Mke hufurahia mume anapougua

Mke hufurahia mume anapougua

The CIA

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2017
Posts
479
Reaction score
479
Habari wana jamii. Kwa muda mrefu kidogo nimekuwa nikijaribu kuchunguza hili suala kama ni kweli ama siyo na kama ni kweli sababu ni nini.

Ninegundua pasi na shaka kuwa mke hufurahia sana anapoona mume wake anaumwa, hasa anapolazwa hospital japo wiki moja hufurahia zaidi.

Katika kufurahia kwake huambatana na maombi ya nguvu sana ya kumuombea mumewe apone,

Hivyo basi anapofurahia mumewe kuugua haimanishi anamchukia balada yake kuna suala la maslahi yake binafsi pamoja na internal forces ambazo hata yeye ushindwa kuzicontrol zikiongozwa na sababu zifuatazo:-

1. Huamini ndo wakati rasmi wa kuonesha upendo kwa wazazi na ndg wa mumewe walioko mikoani,
hilo huambatana na simu nyingi huku akijinasibu hasinzii usiku kucha(hata kama anasinzia) kwa siku kadhaa na anajaribu kupambana ili mumewe apone haraka,
automatically wazazi na ndg wa mume hata mama mkwe humuongezea credit mwanamke huyo kwa kupigana, kuokoa maisha na kumjali mwanae.

2. Huamini ndo wakati muafaka wa kumuonesha mumewe upendo uliotukuka kwake,
hili halitaishia hapa, baada ya kupona kila atakachoforce kupata atakiamba na ugonjwa wako na kuonesha wewe haumjali wakati yeye anakujali sana kupita kawaida.

Asanten kwa kunisikiliza,.
nakaribisha
maoni, mapendekezo, dukuduku, maandamano, n.k


Updates.
Baadhi ya magonjwa tuyaache constant,
mfano HIV, CANCER, and the rest of this nature.
 
Inategemea mume anaumwa nini mkuu, kuna magonjwa mengine daktari anakupeleka kwenye chumba kwa maongezi ukitaka huko na wewe pia ni mgonjwa
Fafanua, unatoka una positive?
 
Uchunguzi wako ni fake,
Hakuna mwanamke anafurahia kuona mumewe anagua Eti ndio atumie oportunite hiyo kuonyesha upendo kwako na nduguzo. Ila ni wajibu wake kukuhudumia kwa Hali zote kwa shida na raha, na ndio maana cku ya ndoa yenu huwa munaulizwa unamkubali mwenzako kwa shida na raha?
Kwa hiyo cyo anajipendekeza hapa ila ni wajibu wake kwa vile alimwacha mama,baba,na ndugu zake na akaja kuungana nawe na mukawa mwili mmoja.
 
Hivi Mkuu unajua kuuguza wewe? Kuuguza kunachosha labda kama utauguza ugonjwa wa malaria ambayo unajua akitumia Anti Malaria siku 2 tu ameshanyanyuka tena,hapo kweli utafurahia lakini si kuuguza ugonjwa mkubwa uliomkamata mumeo kisawa sawa! Huwezi kufurahia huwezi kucheka wala kutabasabu muda wote utaumia na utalia maana ni muda ambao unaweza jikuta unapokea lawama nyingi ambazo usipokua makini na usipokua mtu wa imani basi zitakukatisha tamaa!
Niliuguza mume wangu mwaka huu huu baada ya kuteguka nyonga,hakika nikipata mateso sana ya mwili na moyo ! Maana mgonjwa mwenyewe kuna muda anakutia hasira kwa kukupa lawama ambazo pengine hazikua zinakustahili.
Usiombe kuuguza kwa kweli hasa sisi watumishi kazini unatakiwa kwa mgonjwa unatakiwa yaani lazima uchanganyikiwe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom