Foxhound
JF-Expert Member
- Dec 15, 2013
- 28,740
- 76,384
Salaam wana jukwaa pendwa, nisiwachoshe twende kwenye mada.
Jana usiku majira ya saa 2 kasoro maeneo ya huku kwetu Gomz umeme ulikatika, sasa nikajaribu kumuuliza mmoja kati ya marafiki zangu wa kike ambae haishi maeneo haya, kuwa maeneo anayoishi yeye umeme upo! Nilimuuliza kwa njia ya whatsapp, baada ya kunijibu nilimtakia usiku mwema na mimi akanitakia.
Sasa kwa vile ndani ilikuwa joto sana ikanibidi nitoke nje ya nyumba nilikaa hapo hadi kufikia saa 4 umeme ukawa bado haujarudi, nikaamua niingie ndani nijipumzishe sebuleni kwa vile jana ndio nilikuwa nimerudi toka kwenye mihangaiko ya kutafuta maisha, nilikuwa najisikia uchovu sana, hivyo pale nilipojipumzisha nimekuja kushtushwa na ubaridi kwenye saa 8 usiku, kumbe wife alikuja na kunimwagia maji ya baridi toka kwenye friji then ye akaingia chumbani.
Nikajinyanyua ili nami niingie kushika mlango, kumbe tayari umefungwa kwa ndani nilikaa pale kama nusu saa nikitathmini kilichonitokea kama ni kweli Kwa vile nimejawa ujasiri nikafungua mlango wa nje na kwenda kuingia chumbani kwa kupitia dirishani, wakati naingia mke wangu alitaharuki kwa kudhani ni kibaka nikamtuliza na kulala hadi asubuhi sasa hiyo kufika asubuhi ndio ameondoka na kuacha watoto ushauri wenu jamani, nifanye/nimwambie nini ili arudi.
Povu ruksa lakini sio matusi.