Mke wa balozi Daraja auawa; Mfanyakazi wa nyumbani atafutwa

- Sijui sheria za Tanzania kuhusu uchunguzi wa mauaji kama haya, maana za majuu the husband automatically anakuwa the first suspect, sasa sijui sisi Tanzania.

- Majuu wanaangalia kama mume alikuwa na vimada, alikuwa na mapenzi ya kweli na mkewe, I mean wanaangalia mengi sana ambayo yanaweza kuwafikisha kwenye the truth, tena kesi nyingi za namna hii ukiangalia huko majuu huamuliwa na circumstantial evidence na waume wengi wameishia kupatikana guilty, si unajua criminology ndio mambo yangu. Bwa! ha! ha!

Resepct.

FMEs!
 
Pole sana familia ya Daraja. Msiba huu unasikitisha sana kutokana na jinsi ulivyotokea. Nawaombea Polisi kila la kheri katika jitihada za kuwatia hatiani wahusika wa mauaji hayo.
 
Hivi huu utaratibu wa "jina limehifadhiwa" kwanini unatumika katika kila kesi/ tukio linalohusisha polisi/ waandishi wa habari?

Kama mtu anatafutwa halafu tena jina linahifadhiwa, wananchi watasaidiaje katika upatikanaje wa huyo mtu?

Naelewa kuwa baadae jina la mtuhumiwa hapa limekuja kutajwa, lakini nadhani sasa huu utaratibu umevuka mipaka.
 
mwanakijiji vipi ndugu yangu wewe na Daraja mna ugonvi usiokwisha,anyway unachosema kinaleta sensi kidogo,binafsi namfahamu mama ni mtu mzuri sana,mungu amlaza mahala pema peponi
 
mwanakijiji vipi ndugu yangu wewe na Daraja mna ugonvi usiokwisha,anyway unachosema kinaleta sensi kidogo,binafsi namfahamu mama ni mtu mzuri sana,mungu amlaza mahala pema peponi

Houseboy !
Unahusishwa na haya mauwaji uko wapi niisaidie polisi? Teh teh teh teh
 
Houseboy !
Unahusishwa na haya mauwaji uko wapi niisaidie polisi? Teh teh teh teh

Massa, jana tumewabipu. tumempiga mtu dala kwa tairi. Back to the issue: This might be beyond the theory behind the 'houseboy'. The driver and the widower might also need to 'help the police'
 
Massa, jana tumewabipu. tumempiga mtu dala kwa tairi. Back to the issue: This might be beyond the theory behind the 'houseboy'. The drive and the widower might also need to 'help the police'

Now we are talking.. Kwa sababu hawa jamaa ndiyo wametoa hiyo decoy story ya msaidizi wa nyumbani na mara moja polisi wetu na wenyewe wakaanza kumtafuta huyo na kumtangaza...
 
Kwa wale wanaopenda conspiracy theories ala James Hadley Chase ngoja niongeze mkaa kwa moto. Nasikia miongoni mwa wale wanaogombea kiti anachogombea balozi Daraja ni balozi wetu wa Zimbabwe ambaye aliwahi kuwa kamanda wa polisi vile. I am out!
 
I know Adadi Rajabu.. ambaye intelligence sources at my disposal inadai mwanga unaommulika siyo mzuri. Siyo kwenye suala hili (as far as I know) ila kwenye mambo mengi tangu akiwa DCI.. Ndiyo maana take yangu ya kwanza nilisema.. something is not right..

Kwamba auawe muda mfupi baada ya kupewa taarifa kuwa mumewake anarejea nyumbani is not coincidental (in my humble and untrained opinion). Kama kuna mtu alitaka kufanya kitu angeweza kufanya within the three weeks ambazo balozi hakuwa nyumbani.. why wait until he is on his way back?
 
Mwanak,
Inategemea ni nani au wangapi walijua balozi was on his way back. Kumbuka alisema alimpigia mama simu kuwa narudi kesho. Sasa who else beside mama alijua hilo?
 
Jasusi

Ulikuwa wapi mkongwe tunawahitaji majasusi kushika majasusi wenzao.
 
Swahiba wa ‘muuaji' wa mke wa Balozi akamatwa
Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 9th March 2010

HabariLeo

POLISI mkoani Kinondoni imemkamata mfanyabiashara aliyempeleka kijana anayetuhumiwa kumuua mke wa Balozi mstaafu, Andrew Daraja, kufanya kazi katika familia hiyo.

Anna aliuawa usiku wa Jumamosi iliyopita na baada ya mauaji hayo, kijana aliyekuwa akifanya kazi nyumbani hapo kwenye bustani na kutunza bata, James Mabakuri (22), alitoweka.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, alimtaja mfanyabiashara aliyempeleka Mabakuri nyumbani kwa Balozi kuwa ni Majiga Masanga (27), anayemiliki duka katika eneo la Kimara Temboni.

