Mkataba wa Bandari: Tatizo ni kubwa kwa sababu kuna watu wanaamini hawawezi kukosea

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,075
Katika Ulimwengu huu, hakuna mwanadamu ambaye hawezi kufanya makosa, iwe ni kwa bahati mbaya au kwa kukusudia.

Wanaofanya makosa, na wakagundua wamefanya makosa, iwe ni baada ya tafakari yao au kukumbushwa na wengine, nao wakakiri, ndio watu ambao wapo kwenye njia ya mafanikio.

Lakini wapo wajinga, wanafiki na waliokosa hekima, wao huamini kuwa hawawezi kukosea. Hao ndio ambao hata wakifanya makosa, wanashupaza shingo na kuendelea na makosa yao ili tu wasionekane wamefanya makosa.

Suala la ubovu wa mkataba wa hovyo wa bandari, lilikuwa tatizo dogo sana kama waliofanya makosa wangekuwa na dhamira njema. Wangekuwa na dhamira njema, watu walipojitokeza kukosoa vipengere vyenye makosa, wangeshukuru sana, lakini kwa sababu wamekosa hekima, na wanaishi kwenye Ulimwengu wa nadharia unaowafanya waamini kuwa hawawezi kufanya makosa, hata walipooneshwa makosa ya wazi, waliendelea kushupaza shingo ili tu waoneshe kuwa wao hawawezi kufanya makosa.

Badala ya kurudi na kwenda kufanya marekebisho na huyo waliyesaini naye, wao wakaanza ziara za kuwahadaa watu kuwa ubaya ule ulio wazi ndani ya mkataba ndiyo neema kubwa kwa wananchi. Ni sawa na mtu anayekushauri uzame baharini akikuaminisha kuwa huko chini ya maji kuna faida nyingi sana kwa sababu kuna samaki wakubwa wakubwa walionona wapo huko, na wewe utakuwa unajichagulia yeyote aliyenona, kumbe wewe ndiye unaenda kuwa chakula cha samaki.

"Hakuna aliye mkamilifu isipokuwa BABA yetu wa Mbinguni"

Namwomba Rais Samia, kwa namna atakayoiona inafaa na muda unaofaa, aifute kabisa ile kauli mbaya kabisa aliyowahi kuitoa, eti "Rais huwa hakosei". Hiyo siyo kweli hata kidogo. Mataifa mengi yameangamia na yanaendelea kuamgamia kwa sababu ya makosa makubwa yanayofanywa na wakuu wa nchi. Ukiishi katika fikra za kuamini kuwa Rais huwa hakosei, ina maana utakuwa umefunga moyo na dhamira yako katika kupokea ushauri sahihi.

Viongozi wanatakiwa kufahamu, kuwa kiongozi hakukuongezei akili, maarifa na hata hekima. Wewe ni yule yule, huna ubongo mpya ulioupata baada ya kuwa kiongozi. Na hakuna kiongozi hata mmoja, awe ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu au mwingine yeyote awaye ambaye ana akili, maarifa na ujuzi kuwazidi Watanzania wote wakiwekwa pamoja.

Fikra potofu za kuamini kuwa ukiwa kiongozi umekuwa mwanadamu tofauti na wengine, ndiyo zinazowafanya viongozi wengi wa Tanzania kuwa waongo. Ndiyo maana hata Hayati Magufuli wakati anaumwa, wakaficha na kusema uwongo kwa sababu waliona mtu akiwa Rais, ubinadamu wake ni kama umebadilika, yaani hawezi kuumwa wala kufa. Mtu anaumwa, amefariki, watu wanasema uwongo eti yupo ofisini anachapa kazi.

Viongozi kama mtaijiwa na hekima, tokeni hadharani, toeni shukurani kwa watu walioyaona mabaya ya mkataba wa DP, kisha ombeni msamaha kwa kukosa umakini, mwishowe mseme mtafanya nini kwenye hayo mapungufu.

Huu ujinga wa kusema eti kwenye kutoa maoni kuhusiana na mkataba, sijui kuna udini, ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu. Nani atafadika na huo mkataba mbaya kwa sababu ya dini yake?

Viongozi kuzidi kushupaza shingo kuwa eti huu mkataba wa hovyo ni mzuri, kunapeleka ujumbe wa aina moja tu kwa wananchi. Kwamba yale mabaya yaliyomo kwenye mkataba hayakuwa kwa bahati mbaya, hayakusababishwa na uzembe au kukosa maarifa, bali yalidhamiriwa kwaajili ya kujipatia faida binafsi, yumkini walipofushwa kwa rushwa nzito. Hakika mtu yeyote ambaye anaona ni sawa nchi yetu isalimishe mamlaka yake kwa DP, ni adui wa Taifa letu. Siyo dini wala kabila lililomtuma kufanya uasi wa namna hiyo kwa Taifa letu, wala asiifanye dini kuwa tawi la kujishikilia tunapotaka kumvuta asituharibie Taifa.

Mstaafu Rais Kikwete, wengi tunakuheshimu lakini maoni yako kule Rorya ulipotoka sana. Ujitafakari sana. Yaani kauli ya maaskofu inayoonesha upubgufu na ubaya wa mkataba wa bandari iwe ni kuchanganya dini na siasa, lakini ubunge wa Askofu Gwajima au marehemu Askofu Rwakatare isiwe kuchanganya siasa na dini!! Ajabu sana. Nadhani ulighafirika, ukakosa maarifa ya kuona jambo katika uhalisia wake.

Nape anatajwa kuzuia taarifa zozote zinazoonesha ubaya na mapungufu ya mkataba wa DP, zisitangazwe wala kuandikwa na vyombo vya habari. Hapa ndipo inapodhihirisha dhamira na nia ovu ya viongozi kwenye mkataba huu. Nape anataka watu wabakie katika ujinga ili wenye nia mbaya waendelee kuwahadaa wananchi. Watu wa namna hii ni maadui wakubwa wa Taifa letu. Tuwaambie wazi kuwa hawatufai maana wamekuwa laana kwa nchi.
 
Wanajua sana wanakosea, ila wameendekeza matumbo yao tu. Wako tayari kukinukisha ali mradi lao la kupata fedha na mali nyingi lipite.
 
Muda ni hakimu wa haki,huu mkataba miaka 10 au 15 ijayo wakati huo mtu ameshastaafu atajitokeza kuomba msamaha kuwa alikosea ila itakua too late.

Utekelezaji wa mkataba ukianza kung'ata hata wanaoshupaza shingo sasa hivi kutetea viongozi kua ni wenzao hawatakua na la kufanya.

Mbaya zaidi ngozi nyeusi ni kichwa cha panzi miaka hiyo madhara yatakapokua yanatokea watamlaumu kiongozi atakayekuwepo madarakani wanasahau chanzo.

Sakata la gesi Mtwara mwaka 2012/2013 Serikali iliua sana watu ili kufanikisha mradi wa gesi kwa maelezo kua ni mwarobaini wa mgao wa umeme. Leo ni takribani miaka 10 imepita shida ya umeme iko palepale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom