Mke mlevi na mpenda starehe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mke mlevi na mpenda starehe!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bondpost, Jun 3, 2012.

 1. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Jana nilikuwa napata mbili tatu za baridi na jamaa yangu, katika maongezi akaniambia hana furaha ya ndoa yake. Mke wake ni anapenda pombe, analewa na watu mbalimbali anawaita 'friends', hana muda hata wa kutandika kitanda wanacholalia. Chumba chao dada wa kazi ndo anafagia, anafua, kupika na hata kutunza mtoto kwani mama hurudi mtoto akiwa amelala.

  Pia kila sherehe anataka kwenda, amediriki kwenda hata kwenye Kili Awards bila ya kumshirikisha mumewe. Alipomuuliza anasema alikuwa na kaka yake, tatizo yote hayo hata ukoo wao wanapenda pombe sana. Kabila la wapenda pombe nadhani mnawajua wale wazee wa migombani walivyo!

  Tatizo ni kwamba jamaa amechoka, mwanamke hashauriki, kaomba msaada hata kwao waongee na binti ila haijasaidia. Wana mtoto mmoja, jamaa ndio anahangaika kuwahi nyumbani japo akae na mtoto. Amefikia maamuzi ya kutaka kuachana na mkewe, jamaa ni msomi mzuri na ana kipato cha kujitosheleza, mke pia pamoja hana elimu ila ameweza kuendesha biashara ambayo mumewe alimuanzishia na inaendelea vizuri.

  Tatizo mke ni mtu wa starehe za kulimbukia kwani wakati wanakutana hakuwa hivyo tena walikuwa na muda wa kukaa pamoja na kushauriana.

  Nimeshindwa cha kumueleza japo nami nikaona labda mnaweza kutoa mchango wowote.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Amuite akaenae chini hilo sio tatizo lakuwacha mke..
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  anawaita 'friends'.....lol

  kweli mfumo jike umeshika hatamu lol
   
 4. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Amuite amuweke kitako,areason kama baba mwenye nyumba,politely but with strong msg.amuambie kuazia leo sitaki ufanye Abcd na unatakiwa ufanye qrst.period.
   
 5. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  The Boss, unajua jinsi wanawake wa siku hizi walivyo! Yani jamaa anatamani amchape makofi ila nimemwambia itakuwa kujidhalilisha kama alishaongea na wazazi wa binti na bado haelewi, then kama hana furaha ya ndoa ampe hamsini zake akalewe vizuri.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kabla ya kutoa talaka
  siku moja amchape makofi kweli na atoe amri marufuku kwenda popote leo
  aone...

  wanawake wengine 'bila makofi haoni kuwa yupo na mwanaume'
  anaona yupo na shostito wake...
   
 7. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  kumbe walioanzisha utaratibu wa ndoa za mikataba hawakukurupuka..
   
 8. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Uko sawa kabisa, ila hapo juu nimeshaeleza mpaka anafikia kuniambia hayo yanayomsibu ni kuwa ameshaita wazazi wa binti na kuwaeleza yote hayo. Kumbuka hata unyumba anapata kwa manati kwani mwanamke mlevi unajua akija anatega tu umalize tena kama hatandiki kitanda i guess hata kule maeneo ni kuchafu. Huwezi jaribu kwenda chumvini japo mkewe ni mrembo ila anatabia mbaya. Pia huwezi jua hao 'friends' kama hawajapita hapo!
   
 9. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Aliapa kanisani siku ya ndoa yao kwa shida na raha,ndo shida zenyewe hizo..pole yake!
   
 10. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha! Aisee umenichekesha ila umeongea kiume ile ya ukwelikweli, dah. Hii naipeleka kama ilivyo kwa kweli. Its true unajua mtu kamtoa mbali, alitoka huko kwao akija kusoma certificate pale magogoni, anakaa kwa mjomba jamaa akafika bei kiukweli binti alikuwa ametulia nasi tulimpa support ya kuwa yule ndiye wife material sasa after three years, jamaa hana furaha ya ndoa! Ila ni kweli siku ampe kibano, honestly, huo ushauri naupeleka kama ulivyo.
   
