Mke Wa Dr. Salaa Josephine Alonga Na JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke Wa Dr. Salaa Josephine Alonga Na JF

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Superman, Sep 5, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/72378-mhariri-joseph-kulangwa-habari-leo-sasa-ni-zamu-yako.html

  Ndugu wana JF,

  Nimekuwa nikisoma nakufatilia trend zote zilizokuwa zinanihusu,naomba kuwashukuru wote mlioweza kutoa maoni ambayo yamewajenga wengi wanaopitia mtandao huu,leo nimeamua kuvunja ukimya na kujiunga na wana JF ili inapotakika basi mniulize mwenyewe kuliko kusikiliza watu wachache wenye ajenda zao binafsi.Mimi ndiye Josephine Mushumbusi.Sijawahi kuongea au kuulizwa chochote juu ya maisha yangu binafsi vyombo hivi nya habari vimekuwa vikiandika mengi juu yangu leo,sitashangaa sana kwakuwa hilo ni lengo lao.

  Ndugu wanaJF,kwa wanaojua maisha ya ndoa,watakubaliana na mimi ndoa ni ya watu wawili ndoa haielezewi mahali pa wazi,ndoa ni ndani ya chumba chenu,watu wengi wamehukumu hasa wanapotazama maadili ya ndoa za kikristo,

  mimi ni mkristu na nimejifunza Biblia vizuri,Lakini ni biblia hiyohiyo imetoa ruhusa kuwa ndoa inaweza kuvunjika kwa sababu ya msingi sana.

  napenda niwaeleze,mtasoma mambo mengi,mimi ninao moyo mkuu kwakuwa najua nijinsi gani mtu anavyoweza kutumiwa,sikutengana na Mahimbo leo wala mwaka jana,nasikuanza kuishi na Dk leo.

  Naomba tu mjiulize katika utaratibu wa kawaida Ndugu tunao,wachungaji tunao mbona wao wako kimya?naelewa na ninajua vitisho vyote alivyopewa mahimbo na kutengeneza habari hizi zote,Ndugu zangu tusipende kutengenezeana shutuma kwani tunajichumia dhambi za bure,
  USILOLIJUA NIKAMA USIKU WA GIZA

  Nilikuwa na Uhuru kumpenda mtu aliyenipa amani na faraja.Na sikuwanasababu ya kujifunga katika shimo lisilokuwa na matumaini hati kwasababu ya ahadi au kiapo.Ni watu wangapi wamepoteza maisha sababu ya kuishi ndani ya viapo visivyo na matumaini?

  Nitasonga mbele na Kumuangalia Mungu kama Hakimu wa kweli,sitaogopa Mtu yeyeto kutoa maoni yake binafsi juu ya maisha yetu kwani hatukuyaanza leo.

  Wahariri nivema mkatumia utaalamu wenu na si kutumika kama mnavyotumiwa sasa,Nililijua hili mapema sitarudi nyuma daima tutasonga mbele.

  NA MUNGU ATAFUNGUA NJIA NITAMTUNZA MUME WANGU MPYA ILI UMAKINI NA HEKIMA ZAKE ZILETE UKOMBOZI KWA WATANZANIA WOTE.NITASIMAMA KATIKA ZAMU YANGU KAMA MKE MWEMA NA HAKUNA LITAKALOHARIBIKA,KWANI NINAYAWEZA YOTE KWAKE YEYE ANAYENITIA NGUVU.Efeso 4:13

  Najua jambo moja tu,mipango ya Mungu si kama mipango ya wanadamu.na ndiyomaana ametupa ujasiri wa kujiweka wazi bila kuogopa shutuma zozote.
   
 2. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mama Josephine;

  Heshima mbele sana.

  Kwanza kwa niaba ya wana JF wote naomba nikukaribishe rasmi katika jukwaa letu.

  Ni katika jukwaa hili uozo wote unaanikwa na kulazimisha watawala wachukue hatua. maisha binafsi ni haki yako na haina mwingiliano na siasa. Bill Clinton alitenda ufuska ikulu na mwenyewe akakubali alitenda lakini wamarekani bado wakampa kura kipindi kingine, kwa kuwa kazi yake waliiona.

