Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Hapo umeshindwa kutofautisha serikali inapata nini kama kodi na shareholders??
Serikali kupata siyo ishu maana kodi lazima ichukuliwe....but shareholders!!!!... ardhi yetu madini yetu...Serikali inatakiwa iwe inanunua share za kutosha hata asilimia zaidi ya 40 ikiwezekana hata kupitia domestic investors....au ingeweka wazi kwamba 40% of share ziuzwe kwa domestic investors ili kuongeza ajira kwa wazawa na transfering of technology. Kuwapa foreigner 80% share hata vyuma vya kujenga madaraja havitapatikana.
Otherwise sioni zitto alienda kusimamia nini pale kama naye hakuona hilo.
Kama uina idea ya masuala ya uchumi nadhani usingeweza kutamka hayo.
Kama umenunua gari kwa milioni 20 kuifanya Cab, halafu unamkabidhi mtu aliendeshe kwa gharama zake mafuta, vipuli nk, halafu we unashinda tu upenuni na kusubiri jioni akuletee mapesa. Kwa vyo vyote 20% ni kubwwa kwako kuliko uliyemkabidhi gari napopambana na mengi mitaani, traffic nk. Jaribu kufikiri kwanza gharama za uendeshaji wa makaa hayo? Kusubiri baadaye wakati tunahitaji kujenga reli kuunganisha bandari ya Mtwara na Mbambabay kiungo na Malawi papo hapo kuiunganisha na Tazara, hapo manufaa ya taifa huyaoni wakati serikali haitatuoa pesa kujenga reli hiyo.
Mjerumani alipojenga reli ya kati serikali ya mkoloni ya wadachi ilipata share kiasi gani? Jibu ni 0%. Lakini reli ndio mkombozi wa usafiri wa walio wengi kwa miaka 50. Ndicho anachokwenda kufanya mchina lakini wengine hapa wanaoni kitu, ni kiza to tolo.