Mke mwema hutoka kwa Mungu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke mwema hutoka kwa Mungu.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sangari, Oct 31, 2012.

 1. S

  Sangari Senior Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 172
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wakuu ni hivi: mimi ni mwanaume, umri wangu ni 30yrs. Mwaka jana mwanzo nikiwa nyumbani kwangu nawaza jinsi nitakavyopata mke wa kumuoa, alikuja mwanamke 1 mjamzito. Akanikuta niko kwa nje dukani kwangu akaniomba apumzike kidogo kwani alikuwa amechoka na amechomwa na jua. Wakati huo ilikuwa mida ya saa 9 mchana na jua lilikuwa kali sana. Nilivyomuangalia kwa makini, alikuwa na ujauzito wa kama miezi 6 kwani hata dalili za tumbo zilionekana. Nilimkaribisha akaweka kibegi chake chini akaniomba maji ya kunywa nikampa akamaliza. Akawa anahema kwa kasi sana, nikamuliza kulikoni dada mbona unahema kwa kasi sana au unaumwa? Alinijibu 'kaka ninasikia njaa sana'. Kulingana na hali alokuwa nayo, nilistuka kidogo. Kwa haraka nikamwambia kuna karanga, mkate, biscuits, juic, popcorn.nikupe kipi kati ya hiv unywe na soda?akasema natamani juic na karanga lkn sina hela. Nikamwambia nakunulia mimi. Basi akapokea akala, mwisho akanishuku sana kwa kusema 'Mungu akuongezee'. Nakumbuka nilimuliza dada unaelekea wapi? Ndopo story kamili ilianza...........DADA: ''Mimi naitwa Jesca Justin Limo, ni mzaliwa wa Moshi Marangu. Hapa nilipo sijui naelekea wapi manake wazazi wangu wamenifukuza nyumbani baada ya kuona mimi ni mjamzito. Nilienda kuanza chuo kikuu Iringa mwaka jana mwezi wa tisa, huku nyumbani nilikuwa na rafiki yangu wa kiume ambaye ndie alienipa huu ujauzito. Kumbe nilipoondoka tayari nilikuwa na ujauzito wa wiki1. Kufika chuoni nilianza kujisikia vibaya na kuanza kuumwa ovyo na kutaapika. Nilijitahidi kuvumilia hadi nikamaliza semista ya kwanza. Nilirudi nyumbani, kufika nikapokelewa na wadogo zangu. Kufika ndani na kukutana na wazazi wangu na kuniuliza nini kimenitokea. Nilivaa ujasiri na kuwaeleza, ghafla mama alizimia na baba akaingia ndani na kuchukua bastola aniue. Wadogo zangu walipiga makelele majirani wakaja baba akawa amerudisha bastola ndani. Mama alipozinduka yeye na baba walinifukuza nyumbani kwa ukali sana nikaondoka kulala kwa jirani. Wakati huo yule kijana alishanikana toka mwanzo na baadhi ya dada zake walokuwa wanifahamu walianza kunitukana kwenye cm na huyo kaka alikuwa masomoni Kampala Uganda. Hapa nilipo sina pa kwenda natafuta tu mahali nikae nifanye hata kazi ya kufua nguo nipate kuishi.'' Wakati huo ni saa 11 jioni. Nilimuita balozi wangu ambaye tunaishi nae jirani, nikamweleza, akahojiwa akatoa maelezo ya kutosha. Nilimuonea huruma sana. Kwa sababu nilikuwa na nyumba yenye vyumba vya kutosha, balozi pamoja na uongozi wa kijiji waliniomba nimpatie hifadhi kwa siku 1 ili kesho yake tuweze kuwasiliana na wazazi wake. Tuliwapigia simu wazazi wake wakasema hawataki kusikia kitu kama hicho. Uongozi wa kijiji waliniomba niendelee kumtunza huyo dada na lolote litakalotokea watakuwa tayari kupambana nalo. Wadogo zangu 2 kike na kiume nilokuwa naishi nao waliridhia jambo hilo kuwa aendelee kukaa hapo nyumbani na nisimdai chochote. Siku zikasogea, tarehe ya kujifungua ikafika. Kabla ya kumpeleka hospital niliutarifu uongozi wa kijji wakanipa go ahead na niliwachukua kina mama 2 walompeleka hospitali. Siku hiyo iyo usiku wa saa 2 alijifungua salama mtoto wa kiume. Nilimchukua nikamrudisha nyumbani kwangu nikamuomba huyo mama 1 awe namwangalia kila cku na kumpa huduma pale atakapohitaji. Kesho yake niliamua kuwapigia wazazi wake simu na kuwaeleza yote yaliyotoke na jinsi mtoto wao ninavyoishi nae. Wakati huu wazazi wake walikubali kupokea simu na kuongea na mimi vizuri sana. Walikubali pia kuongea nae na kukubali kumsamehe. Ila hawakutaka kuja kumuona wala kumchukua. Niliendelea kutoa huduma hadi mtoto akawa na umri wa miezi 7 bila kumfikiria kwa lolote. Siku 1 mdogo wangu wa kike akaniambia 'kaka muoe huyu dada kwani hakuna mwanamke utakaempata mzuri na mwenye heshima kama yeye pamoja na kuwa ana mtoto'. Niliwaza sana nikasema huyu mdogo wangu amewaza nini. Siku chache baadae nikamtania ivi 'tukiona itakuwaje' alinibu ivi 'nitakuheshimu na kukupenda milele' Hivi ninavyoandika haya maneno tayari tumeshaoana na nimezaa nae mtoto ana miezi 4 na wazazi wake wamenikubalia. Ananipenda, nampenda. Wazazi walikuja wakaombana msamaha, mambo yakawa sawa. Wazazi wake wananipenda kupita maelezo. Bahati mbaya mimi na wadogo zangu ni yatima. Ndoa yetu idumu milele. Ameni. NI STORI YA KWELI KABISA.
   
 2. Gogo la choo

  Gogo la choo JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 714
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Bro weka paragaph basi maaana hata kusoma tunashindwa sasa..ila ngoja nitafute miwani ya bia mbili ili nikija ndo ntaelewa vizuri..!!
   
 3. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mhhhh. Hongera.. Mshukuru Mungu kwa kukupa mke.
   
 4. epson

  epson JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 508
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  What a coincidence, looks like your a generous person maisha mema kaka na Bwana awe nanyi daima.
   
 5. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongera sana mkuu, hata mimi bado nasubiria Madam X, Kaunga, Lara1 na wengine wa huku Jf wafukuzwe kwa namana hiyohiyo nami nijibebeee taratiibu.
   
 6. T

  Tetra JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nimejifunza kitu kwa ajili ya maisha yangu.
  THANKS na MUNGU AIBARIKI NDOA YENU.
   
 7. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  safi sana mdogo wangu, Mungu awabariki zaidi na zaidi na aidumishe ndoa yenu, hapo umepata mke nawe kweli
  ulikuwa dume!
  Sasa mambo ya nondoz itakuweje tena au bado mnafarijiana kwanza!!!!
   
 8. Lateni

  Lateni JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 685
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Hongera sana , story yako imenigusa, kila la heri sangari.
   
 9. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,123
  Trophy Points: 280
  Hongeraaaaa! ILA WOTE WANAKUWAGA WAZURI MWANZONIIII!!!!!!!!!! Im jst saying!!!!
   
 10. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hongera. Jitahidi basi umuendeleze kielimu sio unamzalisha tu mtindo mmoja.
   
 11. nipeukweli

  nipeukweli JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  hongera sana mdau, quite a lesson to take from the story...binti aendelee na shule huyo.
  ...hainihusu ila nina hamu sana nije kujua yule poyoyo alomkana ataishiaje...
  nasubiri part two...mhhhh
   
 12. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  hongera sana, huo ndiyo uanaume umeokoa maisha ya huyo mkeo, nahisi atakuthamini siku zote kuliko ndugu mwingine yeyote, nawalaumu wazazi kumfukuza binti, piga picha isingekuwa wewe ingekuwaje?
   
 13. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hongera sana wanaume ndo wewe
  sio wengine wanataka bikra?
  bikra ni roho yako
  unatafuta bikra kuna mtu anakaa bikra milele?
   
 14. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Hongera. Ila ka ukijua ex wake ana access mda wote. Ni kumwambia tu,, sasa...tujikumbushie basi...

  Chezea watoto wa kike wewe.
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  congrats
   
 16. Mshawa

  Mshawa JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 711
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Hah hah hah... hivi ya kwako uliipotezea wapi vile...?
   
 17. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  ninayo bado! but unaweza kuoa hata changudoa akawa mke mzuri tu
  si unaona jamaa kachukua mjamzito barabarani na wako vizuri
   
 18. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,215
  Likes Received: 10,559
  Trophy Points: 280
  Hongera zako mkuu...mkono mtupu haulambwi..
   
 19. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,215
  Likes Received: 10,559
  Trophy Points: 280
  Nilitaka kusahau! vipi na masomo anaendelea nayo?
   
 20. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  gud!Mungu awabariki sana !
   
Loading...