wengine,au sijui ndio umaarufu...

Kama pengo hajiheshimu unataka aheshimiwe na nani.

Viongozi wa wakristo wamekubaliana jambo, wamelitolea tamko pengo anakujaje kinyume nao??

Kadhi anakuja kuisilimisha Tz, umoja wa wakristo Tz unatakiwa zaidi saa hizi kuliko wakati mwingine wowote.

Mikurupuko ya pengo ni hatari kwa afya ya UKRISTO kuliko maneno makali ya Gwajima.
 
Gwajima akitoka hapo hospitali Polisi waendelee kumuhoji ikiwezekana wamtandike kidogo ili aseme ukweli huwa ni nani anamtuma kutukana viongozi wa dini.[/QUOTE

Kitendo cha askari wengi kuwepo hospitali inamaanisha nini? KAma huyo Gwajima alienda peke yake Polisi kutoa maelezo yake na katikati ya maelezo akaugua inamaana Gwajima ni Mhalifu!
 
Kama anaongea anasubiri nini kusema walimfanya nini?.
inavyoelekea jamaa ali act ndo maana hata vipimo havijaona tatizo.
uzuri polisi nao bado wanae tu mpaka atasema tu

Huyu waswahili wanasema unakula ngadu kwa ngadu mpaka aseme chanzo cha utajiri wake.
 
Kama pengo hajiheshimu unataka aheshimiwe na nani.

Viongozi wa wakristo wamekubaliana jambo, wamelitolea tamko pengo anakujaje kinyume nao??

Kadhi anakuja kuisilimisha Tz, umoja wa wakristo Tz unatakiwa zaidi saa hizi kuliko wakati mwingine wowote.

Mikurupuko ya pengo ni hatari kwa afya ya UKRISTO kuliko maneno makali ya Gwajima.

Kenya kuna kadhi imesilimishwa?
 
If your strength is weak,don't carry heavy burdens.

Acha mchuma janga ale na wa kwao.
 
Gwajima alipigwa maswali kuhusiana na biashara ya UNGA hicho ndio kilizidi kumpa kihoro...ndio alitanabahi kumbe polisi wanajua mengi kuhusiana na biashara yake so kadata ganja..ila yule wanae tu ngoja apate nafuuu waendelee nae
 
Huyo mke wa Gwajima anatia huruma.Hata ukimwona kwa kweli kajikatia tamaa.Jitu likiwa zima kazi kutukana watu kwenye majukwaa kanisani na kutembea na viruka njia akina Flora Mbasha.Likiumwa mke ndie anatupiwa zigo la kuliuguza na kulitolea maelezo linaendeleaje.
Pole mke wa Gwajima.Pokea pole toka moyoni mwangu kabisa.

Je ulinzi wote na nguvu yote inayotumika, tatizo ni kumkashifu Pengo? Mimi nadhani hapa kuna jambo ambalo wanaolijua ni Pengo na CCM
 
Je ulinzi wote na nguvu yote inayotumika, tatizo ni kumkashifu Pengo? Mimi nadhani hapa kuna jambo ambalo wanaolijua ni Pengo na CCM

Kamwuulize Gwajima kilichofanya presha ipande.Kaonyweshwa ukurasa mmoja tu wa yaliyomo kwenye faili lake lililoko kwenye vyombo vya usalama na polisi kapanda presha. Kwani akicheki faili lake anakuta lina kurasa kibao na ukurasa huo mmoja tu anasikia kufa.Kwa nini asipande presha hapo.Alikuwa hajui kama kuna faili lake.

Sasa hivi nasikia ukimwekea tu kale kavideo kanakoongelea yeye akitukana pengo akisikia tu anazimia sijui kwa nini.Anayebisha akienda kumwona hospitali aweke ile sehemu ya kumtukana pengo kama mlio wa simu ili ikiita itoe ile sauti ya Gwajima akimtukana pengo utaona Gwajima anazimia hapo hapo.Hana hamu na sauti yake mwenyewe.
 
Wale malaika aliotaka wamshughulikie askofu Pengo wanashughulika naye sasa.

Imeandikwa "usihukumu usije ukahukumiwa"

Namtakia afya njema ili apate nafasi nyingine ya kutubu makosa yake.
 
Natoa pole nyingi kwa watu wote waliothirika na sakata la baba askofu Gwajima na sirikali mpaka sasa.Mungu wa Amani awatie nguvu mpya kama Simba wa Yuda na kuwafariji wote bila kusahau familia na kanisa lote la Mungu wa Kweli na Uzima. Tuseme "AMEN".
 
Gwajima alipigwa maswali kuhusiana na biashara ya UNGA hicho ndio kilizidi kumpa kihoro...ndio alitanabahi kumbe polisi wanajua mengi kuhusiana na biashara yake so kadata ganja..ila yule wanae tu ngoja apate nafuuu waendelee nae

Inawezekana akawa anafanya biashara ya unga kama unavyodai,na polisi wanajua kama unavyodai ila ninakushangaa unavyowaunga mkono polisi.kama wanajua ni kwanini hawajamkamata kwa tuhuma hizo? Kwanini wamkamate baada ya kwenda mwenyewe kuhojiwa kuhusu tamko lake kwa Pengo ndio wamuulize maswali yahusuyo unga kama unavyodai hao walinzi waliokamatwa kwa tuhuma za kutaka kumtorosha kwani si alikwenda mwenyewe baada ya kushindwa kumpata?sasa anatoroshwaje?
 
Wale malaika aliotaka wamshughulikie askofu Pengo wanashughulika naye sasa.

Imeandikwa "usihukumu usije ukahukumiwa"

Namtakia afya njema ili apate nafasi nyingine ya kutubu makosa yake.

Malaika(Majini) (Gwajima hatumii malaika anatumia majini) aliowatuma wakampige Pengo wamemgeuka Gwajima na kuanza kumbonda.Kuna mahali niliandika Gwajima ni mtoto mdogo mno kwa Pengo na niliandika amwombe msamaha yule mzee haraka iwezekanavyo hakusikia.Hata sasa akipata unafuu tu aitishe press conference haraka aombe msamaha bila kumumunya maneno wala kuongea lugha ya mafumbo itamsaidia.Ila akiendelea kushupaa mimi simo.
 
Back
Top Bottom