Kulingana na maelezo ya Balozi Daraja kwa gazeti hili juzi, wameishi na Mabakuri kwa takribani miezi minne kabla ya tukio hilo. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana msibani hapo, Masanga aliwahi pia kufanya kazi kwa Balozi, akaacha kazi.

Baadaye alimpeleka kijana huyo kuchukua nafasi yake. "Huyu kijana bado hatujamkamata lakini tumemkamata aliyempeleka kufanya kazi hapo," alisema Kamanda na kusema Masanga anashikiliwa ili kuisaidia Polisi wakati harakati za kumsaka kijana huyo zikiendelea, baada ya kutoonekana tangu mauaji hayo yalipogundulika.

Akielezea matokeo ya uchunguzi uliofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kamanda alisema marehemu aliuawa kwa kuchomwa kisu mara tatu; viwili karibu na kitovu na kingine chini ya titi la kushoto.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuchukuliwa hospitalini Muhimbili leo jioni kupelekwa nyumbani kwake, Kimara Temboni. Kesho baada ya mtoto wake wa kiume anayeishi Marekani kuwasili, mwili utaagwa kabla ya kuendelea na utaratibu wa kuusafirisha kwenda Muheza, Tanga kwa maziko.

Mauaji hayo yalitokea Jumamosi iliyopita na wauaji waliiba takribani Sh milioni mbili baada ya kupekua chumba cha Balozi. Balozi Daraja alikuwa safarini wakati mauaji hayo yakifanyika.
 
Swahiba wa ‘muuaji’ wa mke wa Balozi akamatwa
Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 9th March 2010

HabariLeo

POLISI mkoani Kinondoni imemkamata mfanyabiashara aliyempeleka kijana anayetuhumiwa kumuua mke wa Balozi mstaafu, Andrew Daraja, kufanya kazi katika familia hiyo.

Anna aliuawa usiku wa Jumamosi iliyopita na baada ya mauaji hayo, kijana aliyekuwa akifanya kazi nyumbani hapo kwenye bustani na kutunza bata, James Mabakuri (22), alitoweka.

wanajuaje aliuawa "usiku wa Jumamosi"? Kwanini isiwe kati ya mchana na jioni ya Jumamosi kama kauli ya Balozi ilivyoashiria.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, alimtaja mfanyabiashara aliyempeleka Mabakuri nyumbani kwa Balozi kuwa ni Majiga Masanga (27), anayemiliki duka katika eneo la Kimara Temboni.

Kulingana na maelezo ya Balozi Daraja kwa gazeti hili juzi, wameishi na Mabakuri kwa takribani miezi minne kabla ya tukio hilo. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana msibani hapo, Masanga aliwahi pia kufanya kazi kwa Balozi, akaacha kazi.

Baadaye alimpeleka kijana huyo kuchukua nafasi yake. “Huyu kijana bado hatujamkamata lakini tumemkamata aliyempeleka kufanya kazi hapo,” alisema Kamanda na kusema Masanga anashikiliwa ili kuisaidia Polisi wakati harakati za kumsaka kijana huyo zikiendelea, baada ya kutoonekana tangu mauaji hayo yalipogundulika.

Kama kila mtu ambaye amewahi kumpeleka au kumuunganisha mtu kwenye ajira atakamatwa na kushikiriwa kwa sababu aliyeajiriwa anatuhumiwa kufanya uhalifu kwenye ajira yake basi tutaanzisha mtindo mpya kabisa wa kusimamia haki. Watu wanaanza kuwa guilty not even by association but by recommendation! Its ridiculous.

Mauaji hayo yalitokea Jumamosi iliyopita na wauaji waliiba takribani Sh milioni mbili baada ya kupekua chumba cha Balozi.
Balozi Daraja alikuwa safarini wakati mauaji hayo yakifanyika.

That is what they told us!
 
And now this,

*Kikwete atuma rambirambi (Mwananchi)

Fidelis Butahe

JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limeomba ushirikiano kutoka kwa wananchi ili kusaidia kumkamata mtu anayetuhumiwa kumuua mke wa balozi mwandamizi wa zamani wa Marekani, Andrew Daraja.

Anna Daraja, mke wa balozi huyo, aliuawa juzi nyumbani kwake Kimara Temboni kwa kuchomwa kisu kifuani na mtu ambaye anatuhumiwa kuwa ni James Mabakuri, 22, ambaye alikuwa mhudumu wa shamba.[/quote]

Nani anamtuhumu,.. soma hapa chini. Inaonekana ni magazeti tu ndiyo yenye kumtuhumu na Polisi.

