Mke apewa kichapo baada ya kumjibu mumewe matusi kupitia JF

Midavudavu

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
287
59
Mke na mume walikuwa wanatumia computer Moja. walikuwa hawajuani kumbe kila mmoja ni mwanachama wa JF na kila mmoja alikuwa anatuma threads zake ktk jukwaa la utani. Mke baada ya kutuma thread yake akasahau ku log out; mumewe aliporudi toka kazini akakuta computer iko wazi na threads kibao zimetumwa kwa jina ..........Akagundua kumbe mkewe ndiye mwanacha wa JF mwenye jina la........(Jina limefichwa kwa sababu za Maadili). Mume akagundua kuwa mwana JF mwenye jina hilo aliwahi kumtusi kutokana na thread aliyo post. Basi akamsubiri hadi mkewe aliporudi na kumpa kipondo cha nguvu kwa madai ya kumtusi kupitia jukwaa la JF. Hivi sasa ndoa yao iko shakani; angalieni lugha tunazotumia katika jukwaa hili wakati mwingine unaweza kuwa unamtusi mzazi wako au la azizi wako kama ilivyo kwa wanandoa hawa. Ni Habari ya kweli na wala si uzushi, kesi hivi sasa iko kwa mshenga wa mume.
 
Unajua uzuri ni kwamba tushajua kuwa hili ni Jukwaa la utani.Hivyo kila kinachoandikwa tunafahamu kinamaanisha nini. Sijui kama nimeeleweka?
 
Uzembe ni hatari sana ndio maana Mwl Nyerere aliupinga vilivyo ona sasa kitu kidogo cha ku log out kinavunja ndoa safi sana next time she will become aware!
 
Back
Top Bottom