Mke anadai tuachane mara kwa mara

Mke anadai tuachane mara kwa mara

Hahahaaaa... sio ndio maana huwa mnatuonea sana linapokuja lile swala la Papuchi?

Kwa maana wanaume wanaonekana wapo deperate sana na hio kitu mwanamke anamringia.

Fundi ujenzi mmoja alikua anatupa kisa chake na mkewe akasema alioa mke kule kijijini akamleta mjini. mkewe akabana bana hela ya matumizi na nyingine nyingine akacheza kamchezo gani sijui unaitwa kibati na majirani zake.. ilipofika zamu yake akapokea laki NNE na nusu... kilichofuatia akamwambia mumewe ''sikutaki tena narudi nyumbani' Mume akajua kiburi ni hako kahela maana alikua hajawahi kushika hela nyingi ivo... akamwambia nenda mama. wapi na wapi baada ya wiki mbili kaja kumlilia mumewe? maana vile vihela alienda kujidai kuweka jina kijijini fasta zimeshakauka. kwa kuwa mumewe alikua keshajua ni ulimbukeni wa hela unamsumbua.. akampokea mkewe bahati mbaya jamaa amefariki mwaka jana.

Wanawake hamtabiriki aisee.

Hatueleweki kama hizi nanii zetu kwakweli.....
 
Kabisa Mkuu Bill. Hawa watu wanatabia ya kututingisha tingisha sana. Na bahati mbaya ukatingishika tu... IMEKULA.
Ugumu na kutotabirika ni nyenzo muhimu sana kwa Mwanaume.

ba nso chukua ushauri hapo juu wa Tized hapo juu. Ukiendelea kumbembeleza atakusumbua sana. Siku akikwambia anataka kwenda mwambie sawa we nenda tu mi sina tatizo. Na akifungasha wewe mwache aende. Lakini nakuhakikishia lazima atarudi mwenyewe na hatakaa akusumbue tena.

Nina uzoefu na hicho ninachokuambia ama alichosema TIZED
 
Last edited by a moderator:
....kuhusu ndugu kuna ka ukweli hapo, maana jamii zetu hizi nazo, mnh!
Usimkatalie kila jambo mkeo analokulalamikia....huenda ndio sababu kubwa anayohisi
humjali wala humsikilizi kiasi kwamba anaona labda akikwambia umuache utamuacha.

Miaka miwili ya ndoa ni muda mfupi sana. Changamoto za ndoa ndio hizi kaka,
ukisikia for better or worse ndio pamoja na haya....
hizi changamoto ni ndogo mon kwako wewe kuanza ku panic....

Mwenyezi Mungu akuzidishie mapenzi kwa mkeo, na baada ya miaka kumi na ushee nawe utasimama kifua
mbele kutoa #Wosia kwa ndugu jamaa na marafiki zako ambao watakuwa wanaingia kwa mara ya kwanza kwenye maisha ya ndoa wakidhania ndoa ni #Lelemama ...

Kila la kheri.

Huu ni Wa Busara Sana
 
kwa Kweli nakosa raha sana. uamuzi unakua mgumu kwangu kwaajili ya wanangu
Napata wasiwasi sana na uwezo wako wa kumdu ndoa. Wanao watateseka vipi? Popote walipo unao uwezo wa kuwatunza wasipate shida. Zaidi sana watakumiss wewe baba yao. Mara zote wenye mawazo ya ....kwa ajili ya wanangu..... Ni akina mama. Au unaandika story ukijifanya mwanamke?
 
ni kweli unafanya hayo maswala na ana ushahidi wa usaliti wako?
Kama ni hivo badirika na ufanye kile anachokitaka yaani husiwasiliane na wanawake hovyo pia kama unaishi na ndugu jaribu kuwa mbali nao ili muwe na amani ktk ndoa yenu!
Pole sana kiongozi!

huwezi kukaa mbali na ndugu kisa mwanamke cha msingi aangalie wapi pana matatizo na ajaribu kukaa na ndugu zake kuwaelewesha juu ya kumheshim mke wake pia hata mwanamke mwenyewe awaheshim
 
Naomba ushauri, mimi ni kijana miaka 28 mke wangu umri huo pia, tumeanza kuishi pamoja 2012 baada ya kumpa Mimba.

sasa mwenzangu ni jeuri kiasi na ana wivu sana na sim zangu.

Shida kila wakati ataka tuachane, kwasasa anadai ndugu zangu hawampendi na pili mimi ninawasiliana na wanawake sana.

Anataka tuachane tuna watoto 2, nimekua nikimuomba aachane na hayo mawazo kwa muda Sasa.

Naomba wenye uzoefu nishauri nifanyeje?

bila shaka mlipatana katika michepuko...

kaa na mkeo, kubali kuungama makosa yako endapo kweli kagundua unayatenda..

ukiendekeza mfumo dume, ukikataa neno la mkeo, kumbuka kuna means nyingi tu za kuvunja uhusiano ikiwemo wengine kutumia maamuzi mazito ya kujiondoa duniani...

chukua hatua,... muda ndio huu..
 
Mwanamke siku zote ukimpenda sana mpaka ukaonyesha udhaifu kwake atakusumbua sana kuna jirani yetu mke wake alikua na tabia wakikorofishana kidogo anakwenda kwao jamaa anaenda kumuomba arudi ikawa ndo mazoea ya kila siku ya kutishia kwenda kwao watu wakamshauri apunguze mapenzi kwake afu asiwe anambembeleza anapokua anatishia kwenda kwao siku moja wamegombana jamaa akamyuka mwanamke alipo tishia kwenda kwao jamaa akawa wa kwanza kumpa nauri na kumtorea begi ndani mwanamke alienda paka stand cha ajabu akarudi kuomba msamaha
 
too much love is harmful....

kuna wakati mwanaume inabidi uwe mbogo! sio kila wakati beibe beibe imekujaa tu mdomoni!
 
Back
Top Bottom