  Wengi wamekutetea sana humu na wengi wanakuamini.

  Jipe moyo na matumaini, tutamshinda ibilisi.

  Na sasa tunamkoma nyani usoni mchana kweupe.

  Karibu JF.
   
 3. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Wou! wou! wou! Josephine, Big up.
  Tena nakushauri sana, usiseme lolote baya juu ya Mahimbo. Mheshimu na kumtunza Mahimbo. Mwache yeye atumiwe na CCM na mwisho wa siku watamtupa kama Toilet paper. Kama hajui namna ya kutumiwa amtafute Angelina aliyekuwa mke wa Lyatonga Mrema (Kama bado yuko hai). Ndoa ni makubaliano ya wawili wenye mapenzi. Mapenzi yakiisha, yanabaki mazoea tu.

  Na kwa kuwa umefungua pazia, tunawataka sasa nyumba ndogo zote za Kikwete zije JF na kujieleza. Josephine si nyumba ndogo ni mchumba na ametambulishwa mbele ya majukwaa. Tunamtaka Salma aje hapa atueleze kwa nini anamchukia Shy...., Chi....., n.k
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh teh! Ahsante Josephine! songa mbele mama! hakuna kurudi nyumba. Mtunze Mr President ili watanzania waweze kukombolewa, naimani unampa ushauri nasaha kabisa na unastaili kuwa First lady wetu.
   
 5. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Asante sana Baija Bolobi,

  Kwa nini usipeleke facts zako kwa hii in blue kule kwenye thread ya: KIKWETE: In Black And White?
   
 6. P

  Paul S.S Verified User

  #6
  Sep 5, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kwa ama hakika kama kweli wewe ndiye basi umechagua jukwaa sahihi litakalo kupa kila aina ya sapoti, na yeyote atakaye kuhoji atasakamwa kama nyuki
  mimi naomba kama upo tayari tukuulize maswli ywtu utuweke sawa ambao hatujui vizuri hii issue nzima ukizingatia wewe ndio muhusika mkuu
   
 7. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  =======

  Nipe hiyo thread Superman
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Baija Bolobi ungemalizia Shy..............na Chi............ungekata mzizi wa fitina.

  Lakini nampongeza sana Josephine nampa moyo ajue katika kuirudisha nchi hii mikononi mwa wananchi tunapambana na mapapa na manyangumi ambayo hayatakubali kirahisi kuiachia. Kwa hiyo yatafanya kila mbinu chafu kuchafua kinachoonekana kutuletea mwanga.

  Josephine ajipe moyo na ajiaandae kwa makubwa zaidi, naomba ajifunze kwa Hillary Clinton alivyo ushinda moyo hadi sasa ni mtu wa kuaminiwa na wamarekani. CCM hawajaanza leo mchezo huo waliufanya hata kwa Mrema na Angelina tuliona na sasa wanajaribu tena. Lakini Mungu ni mkuu ashinda yote watajaribu kila mbinu hatimaye siku moja shetani atashindwa.
   
 9. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  aluta continua
   
 10. Josephine

  Josephine Verified User

  #10
  Sep 5, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Karibu,Na ndiyomaana nimejiweka wazi.nimejifunza mengi kwa kuwa huru na muwazi,Sipendi kuwa mtumwa wa maisha yangu mwenyewe.Mimi ni mke wa kiongozi na si kiongozi kama sitakuwa huru sitaweza kumtia moyo mwenzangu.Naelewa mengi yanakuja maisha yangu hayatakuwa siri tena.
   