 11. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ushauri wa kijinga! Akimchapa makofi akimpeleka mahakamani ujue atafungwa huyu mshikaji, kwani kumpiga mke ni shambulio ambalo ni kosa la jinai. Yeye cha kufanya aende kwa waliowasimamia ndoa au atafute watu anaoheshiana nao wawasuluhishe, ikishindikana watafute ndugu zao wanao heshimiana wawashauri, ikishindikana aende kanisani (kama ni waislamu waende kwa mashehe) wakawashauri, na ikishindikana pote, namshauri jamaa aende mahakamani ampe talaka ikiwa bado mapema!!
   
 12. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  duh, unaweza kwenda chumvini kumbe friends wameshashushia mizigo mle ukaishia kunywa 'uji'
   
 13. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Umestukia eeh? Sasa raha ya ndoa unadhani ataipata vipi.
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mkuu
  chunguza sana utagundua kuna watu 'hawaendi polisi au mahakamani'
  au popote pale kushtaki...
  ukiwaona huko ujue wanashitakiwa na sio kushitaki
  sometimes in life we choose to be victims or not.....

  wote wanaopigana barabarani au kuwapiga wake zao na waume zao
  wangepelekwa kushitakiwa 'pangekuwa hapatoshi'

  ukifuata sheria hata kumpiga mwanao ni kosa
  kuongea matusi hadharani ni kosa

  akili mu kichwa....
   
 15. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  Wakati huyo mwanamke anaenda kili awards bila kumtaarifu mumewe, yeye mume nae alikuwa wapi?
  Just like it takes two to tangle, maybe it takes the same two to untangle. Si ajabu mwanamke ana-respond kwa frustrations za mwanaume, just a second thought...
   
 16. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Hapana mamii, hizo shida wakipata wanawake mbona huwa mnawaambia watoke kwenye ndoa? Mshkaji anampenda mkwewe ila hana furaha kwenye ndoa, do u think hapo kuna usalama kweli? Naturally he becomes vulnerable, atakuja kupata maukimwi bure mie hata suala la nyumba ndogo nimeshindwa kumpa support kwani hayo yanahitaji maamuzi yake.
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  mmmh, umenikumbusha mama jafari lol

  mke akishakuwa mpenda pombe jua keshakuwa cha wote, kuna mama jirani yangu lol, pombe zimekolea hadi akakimbia kwake na kwenda kuwa 'muuza vocha' machimboni.

  Alianza hivi hivi.
   
 18. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Tulikuwa kikazi Arusha, na muda huo kuanzia saa tatu likuwa hotelini, akawa anampigia ili aongee na mtoto hakupokea mpaka saa sita usiku ndo kumpigia. Wakati huo alijaribu kupiga simu ya mlinzi akamuomba apeleke ndani ndipo mlinzi alipomuambia kuwa mkewe hayupo. Hiyo second thought yako naifuatilia lakini najaribu kudhani kuwa unataka kumtetea binti kwa namna fulani, hebu chambua tena. Huyu ni mshkaji niliekuwa nae toka utotoni na hana mambo ya kurukaruka. Alikuwa hanywi pombe, sasa ameanza kupata viglass vya wine. In short iangalie story tuchangie kwa mlengo huo! Thanx.
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  The best way to stop smoking is to never start.

  Hivi hizi ndoa za siku hizi hazina kipindi cha uchumba kuchunguzana na kujuana tabia kabla ya kuoana? Najua kuna kuficha makucha and all, lakini kama mtu ni extreme kiasi hiki chances are ata slip na kumpa mtu yeyote observant reason to pause.

  Words to the wise, msikimbilie kuoa.

  Kama vipi mna chill kwenye Kiranga's Club of Perpetual Bachelors for Eternal Balling.
   
 20. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kuwaambia jamaa zangu fulani kuwa mke chapombe hana ujanja wa kujisitiri mbele ya wakware lazima tu watajifanya 'friends' kumbe unatafutiwa siku yako zitakapokupanda mpaka ushindwe kutembea ndo utasikia 'lup'.
   
Loading...