Mke anadai tuachane mara kwa mara

Mke anadai tuachane mara kwa mara

kwanza naomba kufahamu,mlioana kwa sababu yeye alikuwa mjamzito au toka mwanzo mlikuwa na mpango wa kuoana,mbona ni kama huyo alilazimika tu kuolewa na wewe kwa sababu ya ujauzito na siyo kwa sababu anakupenda, those are empty shells marriages which normally do not last very long....
 
ulimpa mimba 2012 na kuanza kuishi naye na sasa ni 2014 mna watoto 2 hongera sana mkuu!
 
mimi sijawai hata kufikiria swala la kuachana naye nahisi nampenda pili hawa kids sipendi wakose malezi yetu sote

Then Mpuuze,
hayo ni maneno ya "kike" tu, wengi wetu tushatishiwa huyo "nyau!"

Nakutakia ujasiri na uvumilivu Mkubwa katika dhahma hiyo. kwani yaelekea
wewe unampenda na kumthamini mkeo, na kwamba upo tayari kuilinda ndoa yako kwa gharama zote.

Mkeo ni kiumbe dhaifu, la msingi jitahidi kumuonyesha mapenzi zaidi, na hata ikibidi mwambie kauli zake hizo
zinadhoofisha mapenzi, aachane nazo.
 
kwa Kweli nakosa raha sana. uamuzi unakua mgumu kwangu kwaajili ya wanangu

Ndoa inasimamia nguzo Mbili,
#Mapenzi na #Huruma .
Mpaka yatapokosekana yote mawili ndio utasema umeshindwa,
kwasasa simamia kile moyo wako unaamini ndio sahihi.

Usimuache Mkeo.
 
Mkubalie ndio dawa yake. Kadiri anavyokuambia muachane then ukambembeleza ndio ataendelea kukusumbua maana anajua huwezi kukubali na anatumia hio kama silaha/fimbo yake. Na atakuwa keshakujulia unampenda sana na hutaki muachane kwa sababu ya watoto wenu na jina lako pia.

We nenda tu jioni mwambie ''Mke wangu nimekaa nimetafakari naona bora tuachane kama unavyotaka. ukitaka watoto nenda nao au niachie tu'' usiongeze neno nenda kafanye mambo yako mengine....uwe siriazi kweli kweli then uone reaction yake. Sentensi zake tatu za kwanza zishike vizuri...Ndipo ukweli ulipo kama anataka kweli au anatishia.

Nina Jamaa alizaa na dada mmoja, kukawa kuna kitu wametofautiana.. yule binti akamwambia ''njoo chukua takataka yako'' akimaanisha mtoto. jamaa kwa hasira kaenda.. unafikiri binti alikubali? hakutaka kumuachia. akadai lazima nipajue kwenu kwana nione nani atakaa na mwanangu.. jamaa kampeleka, kufika oooh siwezi muacha mwanangu... ''mnajua uchungu wa mwanangu nyie'' then ngoma ikaisha bila bila.

Yawezekana nawe anakuchezea tu akili.. maana mara nyingi huwa hawamaanishi wakisemacho na wakimaanishacho huwa hawakisemi. Mtaalamu Mr Rocky plz leta hekima zako hapa.

Tafadhali kama unamsaliti.... NAKUOMBA kWAROHO MOJA UACHE. WANAO NA FAMILIA YAKO INAKUHITAJI SANA KULIKO UNAVYOJUA.

hapo juu umemaliza kila kitu hana cha kuongezea ila jamaa nae anajitahidi kamuoa 2012 leo 2014 march wana watoto wawili tena sijui ana mimba nyingine ama sijamuelewa vizuri....
 
wakwanza kazaliwa 2011 wapili 2014. Mimi nilimpenda tangu nlipo muona sjui kuhusu yeye. khs ndugu si Kweli kua wanaingilia yeye tu ndo ahisi huvyo

....kuhusu ndugu kuna ka ukweli hapo, maana jamii zetu hizi nazo, mnh!
Usimkatalie kila jambo mkeo analokulalamikia....huenda ndio sababu kubwa anayohisi
humjali wala humsikilizi kiasi kwamba anaona labda akikwambia umuache utamuacha.

Miaka miwili ya ndoa ni muda mfupi sana. Changamoto za ndoa ndio hizi kaka,
ukisikia for better or worse ndio pamoja na haya....
hizi changamoto ni ndogo mon kwako wewe kuanza ku panic....

Mwenyezi Mungu akuzidishie mapenzi kwa mkeo, na baada ya miaka kumi na ushee nawe utasimama kifua
mbele kutoa #Wosia kwa ndugu jamaa na marafiki zako ambao watakuwa wanaingia kwa mara ya kwanza kwenye maisha ya ndoa wakidhania ndoa ni #Lelemama ...

Kila la kheri.
 
naomba ushauri, mimi ni kijana miaka 28 mke wangu umri huo pia. tumeanza kuishi pamoja 2012 baada ya kumpa Mimba. sasa mwenzangu ni jeuri Kiasi na ana wivu sana na sim zangu. Shida kila wakati ataka tuachane, kwasasa anadai ndugu zangu hawampendi na pili mimi ninawasiliana na wanawake sana. Anataka tuachane tuna watoto 2, nimekua nikimuomba aachane na hayo mawazo kwa mda Sasa. Naomba wenye uzoefu nshauri nifanyeje?

