Mke mlevi na mpenda starehe!

Unaweza kumpa ngumi akafa bure, bora yaishe, unampiga red card aende zake kwani mlizaliwa wote bana. As time goes on, time will heal your broken heart though its tough to move on but it better than sleeping with a broken heart.
 
kuwa kichwa cha nyumba hakujumuishi kumchapa mwanamke makofi.... in boxing parlance, that's hitting below the belt...

mahali pa kuadhibu inabidi incase hana utii, na kwa hili siyo dhambi kwani mwanamke mwenyewe kashindwa kujiheshimu.
 
haya maajabu tupu. Swali moja tu, ALILIZOA WAPI zigo zito namna hiyo? Ajipange upya fasta.
 
Jana nilikuwa napata mbili tatu za baridi na jamaa yangu, katika maongezi akaniambia hana furaha ya ndoa yake. Mke wake ni anapenda pombe, analewa na watu mbalimbali anawaita 'friends', hana muda hata wa kutandika kitanda wanacholalia. Chumba chao dada wa kazi ndo anafagia, anafua, kupika na hata kutunza mtoto kwani mama hurudi mtoto akiwa amelala.

Pia kila sherehe anataka kwenda, amediriki kwenda hata kwenye Kili Awards bila ya kumshirikisha mumewe. Alipomuuliza anasema alikuwa na kaka yake, tatizo yote hayo hata ukoo wao wanapenda pombe sana. Kabila la wapenda pombe nadhani mnawajua wale wazee wa migombani walivyo!

Tatizo ni kwamba jamaa amechoka, mwanamke hashauriki, kaomba msaada hata kwao waongee na binti ila haijasaidia. Wana mtoto mmoja, jamaa ndio anahangaika kuwahi nyumbani japo akae na mtoto. Amefikia maamuzi ya kutaka kuachana na mkewe, jamaa ni msomi mzuri na ana kipato cha kujitosheleza, mke pia pamoja hana elimu ila ameweza kuendesha biashara ambayo mumewe alimuanzishia na inaendelea vizuri.

Tatizo mke ni mtu wa starehe za kulimbukia kwani wakati wanakutana hakuwa hivyo tena walikuwa na muda wa kukaa pamoja na kushauriana.

Nimeshindwa cha kumueleza japo nami nikaona labda mnaweza kutoa mchango wowote.

Hapo kwenye bold kijani
 
mahali pa kuadhibu inabidi incase hana utii, na kwa hili siyo dhambi kwani mwanamke mwenyewe kashindwa kujiheshimu.

Katika hili utii haupo, kushindwa kutandika kitanda,
Kunilaza njaa na watoto,
Kunifanya niwe karibu na housegirl.
Nini ... kisa mapombe! Huyu ni wadis tu!
 
Jana nilikuwa napata mbili tatu za baridi na jamaa yangu, katika maongezi akaniambia hana furaha ya ndoa yake. Mke wake ni anapenda pombe, analewa na watu mbalimbali anawaita 'friends', hana muda hata wa kutandika kitanda wanacholalia. Chumba chao dada wa kazi ndo anafagia, anafua, kupika na hata kutunza mtoto kwani mama hurudi mtoto akiwa amelala.

Pia kila sherehe anataka kwenda, amediriki kwenda hata kwenye Kili Awards bila ya kumshirikisha mumewe. Alipomuuliza anasema alikuwa na kaka yake, tatizo yote hayo hata ukoo wao wanapenda pombe sana. Kabila la wapenda pombe nadhani mnawajua wale wazee wa migombani walivyo!

Tatizo ni kwamba jamaa amechoka, mwanamke hashauriki, kaomba msaada hata kwao waongee na binti ila haijasaidia. Wana mtoto mmoja, jamaa ndio anahangaika kuwahi nyumbani japo akae na mtoto. Amefikia maamuzi ya kutaka kuachana na mkewe, jamaa ni msomi mzuri na ana kipato cha kujitosheleza, mke pia pamoja hana elimu ila ameweza kuendesha biashara ambayo mumewe alimuanzishia na inaendelea vizuri.

Tatizo mke ni mtu wa starehe za kulimbukia kwani wakati wanakutana hakuwa hivyo tena walikuwa na muda wa kukaa pamoja na kushauriana.

Nimeshindwa cha kumueleza japo nami nikaona labda mnaweza kutoa mchango wowote.

huyu sio mke jaman mpeni jina jinginee sababu hicho ni kitu kingine kabisaa..MKE ni yule anayejua majukumu yake kama mke kinyume na hapo apewe jina jingine.......pole kwa huyo kaka aendelee kumpa somo labda atabadilika na kua mke sasa.
 
Jana nilikuwa napata mbili tatu za baridi na jamaa yangu, katika maongezi akaniambia hana furaha ya ndoa yake. Mke wake ni anapenda pombe, analewa na watu mbalimbali anawaita 'friends', hana muda hata wa kutandika kitanda wanacholalia. Chumba chao dada wa kazi ndo anafagia, anafua, kupika na hata kutunza mtoto kwani mama hurudi mtoto akiwa amelala.

Pia kila sherehe anataka kwenda, amediriki kwenda hata kwenye Kili Awards bila ya kumshirikisha mumewe. Alipomuuliza anasema alikuwa na kaka yake, tatizo yote hayo hata ukoo wao wanapenda pombe sana. Kabila la wapenda pombe nadhani mnawajua wale wazee wa migombani walivyo!

Tatizo ni kwamba jamaa amechoka, mwanamke hashauriki, kaomba msaada hata kwao waongee na binti ila haijasaidia. Wana mtoto mmoja, jamaa ndio anahangaika kuwahi nyumbani japo akae na mtoto. Amefikia maamuzi ya kutaka kuachana na mkewe, jamaa ni msomi mzuri na ana kipato cha kujitosheleza, mke pia pamoja hana elimu ila ameweza kuendesha biashara ambayo mumewe alimuanzishia na inaendelea vizuri.

Tatizo mke ni mtu wa starehe za kulimbukia kwani wakati wanakutana hakuwa hivyo tena walikuwa na muda wa kukaa pamoja na kushauriana.

Nimeshindwa cha kumueleza japo nami nikaona labda mnaweza kutoa mchango wowote.

Aangalie alipo jikwaa c alipoangukia,alifanya mistake ktk uchaguzi wa mke,kumbe alijua familia wanywaji alitegemea nn?
 
Mambo ya kupigana kwa mimi hapana, lakini nayo hasira inaweza kufanya maamuzi yake. Tumeshapigana sana ngumi za utotoni mashuleni hivyo katika utu uzima huu haifai.

Mke akikuuzi ni kuachana nae tu na wala usiogope kugawana nae mali, kitu pekee ambacho kinaweza kunipa shida kuachana na mke ni pale tu tunapokua na mtoto wa chini ya miaka saba, hapo naweza vumilia kuwa naye without tendo la ndoa.
 
pombe ni adui wandoa na kama unabisha si kwa wanaume wala si kwawanwke maana ukinywa akili inashindwa kujizuia kuwa hili ni mbaya au nizuri yote unaona mazuri na ndio mwanzo wa kugonoka bila hata mpiara
 
Nigomba iko mbeya, iko bukoba, iko tarime, ni wa wapi hao jamani?

Mie niacha kwa msomaji kujua mwenyewe, kwa sababu halikuwa suala la msingi katika hii post, cha msingi ni tabia yake. Tatizo watu wanachokoza ili wapate kuanzisha maneno yao ya ukabila. Im not there my friends. Chagueni wenyewe itakuwa kabila gani. Mie sihusiki.
 
Mambo ya kupigana kwa mimi hapana, lakini nayo hasira inaweza kufanya maamuzi yake. Tumeshapigana sana ngumi za utotoni mashuleni hivyo katika utu uzima huu haifai.

Mke akikuuzi ni kuachana nae tu na wala usiogope kugawana nae mali, kitu pekee ambacho kinaweza kunipa shida kuachana na mke ni pale tu tunapokua na mtoto wa chini ya miaka saba, hapo naweza vumilia kuwa naye without tendo la ndoa.

Yani mkae miaka yote bila tendo la ndoa ndani ya nyumba moja kisa unasubiria mtoto afike miaka saba? Hapo utakuwa unataka tu wewe, je siku mkajikuta mmeongea vizuri, jamaa akapika msosi, akakutaniatania pale japo umenuna, akanunua a bottle of wine, unadhani akikukumbatia what will happen next? Na hujachangamsha damu muda mrefu na hapo kadamu kameshachemka mwili umekuwa wa moto, lips za moto? Weeeeewe, usilete utani aisee! Hapo kitanda kitavunjika, kama ni sebuleni, makochi lazima yachanike wewe!
 
Rafiki yako kuna sehemu kakosea kama alimuanzishia biashara je alifuatilia mapato ya biashara? Na pia inawezekana amebadilika kutokana na kampani aliyo nayo au pia aina ya biashara anayoifanya kiasi cha mapato nacho kikiwa kikubwa bila udhibiti ni tatizo hasa kama mwenye kufanya hiyo biashara akili zake ziko kistarehe zaidi.Kama tangu mwanzo wa biashara angekua anafuatilia mapato na matumizi pia kukaa pamoja inapopatikana nafasi na kupanga mipango ya familia sidhani kama hayo yangefika huko jaribu pia kuangalia upande wa rafiki yako naamini kuna sehemu nae kateleza kimajukumu kama MLEZI na MKUU wa familia
 
Back
Top Bottom