aj styles
Member
- Feb 9, 2017
- 17
- 14
Bwana mmoja alisafiri kwenda kijijini, alipofika akakuta mtandao wa simu unapatikana bila matatizo. Akamwandikia mke wake sms. Kwa bahati mbaya akakosea namba na ikamwendea mtu mwingine ambaye alikuwa ni mwanamke mjane. Yule mjane baada ya kuisoma akaanguka na kuzimia! Mwanae kuona vile akachukua simu na kusoma kilichomfanya mama yake azimie. Iliandikwa hivi:
MKE WANGU MPENZI, NAJUA UTASHANGAA KUONA SMS HII. HUKU NAKO KUNA MTANDAO KAMA HUKO. MIMI NIMEFIKA SALAMA NA MATAYARISHO YA WEWE KUJA HUKU KESHO NIMEYAKAMILISHA NA HIVI NAKUSUBIRI SANA KWA HAMU HONEY!
MKE WANGU MPENZI, NAJUA UTASHANGAA KUONA SMS HII. HUKU NAKO KUNA MTANDAO KAMA HUKO. MIMI NIMEFIKA SALAMA NA MATAYARISHO YA WEWE KUJA HUKU KESHO NIMEYAKAMILISHA NA HIVI NAKUSUBIRI SANA KWA HAMU HONEY!