Kaimu kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Charles Kenyera alisema kuwa polisi wamekuwa wakimfuatilia mtuhumiwa tangu tukio hilo litokee lakini hawajafanikiwa kumpata mtuhumiwa.

Watoke hapa, kwani walifanikiwa kiasi gani kumpata dereva aliyesababisha ajali ya Waziri Salome Mbatia? au wanafikiri tushasahau?

"Tangu litokee tukio hili la mauaji tumekuwa tukimtafuta mtuhumiwa kwa kuwa yeye alikuwa akiishi katika nyumba ile na baada ya mauaji hakuonekana na hajulikani yuko wapi," alisema Kenyera.

Labda waache kumuita mtuhumiwa kwanza.. hata ningekuwa mimi kama sikufanya hivyo na katika mazingira hayo na kila mtu ananiita mtuhumiwa nitatimka! Mmesahau "The Fugitive"?

"Tunaomba wananchi wanaomfahamu kijana huyo pamoja na mwajiri wake kushirikiana na Jeshi la Polisi ili tuweze kumkamata... nasema hivi kwa kuwa polisi hatuwezi kumfahamu bila kuwepo kwa ushirikiano kumpata itakuwa kazi ngumu, tunaamini kuwa malengo yake yalikuwa ya kinyama."

Polesi acheni ushamba; acheni kumuita mtuhumiwa, hakikisheni usalama wake, na mumtie moyo huko aliko kuwa atapata nafasi ya haki ya kuelezea upande wake. Huko aliko huyo kijana kama hakuhusika na anajua kilichotokea asijitokeze hadi Polisi wabadilishe kumuona ndiye mhusika wa mauaji!
Kamanda Kenyera alisema kuwa Februari 14 mwaka huu Balozi Daraja alimuaga mke wake kuwa anasafiri kwenda Muheza, Tanga na kumuacha na mhudumu wa shamba ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo.

"Balozi Daraja aliporejea alifika getini na kugonga geti, lakini hakuna mtu yeyote aliyefungua ndipo dereva wake alipoamua kuruka uzio na kwenda kufungua mlango lakini alipoingia ndani alikuta mwili wa marehemu ukiwa gereji huku kisu kikiwa kimechomwa kwenye titi, mpaka sasa hatujafanikiwa kwa lolote ila tunamshuku huyu kijana kwa nini atoweke baada ya kutokea mauaji,"alisema Kenyera.

Excuse me.. what about the phone call kuwa Amb. Daraja alipiga kutaarifu ujio wake. Simu ya marehemu imepatikana?

Vyombo vya habari jana vilimnukuu kamanda wa polisi wa Kinondoni, Elias Kalinga akisema kuwa baada ya kuhakikisha mama huyo amekufa, mtuhumiwa alifanya upekuzi kwenye nyumba hiyo, ikiwa ni pamoja na chumba cha balozi na kuiba kiasi cha Sh2 milioni na kutoweka kusikojulikana.

Haiingii akilini. Yaani, anamuua mtu halafu ndio anatafuta kama kuna fedha? Au alishajua kuwa zipo fedha ndio akafanya hicho kitendo? Lakini on the other hand, kama huyo kijana alikuwa anataka fedha tu, na yuko na huyo mama angeweza kabisa kuiba hizo fedha na kutoweka bila kuua? don't you people use some neurons!?

"Tunatarajia kuondoka Alhamisi kueleleka Muheza kwa mazishi kwa kuwa kijana wangu atafika kabla ya siku hiyo. Huyu kijana ninamshuku ila siwezi kusema kuwa yeye ndio aliyeua lakini akipatikana na uchunguzi ukafanyika ndio ukweli itajulikana," alisema Daraja.

what what what?? kumbe Balozi Daraja hamtuhumu mtumishi wake kuwa ndiye aliyefanya kitendo hicho? so kwanini Polisi wanafikiria hivyo? Change the strategy you morons! Mnampa muda muuaji au wauaji kujificha zaidi!
 
Mwkjj,

Not really, hiyo ni mbinu ya kumfanya kijana ajisikie "hahusiki" na then kujitokeza nyumbani ili ahudhurie mazishi .... of course we all know what will happen kama akijitokeza hapo.
 
Mwkjj,

Not really, hiyo ni mbinu ya kumfanya kijana ajisikie "hahusiki" na then kujitokeza nyumbani ili ahudhurie mazishi .... of course we all know what will happen kama akijitokeza hapo.

basi ni mbinu mbaya.. ya kumtaja kuwa ni muuaji halafu aje msibani?
 
Back
Top Bottom