Mke wa Bro anajenga ghorofa kimya kimya

Mke wa Bro anajenga ghorofa kimya kimya

Tatizo sio ujenzi wa nyumba. The issue is: Breach of Trust.
* Kama kuna kizunguzungu duniani ni zoezi la kujenga trust - atabidi apigane kama anaona sababu ya kuipigania ndoa na familia yake
* Tatizo ni mawazo yanayoenda mbali : kwamba inakuwaje sikujua wala kuhisi haya mambo
* Kama haya yanaendelea - ni yapi mengine ambayo siyajui?

Ninachoweza kusema ni hivi: Mambo kama haya huwa hayatokei mara moja - yanaanzaga na wizi wa vocha hadi kukua na kuwa ujenzi wa jumba zima
 
Brother ana mke wake (mmachame) wana miaka 8 ya ndoa sasa na wana Nyumba yao mitaa fulani hapa Dar.

Sasa juzi amekutana na rafiki wa mke wake akawa anampa hongera ''shemeji kweli nimekukubali ile njenge unayodondosha kule mbezi ni majanga, nawewe ulipata mgao wa escrow nini'' bro akawa anashangaa huku anasema mbona mi sina nyumba nyingine, huyu best akazidi kumwaga data, si kule ambapo mke wako huwa anasimamia.

Bro ikabidi awe muwazi kuwa sifahamu lolote kuhusiana na hilo jambo please naomba tupangesiku nikapaone, sasa ameenda amekuta mjengo wa hatari. Floor mbili zishakamilika na alikuta siku hiyo mafundi wakipaua vigae.

Bro alipata pressure, mpaka muda hajamuuliza mke wake, haelewi pesa katoa wapi maana hana hata uwezo wa kununua uwanja mke wake anapesa za voucher na kuendea saloon tu.

Bro anasema anasubiria aone mwisho wake itakuwaje, japo hana amani kabisa muda huu.

By: SUPU YA MAWE
Duuh
 
Kuna mmama nilimuona ana akili sana.

Mafundi wao walikutana nae na kumwambia ile nyumba yenu walishaweka fremu za milango na magrili dirishani tumeanza kupiga plasta. Ila sijawahi kukuona ukija kukagua zaidi ya mzee tu na dada yake.

Mke akajiongeza fasta hana wifi eneo hilo. Huo utakuwa mchepuko unajengewa nyumba. Mke fasta akawaambia mafundi kesho ntakuja kukagua.

Kesho yake mke kaenda na fundi milango kapima mlango wa mbele na wa jikoni. Siku nne milango ipo tayari na ya tano ikaenda kupachikwa mafundi wanamalizia plasta vyumbani. Jioni mke kawa wa mwisho baada ya mafundi kutoka na kafunga nyumba. Karudi nyumbani na kukabidhi funguo kwa watoto. Walikuwa wakubwa, mkubwa akiwa na miaka 21.

Mume kufika jioni wanasalimiana na kukaa sebuleni na watoto, mke kaanzisha mada. MUME WANGU KWENYE ILE NYUMBA YA MAHALI XXXX, NIMESHAWEKA MILANGO YA NJE BADO YA VYUMBANI TU, FUNGUO NIMEWAKABIDHI WATOTO MTAENDA KUMALIZIA. Mume hakujibu kitu.

Mpaka leo ile nyumba ni ya familia na hapakuwa na ugomvi wala majibizano😎

Huwa nampa hongera sana huyu mmama, mdogo wake na rafiki yangu. Hekima nyingi.
 
Back
Top Bottom