Mke kama msaidizi wako

Mke kama msaidizi wako

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
1,977
Reaction score
2,216
Mwa 2:18
BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Mk 10:8
na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.

Kila mtu ana maamuzi yake na mtazamo wake na mapenzi yake na uhuru katika kufanya mambo yake bila kupangiwa na mtu yeyote ila hutofautiana uwezo n wengine HUSHINDWA kabisa kukabiliana na kuhimili kustahimili MATOKEO ya hayo maamuzi au machaguo yao.

Kupanga ni kuchagua..
hapa kuna machaguo makuu mawili moja mke kama msaidizi wako na mke kama asiye msaada kabisa kwako

faida za kuwa na mke kama **msaada kwako ama msaidizi wako.
1)UPENDO-- upendo ni sawasawa na kutoa ,unaposema unampenda mtu maana yake ni lazima utoe kwa ajili yake ,umpe kitu..mfano wa upendo unaanza na Mungu mwenyewe...

Yn 3:16-17
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee

mwanamke ambaye yupo tayari kutoa kwa ajili ya familia kwa ajili yako huyo ana upendo.

kama wewe mwanaume unaoata milioni 2 na mke wako anapata milion 2 basi hapo kwenye familia hesabu una milioni 2 ya kwako peke yako tu,ya mwanamke usihesabu?ni sawa lakini kama ana upendo ni rahisi kwa yeye KUJIONGEZA kwa upendo wake na hiyari yake mwenyewe si kwa lazima..

na kama mke hana kazi kabisa ni mama wa nyumbani,si vibaya ukampatia mtaji akafanya kashughulu kadogo kadogo akapata hata vijisenti vya kwake vidogo vidogo,hata kwa ajili yake mwwnyewe sio lazima kila kitu anachohitaji akuombe mumewe suku nyingine aombe mtaji wa biashara au aombe wazo la biashara au aombe kupewa elimu ya ujasiriamali maarifa elimu ya ujuzi fulani.
na sio lazima mpaka aende chuo anaweza kujifunza kwa waliofanikiwa au hata mtandaoni ili naye afanye shughuli yeyote ya kuingiza kipato.

2)KUNA LEO NA KESHO
Siku hazifanani siku ikulitokea mwanaume umefeli umeanguka aunumeyumba kiuchumi au umeitwa umetwaliwa duniani. au umeumwa upo kitandani unaugua ??

3)KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWA.
Mnaposaidiana wote wawili katika familia mnapunguza ukali na ugumu wa maisha uliopo.

N;B
Uzinzi na kukosa uaminifu ni tabia binafsi ya mtu ,kama mwanamke ni mzinifu na muasherati asiye mwaminifu..KUMZUIA ASIFANYE SHUGHULI/KAZI yeyote na kumfungia ndani ya geti,au kumpa mahitaji yake yote anayoyataka ,HAITAMBADILISHA.

Na kumruhusu afanye shughuli kazi yeyote ya kuingiza kipato kadhalika haitambadilisha tabia yake.
Mwanamke ni kama bahari huwezi kulinda bahari watu wasiogolee by the time wewe unalinda koko beach wengine wanaogelea kawe au kigamboni,huwezi kumchunga kama mbuzi.Akiamua kukusaliti hata kama unemfingia ndani atakusaliti tu.

DALILI ZA HATARI UTAZIGINDUA UTAKAPOMCHUMBIA.

1) anapenda vitu vya bei kali..hajui BAJETI..matumizi ya hovyo ya ufujaji...MATUMIZI MAKUBWA.
Kama wewe ni milionea au bilione sio issue ila kama ni mwanaume unayejitafuta unayetegemewa na familia yako wazazi wako na wadogo zako.

2)Ukimpa mtaji wa BIASHARA ndogo ndogo mfano milioni 3 au 5 au hata milioni 1...MTAJI ANAULANUNAISHA halafu ukiangalia alichofanya hakuna na wala haoni tatizo,unarudia kumbadilishia kwa kujaribu biashara tofauti tofauti hata mara 5 yote ni yale yale mtaji unaisha bila kuona matokeo ya alichofanya.

3)Hana mawazo ya kufanya maendeleo ,hana mawazo ya ya

4)KAMA ana KIPATO hana mawazo ya kufanya maendeleo ya pamoja ,KIPATO CHAKE ni chake na KIPATO CHAKO ni CHENU WOTE .

5)DHARAU hii ndio hatua ya mwisho ya juu kengele ya hatari/RED FLAG .ukishaona mwanamke wako amefikia hatua ya kukudharau kwa namna yoyote hiyo ni kengele ya hatari.

6)UAMINIFU

Mara nyingi mwanamke ana penda kweli akikupenda sio rahisi kukusaliti.Hasa kama ana 7) hofu ya MUNGU


Kwa sisi wanyonge wanaume wa halu ya chini tunaojitafuta ni vizuri ukaoa mwanamke ANAYEKUPENDA sio lazima awe PISI KALI mana uzuri wa mwanamke sio urembo ni wema wake KINDNESS au tabia njema.
Ni vizuri uka fall in love na mind yake kindness yake utu wake kuliko mwenye kuvutia kwa uzuri wa muonekano wa nje ,utakaompa kiburi na dharau kwa vile wengi wanavutiwa naye ama hulka yake malezi yake na tabia yake binafsi ikawa ni ya UKAIDI,KIBRI,DHARAU,MAJIVUNO

wananawake wenye upendo wa kweli kwako ambao wanapenda kwa moyo wote bila kujali hali yako kwa shida na raha wapo ukitazama kwa mtazamo wa jicho la ndani utawaona wapo hawajaisha.
Isipokuwa kwa muonekano wa nje wanaweza wakawa wakawaida wasiwe na muonekano wa kuvutia sana kwa nje kama wanavyovutia kwa utu wao wema wa ndani na moyo safi walionao.

kipindi cha uchumba ni kipindi kizuri cha kusomana,vitu vingine MUNGU AMETUPA akili vipo ndani ya uwezo wetu na maombi kidogo tu,una macho ya rohoni na mwilini pia uana akili ,kama UKITUMIA AKILI yako katika kumchagua msaidizi wako badala ya kiongozwa na tamaa ya mwili ikiyowakanna muonekano wa nje pekee utamisi uzuri wa ndani ambao ni muhimu kuliko uzuri wa nje.