 11. P

  Paul S.S Verified User

  #11
  Sep 5, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kwa JOSEPHINE
  Nimatumaini yangu wewe uliye post kwa jia la Josephine bado upo online,
  Kama kweli wewe ndio Josephine naomba sana tumia nafasi hii kutoa ufafanuzi wa jambo hili na mumeo, maswali mengi watu wanajiuluza hayana majibu, na kukaa kwenu kimya au kutoa tamko kama ulilolitoa halikidhi hata kidogo, hebu uelezee uma upime ukweli na uongo
   
 12. TinyMonster

  TinyMonster JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Sio Shy na Chi tu. Kuna Betty,Nyamubi,Simba....
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Josephine nakuona hapo chini upo humu karibu kwenye jukwaa,

  Ushauri wangu, kwenye jukwaa hili kuna watakao kutia moyo kuna watakao kuvunja moyo kwa hiyo tegemea yote hayo mawili. Jaribu sana kuchunga utakacho ongea(post) maana kitakaa humu siku zote kama siyo milele na watu watakuwa wanakitumia kama reference na huwezi kukwepa.

  Nimeipenda sana post yako ya kwanza iko very clear plain na haikuingilia personality ya mtu. Jifunze kwa wanaJF viongozi wenzako kama Zitto, Mkumbo, JJ Mnyika na wengine, kama huna cha kuchangia soma tu post za wengine. Ni mawazo yangu binafsi.

  There are currently 30 users browsing this thread. (9 members and 21 guests)
   
 14. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Acha uwongo wako na huyo Mungu wako. Ungekuwa kweli unataka faraja ya moyo usingethubutu kwenda Dodoma Kinyemera kumfuata Slaa huku ukiaga familia yako kuwa unaenda kikazi!. Wala usingewaacha wanao nyumbani na kwenda kujirusha na Slaa kule Mtongani na baadaye kurudi kwa mmeo. Umetenda dhambi kubwa sana. NInachojua mimi na huko nako ulikoenda faraja itakuishia muda si mrefu utaitafuta pengine. Shauri yako na kesha ukiomba.
   
 15. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #15
  Sep 5, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tunashukuru sana kwa ku set record straight nadhani nakala ya hii testmony wanapaswa kupatiwa vyombo vya habari vya kifisadi kama Habari leo na vinginevyo ili wajue kuwa wanachokifanya ni uhuni uliopindukia na wanapaswa kupuzwa kwani lengo lao la kufanya character assasination ni kututoa kwenye mijadala muhimu inayowahusu watanzania wote na yenye maslahi ya Taifa,

  Hii ni moja ya mbinu ya kutaka kunyamazisha sauti ya ukombozi na mjadala mzima wa ufisadi, sasa tunasema Gloves are off tunaomba Dr. aanze kutumia Surrogates kulipua mizinga iliyobaki ili watu wayakimbie majukwaa ya siasa kwa jinsi watakavyo kuwa uuchi, na DR. EELEKEZE MASHAMBULIZI KWA JK kuanisha weakness zake kama kiongozi kwani taifa hili halijawahi kuwa na kiongozi weak kama JK kwa kuwa yupo kwenye DEEP POCKETS ZA MAFISADI.

  Pole sana kwa yote but kuwa na moyo mkuu na ndio kwanza mapambano yameanza! na zaidi ya yote mwombe sana mwenyezi mungu akupe ujasili na ushujaa kuweza kusonga mbele, mimi mwenyewe binafsi nitakutilia DUA.
   
 16. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #16
  Sep 5, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Maaaama Mama Mamaaaaaaa,Mama huyoooo Mamaaaaa Mama huyooo Mamaaaa Mama huyooo Mama Li Mamaa hiloooooh!!!
  Mama Josephine,pole kwa kwa yote unayo ya face,maisha ni maamuzi,hakuna mtu yeyote wa kuhoji kile amabacho wewe unaamua...
  Ombi langu moja kwako Mama,kuwa Makini sana,CCM watakufuata (Kama hawajaanza bado) kuku rubuni um let down Dr Slaa..siamin kama utakubaliana nao kwa hilo,watatumia kila hila kukushawishi,tafadhali Mama,ushauri wangu na angalizo langu litilie mkazo.
  Otherwise,karibu Mama,cha kwanza ukiwa first lady tu tushtakie mafisadi wooote wa WAMA wakiongozwa na yule anayetumia Fedha za misaada ya kina Mama kwa maslahi binafsi na mumewe
   
