Mke ni nani? Rafiki au ndugu?

Mke ni nani? Rafiki au ndugu?

Mi nadhani mke anastahili zaidi...kua na mume anaekuona/kuita pepo si mchezo!
Ni kweli mke anastahili, bt ukute hajui kama mwenzie anamwona ni pepo! Mh, hii kali mke kuwa pepo afu bado uendelee kuishi nae, yawezekana kweli jamani??
 
Mke ni zaidi ya Ndugu, Rafiki. Ataitwa mke/mume hawezi kuwa mjomba, babu, kaka, dada, baba wala mama etc. Kama ubavu wa mwanaume alitolewa mwanamke leo hii unamuitaje adui? Ki ulewa zaidi ebu soma Kitabu cha mwanzo chote sitaki uache sura wala msitari. Utapata maana ya mke/mume.

Ubarikiwe sana.
 
Mke si ndugu na wala si rafiki. Biblia inatuambia kuwa mke na mume ni mwili mmoja

"Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake na aambatane na
mkewe; na hao wawili wata kuwa mwili mmoja"

Matayo 19:5
 
Mke ni chanzo cha matatizo. Sio ndugu yako wala rafiki yako. Ukioa tu, urafiki na washkaji unaharibika kama hauko stable. Pia undugu huvunjwa na wake zetu.
Pole kwa lolote lililokukuta lililosababishwa na mkeo, usijumuishe wote kiranja mkuu
 
Mke ni zaidi ya hao wote acha mchezo kabisa mtu unalala nae kitanda kimoja anakujua kuliko mama yako mzazi, anajua hadi harufu ya ....yako. zaidi ya hayo mnaunganishwa na watoto, aiseeeeee! ndoa na iheshimiwe na watu wote
 
Ni kweli mke anastahili, bt ukute hajui kama mwenzie anamwona ni pepo! Mh, hii kali mke kuwa pepo afu bado uendelee kuishi nae, yawezekana kweli jamani??

Ndoa ndio sehemu pekee ambapo maadui wawili hulala kitanda kimoja
 
Mke si ndugu na wala si rafiki. Biblia inatuambia kuwa mke na mume ni mwili mmoja

"Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake na aambatane na
mkewe; na hao wawili wata kuwa mwili mmoja"

Matayo 19:5
Huu msemo huwa unanitatiza sana kwa nini mwanamume anaambiwa awaache baba na mama yake aambatane na mkewe ndio maana wazazi wa mke bado wanakuwa benet kwenye ndoa ya mtoto wao au vipi embu baelezee
 
Sijaelewa swali ama km nimeelewa basi mantiki yake imenipotea...aliyeuliza swali nafikiri alikua na jibu hivyo si vibaya akaweka naye jibu lake ili tusitoke nje ya mawazo yake!...Maswali mengine bwana!
 
Hebu elezea kidogo unavyojua wewe
Rafiki ni nani?
Ndugu ni nani?

Usinitie katika majaribu. Nimeuliza swali kwa kuwa mimi nimekosa majibu
 
Sijaelewa swali ama km nimeelewa basi mantiki yake imenipotea...aliyeuliza swali nafikiri alikua na jibu hivyo si vibaya akaweka naye jibu lake ili tusitoke nje ya mawazo yake!...Maswali mengine bwana!

acha kunirushia mpira, wajibika kwa sehemu yako
 
Back
Top Bottom