Mke akiri kumsaliti mumewe miaka 7

Mke akiri kumsaliti mumewe miaka 7

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

mahakamaz_300_173.jpg

SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya kulawiti na kutuma picha katika mitandao ya kijamii inayowakabili wakazi wawili wa Mbagala, Dar es Salaam, alidai kwamba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mlalamikaji kwa miaka saba huku akiwa na mume wake ambaye ni mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo.

Sanifa Sadick alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi Saidi Mkasiwa kuwa mshitakiwa Erick Kasira (39) ni mume wake tangu mwaka 2006 na kwamba wana watoto wawili huku mshitakiwa wa pili, Juma Richard ni shemeji yake.

Alidai kwamba Agosti 23 mwaka huu, waliwasiliana na mlalamikaji huyo ili wakutane katika nyumba ya kulala wageni inayojulikana kama Maembe Bar & Guest House iliyopo Yombo Kiwalani kwa ahadi ya kusaidiwa Sh 100,000.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto, shahidi huyo alidai muda wa saa 7 mchana alimuaga mume wake kwamba anaenda kununua bidhaa za saluni.
Alidai kwamba alichukua usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda huku mlalamikaji akimuelekeza kwa njia ya simu.

Sanifa alidai kwamba wakati anaelekea Yombo kulikuwa na mwendesha pikipiki ambaye alikuwa anamfuatilia kwa nyuma hadi eneo hilo.

Alidai kwamba alimkuta mlalamikaji akiwa peke yake na kuagiza kinywaji baadaye walichukua chumba namba sita na kuingia ndani; baada ya muda mlango wa chumba hicho uligonjwa ndipo alimuona mumewe akiingia pamoja na vijana watatu.

''Sikuweza kuwatambua wote lakini hawakuwa na silaha zaidi ya simu. Mpenzi wangu aliulizwa na mume wangu kuwa anafanya nini na mimi, naye alimjibu kuwa asiniache kwani atampa gharama yoyote ndipo waliandikishiana kutoa Sh 500,000 ,'' alidai Sanifa.

Alieleza mlalamikaji kuwa alikuwa na kompyuta na kwamba alimwambia Erick akae nayo hadi atakapompatia fedha hizo walizoahidiana.

Alidai kwamba alikuwa amejificha chooni na kusikia kwamba wanaume hao wanamtaka mlalamikaji afanyiwe kinyume na maumbile na kwamba walimvua nguo zote huku aliyekuwa mwendesha bodaboda akiwa anapiga picha.

Alidai baada ya tukio hilo alikimbilia nyumbani na kukuta simu aina ya Tecno nyumbani kwake na kuiweka laini yake baadaye dada yake alimtumia picha ikimuonesha mlalamikaji akiwa utupu.

Alieleza kwamba mlalamikaji alimpigia simu Erick na kumwambia aende akachukue fedha alizoahidi kutoa wakati akifumaniwa na mke wa mshitakiwa huyo na kwamba mshitakiwa huyo aliondoka pamoja na ndugu yake Richard.

Alidai walipofika Tandika, waliwekwa chini ya ulinzi na Erick alimpigia simu mkewe kumtaarifu kwamba amekamatwa na polisi naye alipofika aliwekwa chini ya ulinzi. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 3 mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa.

CHANZO: Habari Leo
 
Duu miaka 7 mume hakushtuka? saloon inazidi kunawiri tuu!kuna watu wanajua kuhonga yani nitoe 100000 kwa mali used!sijui labda huyu mama ana vitu adimu ktk majamboozi
 
kuibiwa mke si mchezo,wengi wanaua kabisa na sio kulawitiwa halafu uachwe hai, ashukuru mungu wake
 


...Sanifa alidai kwamba wakati anaelekea Yombo kulikuwa na mwendesha pikipiki ambaye alikuwa anamfuatilia kwa nyuma hadi eneo hilo....


...Alidai baada ya tukio hilo alikimbilia nyumbani na kukuta simu aina ya Tecno nyumbani kwake na kuiweka laini yake baadaye dada yake alimtumia picha ikimuonesha mlalamikaji akiwa utupu....


CHANZO: Habari Leo

Hapa pana ukakasi hapajakaa sawa ni kama vile shahidi kalishwa maneno
 
Ama kweli mkuki kwa nguruwe lakini kwa binadamu mchungu na inauma na inachoma kwenye moyo
 
Eti "mume wangu alimuuliza mpenzi wangu anafanya mini na Mimi"

Watu wanaoa aisee...anamuita hawara 'mpenzi' mahakamani...?

Te te te...haya wanaume kazi kwenu...mke akiwa ofisini shida, akiwa mama wa nyumbani tabu...ukimfungulia salon sheeeda...

Sidhani kama akuolewa natabia yake...watu wengine ndo hivyo tena mnaoa makahaba mkidhani wataacha kumbe tabia aina dawa...
 
Huyo mume wa MTU naye anapaswa kuitazama upya performance yake kwenye unyumba, LA sivyo atalawiti wengi

Noo mkuu hapo ni tamaaa huoni mama alitoa papuchi kwa ahadi ya kupewa laki
 
Mumewe angekuwa nayo papuchi isingetolewa,ukiona mkeo anapendeza jiulize ni wewe unagharamia au???TAFAKARI THEN CHUKUA HATUA
Noo mkuu hapo ni tamaaa huoni mama alitoa papuchi kwa ahadi ya kupewa laki
 
Huo utetezi wa huyo mama ni uongo mtupu na umesukwa ili asiunganishwe kwenye kesi ya kusuka hiyo misheni.
Haingii akilini mtu ajue kuwa anafuatiliwa na bodaboda toka nyumbani kwake na bado aingie gesti na mchepuko. Weak!
 
Back
Top Bottom