Duh! Nyie nanyi!!!! From 2012 hadi sasa 2014 mna watoto wawili? Anyway, kwanza mmefunga ndoa au mnaishi tu (uchumba sugu)
 
imewai tokea Kuna mwanamke tulikua tunawasiliana ila kwasasa hakuna io shida na nilishamweleza

Hapa ndio tatizo lilipoanzia, sisi wanawake baadhi ni wepesi kusamehe ila kusahau inakuwa ngumu.

Muache awe huru na simu yako ili ajiridhishe na unachomwambia! Atakuwa sawa ni hasira za muda tu.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hapa ndio tatizo lilipoanzia, sisi wanawake baadhi ni wepesi kusamehe ila kusahau inakuwa ngumu.

Muache awe huru na simu yako ili ajiridhishe na unachomwambia! Atakuwa sawa ni hasira za muda tu.

....hata ingekuwa yeye ndio kayafumania hayo mawasiliano ya simu baina ya mkewe na mwanaume mwingine,
yangekuwa yale yale ya "ukishaumwa na nyoka,....!"
 
mimi mambo ya kutishana hata sitishiki, na hii inakuja sana ukiwa na misimamo na huweki wazi, na pia ukiwa muovu nje hii inakuwa mbaya zaidi... Tized umenena vyema kaka.....
 
Last edited by a moderator:
Anatishia kujamba tu huyo
akikuambia tena mruhusu mwambie unamtakia kila laheri
atajizungusha huko ndani kama mende haendi popote
 
Mkuu we uko dunia ipi? watu wanazaa chap chap siku izi then wanaanza kuwalea watoto. Kama alimuoa na ujauzito 2012 labda aliupata 2011, 2013 akaweka mwingine. kie kie kie!!!!!

Wengine mtoto wa kwanza 2010, wa pili 2020 wa tatu 2035. what a difference does it make. Bora mtu ukazaa wanao hao watatu ndani ya labda miaka 5 au sita then mkaanza kuwatafutia maisha na pia wanakua kwa pamoja na wazazi nanyi mnapumzika ati. Au Mr Rocky apa unabisha?

hapo juu umemaliza kila kitu hana cha kuongezea ila jamaa nae anajitahidi kamuoa 2012 leo 2014 march wana watoto wawili tena sijui ana mimba nyingine ama sijamuelewa vizuri....
 
Last edited by a moderator:
Asante Mkuu. Hapo kwenye rangi umenikumbusha point muhimu sana. asante

mimi mambo ya kutishana hata sitishiki, na hii inakuja sana ukiwa na misimamo na huweki wazi, na pia ukiwa muovu nje hii inakuwa mbaya zaidi... Tized umenena vyema kaka.....
 
Unaona eeh!!
Bora mimi sijasema. Usikute na wewe huwa unatishia tishia uniambie mapemaaaaa!!!
Ili nisitishe mpango wangu kwako.

Anatishia kujamba tu huyo
akikuambia tena mruhusu mwambie unamtakia kila laheri
atajizungusha huko ndani kama mende haendi popote
 
Then Mpuuze,
hayo ni maneno ya "kike" tu, wengi wetu tushatishiwa huyo "nyau!"

Nakutakia ujasiri na uvumilivu Mkubwa katika dhahma hiyo. kwani yaelekea
wewe unampenda na kumthamini mkeo, na kwamba upo tayari kuilinda ndoa yako kwa gharama zote.

Mkeo ni kiumbe dhaifu, la msingi jitahidi kumuonyesha mapenzi zaidi, na hata ikibidi mwambie kauli zake hizo
zinadhoofisha mapenzi, aachane nazo.

Asante sana mkuu. Ninajitahidi sana kumpenda hata nduguze humweleza hivo ila ni ubishi wake tu.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mkuu we uko dunia ipi? watu wanazaa chap chap siku izi then wanaanza kuwalea watoto. Kama alimuoa na ujauzito 2012 labda aliupata 2011, 2013 akaweka mwingine. kie kie kie!!!!!

Wengine mtoto wa kwanza 2010, wa pili 2020 wa tatu 2035. what a difference does it make. Bora mtu ukazaa wanao hao watatu ndani ya labda miaka 5 au sita then mkaanza kuwatafutia maisha na pia wanakua kwa pamoja na wazazi nanyi mnapumzika ati. Au Mr Rocky apa unabisha?

ohoo mimi si unajua mtakatifu sijuagi hayo mambo ya mimba(mtoto) kabla ya ndoa,kama hivyo basi sawa.
 
....kuhusu ndugu kuna ka ukweli hapo, maana jamii zetu hizi nazo, mnh!
Usimkatalie kila jambo mkeo analokulalamikia....huenda ndio sababu kubwa anayohisi
humjali wala humsikilizi kiasi kwamba anaona labda akikwambia umuache utamuacha.

Miaka miwili ya ndoa ni muda mfupi sana. Changamoto za ndoa ndio hizi kaka,
ukisikia for better or worse ndio pamoja na haya....
hizi changamoto ni ndogo mon kwako wewe kuanza ku panic....

Mwenyezi Mungu akuzidishie mapenzi kwa mkeo, na baada ya miaka kumi na ushee nawe utasimama kifua
mbele kutoa #Wosia kwa ndugu jamaa na marafiki zako ambao watakuwa wanaingia kwa mara ya kwanza kwenye maisha ya ndoa wakidhania ndoa ni #Lelemama ...

Kila la kheri.

Asante sana
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Back
Top Bottom