 17. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #17
  Sep 5, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Bwana Kanyafu Nkanwa, Private matters are off Limit in politics, hakuna familia au mtu asiyekuwa na matatizo kwenye ndoa yake that is fact number one, pili usije kukuta wewe ndo worse zaidi kuliko Josephine, Kwani suala la uaminifu kwenye ndoa ni matatizo ambayo asilimia kubwa ya watanzania wanayo, Tatu ur not so sure with all facts kuwa what real transpared kumfanya amwache huyo bwana! hivyo kuna mengi yanasemwa lakini suala la msingi kwa nini yasemwe sasa? lengo la hao wanaoeneza mambo ya ndani ya mtu binafsi ambayo hayana TIJA kwa watanzania, ni nini lengo, kupotosha masuala ya msingi au kum disqualify Dr Slaa? kama ni hivyo hakuna raisi yeyote aliyepita na aliyepo madarakani ambao hawana scandal za kuwa na mahusiano ya kimapenza na watu ambao sio wake zao? acha kumhukumu binadamu mwenzako kwani nawe utahukumiwa! hii issue ni upuuzi mtupu kufatilia maisha binafsi ya mtu! Tukianza kushabikia mambo haya viongozi wote wachafuka vibaya sana! hivyo tujikite kujadili mstakabali wa nchi yetu sio mambo ya josephine as a person and her weakness
  Yesu aliwaambia wale makuhani na watu mbalimbali waliyemletea yule mama aliyezini kuwa sheria inasema apigwe mawe mpaka mauti impate, lakini bwana YESU hakuhukumu alicho waambiia ambaye anajiona kuwa yeye hana hatia awe wa kwanza kuinua jiwe na kumpiga lakini baada ya mda mchache kila aliyekuwepo alijipeleza na kugundua hata yeye ana hatia mbele za mungu! Tujipeleleze kabla ya kuhukumu wengine na tuuache unafki,
   
 18. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #18
  Sep 5, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Bwana pauls, Private matters are off Limit in politics, hakuna familia au mtu asiyekuwa na matatizo kwenye ndoa yake that is fact number one, pili usije kukuta wewe ndo worse zaidi kuliko Josephine, Kwani suala la uaminifu kwenye ndoa ni matatizo ambayo asilimia kubwa ya watanzania wanayo, Tatu ur not so sure with all facts kuwa what real transpared kumfanya amwache huyo bwana! hivyo kuna mengi yanasemwa lakini suala la msingi kwa nini yasemwe sasa? lengo la hao wanaoeneza mambo ya ndani ya mtu binafsi ambayo hayana TIJA kwa watanzania, ni nini lengo, kupotosha masuala ya msingi au kum disqualify Dr Slaa? kama ni hivyo hakuna raisi yeyote aliyepita na aliyepo madarakani ambao hawana scandal za kuwa na mahusiano ya kimapenza na watu ambao sio wake zao? acha kumhukumu binadamu mwenzako kwani nawe utahukumiwa! hii issue ni upuuzi mtupu kufatilia maisha binafsi ya mtu! Tukianza kushabikia mambo haya viongozi wote wachafuka vibaya sana! hivyo tujikite kujadili mstakabali wa nchi yetu sio mambo ya josephine as a person and her weakness
  Yesu aliwaambia wale makuhani na watu mbalimbali waliyemletea yule mama aliyezini kuwa sheria inasema apigwe mawe mpaka mauti impate, lakini bwana YESU hakuhukumu alicho waambiia ambaye anajiona kuwa yeye hana hatia awe wa kwanza kuinua jiwe na kumpiga lakini baada ya mda mchache kila aliyekuwepo alijipeleza na kugundua hata yeye ana hatia mbele za mungu! Tujipeleleze kabla ya kuhukumu wengine na tuuache unafki,
   
 19. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
 20. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,197
  Trophy Points: 280
  Mbona wewe mke wako ni sandakalawe hatusemi ni PM nikupe namba yake ya simu. Tatizo lako hujui mtu unayemtetea ana ugonjwa ule mkuu unamtafuna ndani kwa ndani anaishi kwa Probability.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...