Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 869
- 810
Habari ndugu zangu, katika pitapita zangu ndugu yenu leo nimekutana na jambo ambalo kibinadamu siyo la kawaida.
Katika mtaa wa Chem Chem maeneo ya Uyole inapatikana familia ya Mzee SIMONI ROMANUS PELLA .
Mzee SIMONI ROMANUS PELLA anasumbuliwa na ugonjwa ambao umemfanya ashindwe kutembea na kujikuta tangu mwaka jana mwezi wa 12 kuwa ndani tu.
Mwanzoni mzee anadai aliwahi kupata matibabu katika hospital ya Rufaa ya kanda ya Mbeya ambapo alifanyiwa operation ya kibofu cha mkojo na kuwekewa mpira kwaajili ya haja ndogo,lakini baada ya hapo hajawahi kupata matibabu tena mpaka leo hii.
Kinachosikitisha sasa nikwamba mzee wakati akiwa na afya njema alikuwa anamiliki duka katika soko la Uyole jijini Mbeya na ilo duka kwa sasa linasimamiwa na mke wake.
Sasa huyo mwanamke pamoja na watoto hawataki kabisa kuhusika na matibabu ya mzee huyo na kila akijaribu kuomba msaada mke wake hataki.
Mbaya zaidi hawataki mtu yeyote aende kumtembelea wala kutoa msaada wowote kwa mgonjwa
Walijitokeza wasamalia wema kutoka kanisa la KKKT DAYOSISI YA KONDE usharika wa Uyole kwaajili ya kumsaidia kwa kutoa pesa za Matibabu lakini wakamta mke wake akasimamie matibabu hayo hospital kama mtu wa karibu lakini alikataa na kudai hana muda .
Mateso anayopitia mzee huyu ni makali sana muda wote anahaki pekee yake ndani bila msaada wowote.
Wanamuachia chakula mezani huku akiwa na ndoo yake ya kujisaidia pindi akipatwa na haja pembeni
Ndugu zangu mzee huyu anapitia magumu mengi, yaani duka lake lipo ila hawataki kutoa pesa za Matibabu
Kwa leo mwanongwa naomba niishie hapa ila kesho nitakuja na maelezo ya majirani wanaosaidia mzee SIMONI ROMANUS PELLA.