SHETANI PIA kwa muonekano wa nje huyu LUCIFER ni mzuri sio kama anavyochorwa kwa picha lakini ni mwizi,baba wa uongo,mchinjaji na muharibifu..ni nyoka..

You are always beautiful when you kind,kindness is thing which make one beutiful and not the out look.

Nawaelewa wanaosema KATAA NDOA

UKIPATA MWANAMKE pasua kichwa lazima upige mayowee kwa nguvu..atakunyosha kweli...usifanye permanent decision based on temporary pleasure.

Usifanye maamuzi ya kuoa kwa kuongozwa na tamaa ya nje peke yake ..TUMIA AKILI badala ya HISIA katika kila jambo .ndio sababu ya Mungu kukupa akili ili uitumie usiangamizwe kwa kukosa akili/maarifa kama matokeo ya maamuzi yako iliyoyafanya mwenyewe.

Maana ya UPENDO NDIO HII

upendo huvumilia,hautafuti mambo yake wenyewe,haukosi kuwa na adabu, haujivuni,hautafuti mambo yake wenyewe(selfishness changu changu chako chetu)...,unakuwa na huruma,n.k

Kwa mwanaume katika suala la kupata mwenza kwa mimi naona hakuna kitu kibaya kama KULAZIMISHA kupendwa na mtu ambaye anakuonyesha kabisa hakupendi,yani kumuonyesha mwanamke kuwa huwezi kuishi bila yeye na kuwa pamoja na dharau anayokufanyia lakini wewe unamuonyesha huna mbadala wake...huna option nyingine zaidi ya kujipendekeza usipopendwa.
 
1 Kor 13:4-8
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote

UKIPATA mwanamke wako ana UPENDO kwa maana hii ya upendo utakuwa umepata chema hata kama kwa muonekano wa nje hana muonekano mzuri kuzidi wengine .

Mit 18:22 SUV
Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA

utakuwa umepata kitu chema

ila kinyume cha hiyo utakuwa umepata matatizo..mwisho wa siku utakuja kilia kwa nguvu hapa na kusema KATAA NDOA
 
sijasoma gazeti lote ila naomba kuuliza uzi wako uko upande gani kati ya Biashara, uchumi au ujasiriamali

Au umekosea road ulilenga upeleke MMU
 
Ni kumwomba Mungu akukutanishe na mwanamke sahii!, wengi wao walioa wake wema mwanzoni ila walivofika ndani wakabadilika wakaanza kuota mapembe na kutaka kumtawala mme kwa kila kitu!.
 
Ipo tofauti kubwa mno ya life partner na msaidizi
mwanamke ni sehemu ya mwanaume ,kiroho ,ADAMU aliumbwa akiwa na nafsi zote ndani ya mwili mmoja yani mwanamke na mwanaume ndani ya mwili wa ADAMU.
Baadae zikawa separated mwanamke kutoka kwa mwanaume (HAWA).
Hawa wawili ni partner kila mmoja ni part ya mwenzake flesh of my flesh mifupa kutoka mfupa wangu.

na hawa wote wamekuwa mwili mmoja ,ni kitu kimoja.

unajua mwanaume na mwanamke wote wana homoni za kike na za kiume ila kwa viwango tifauti na kuna wakati anaweza kuzaliwa kiumbe chenye jinsia zote mbili hermaphroditis kama wale wanyama au mime ambayo inajizalisha yenyewe ni dume na jike hapo hapo.
japo asili ni moja katika umoja japo ni kitu kimoja ila tumetenganishwa mke na mume tofauti kwa sababu maalumu ya kusaidiana ,tunaunganishwa kuwa kitu kimoja mume na mke.
KUSHIRIKIANA na KUSAIDIANA
na UMOJA kwa sababu mume na mke ni wamoja asili wameumbwa kila mmoja kwa ajili ya mwingine na wanaposhirikina kibiolojia kiroho wanakuwa tena mwili mmoja.
WASHIRIKIANE na KUSAIDIANA kwa UMOJA wao kimwili na kiroho na kiakili.
 
Hv mkiweka 50% ya mume na mke 50% kwenye kila jambo kuna athari gani ?

Vipi ambao hawaeki hizo percent na bado inakula kwao imekaaje hapo ?

Je kwann mwanamke akumbatie Mali zake tena kwa Siri bila mume kujua Ila mwanaume ukiwa nazi wanaanza hivi ukifa ghafla,
 
unazizingatia point zao lakin mkuu? eti msaidizi wa kibiashara 😅😅😅
Kwa watu wanyonge wachini vijana maskini kabisa wanaoishi chini ya 5000 kwa siku,ambao bado hawajipata ,hata watumishi wa umma wa kada za chini,kisaidiana kiuchumi ni point pia ..
japo kwa ma wakiojipata kiuchumi haiwezi ku make any sense.
 
Back
Top Bottom